Tafuta Mababu katika Kumbukumbu

Tafuta Mababu katika Kumbukumbu

Kumbukumbu zinaweza kufunua taarifa mpya na kutengeneza njia ya karatasi kwa ajili ya mababu mahsusi.

Mambo ya msingi ya kutafuta mababu

Kuwatafuta mababu zako katika kanzidata ya kumbukumbu za kihistoria kunafanana sana na utafutaji wa Google. Unaingiza kile unachokijua kuhusu kitu fulani unachotaka kukipata. Kisha utafutaji utatafuta kutoka kwenye rundo la data ili kutoa mfanano bora.

Kwa ajili ya utafutaji wa mababu, ni vyema kuingiza taarifa kama jina la mtu na wapi na lini aliishi au kufa. Pia inasaidia kuingiza uhusiano wowote kama vile mwenza, wazazi au watoto.

Ingiza unachokijua au unachoweza kupata kutoka kwa ndugu. Usihofu kama hujui yote, utafutaji bado unaweza kufanyika hata kwa taarifa chache.

Kinachofuata cha kufanya

Kumbukumbu za kihistoria zinakusaidia kukusanya taarifa za hadithi ya familia. Zinaweza kutoa taarifa muhimu au za kuvutia kama anwani, majina ya wanafamilia na maelezo binafsi kama urefu, rangi ya macho na kazi. Unaweza hata kupata sahihi ya mababu zako.

Hifadhi kile unachokipata kuhusu mababu kwenye wasifu wao katika Mti wa Familia. Kile unachohifadhi kitatunzwa na kitashirikiwa kiotomatiki pamoja na ndugu ambao wanaweza kuwa wanatafuta taarifa hiyo hiyo. Taarifa hizi pia ni vyanzo ambavyo vinaweza kuthibitisha ukweli wa maisha ya mtu na kusaidia kuboresha mahusiano.