Tengeneza Mti wa Familia
Jaribu shughuli hizi ili kuanza kutunza kumbukumbu ya matawi ya mti wa familia yako kwenye FamilySearch
Je, mti ni kitu gani?
Ni mkusanyiko unaokua wa vizazi vya familia. Watu kutoka ulimwenguni kote wamekuwa wakiongeza matawi yao kwa zaidi ya miaka mingi sana.
Hatua za kwanza
Ukianza na wazazi wako, ongeza ndugu walio hai na waliokufa kurudi nyuma kwa kadiri uwezavyo. Kupiga simu au kuandika arafa kwa jamaa mzee kungeweza kukusaidia kujaza baadhi ya nafasi zilizo wazi.
Kidokezo: Usihofie kuhusu kuwaongeza ndugu walio hai unapotengeneza njia yako kuwafikia wale waliokufa. Taarifa zote kuhusu watu hai hutunzwa kwa faragha.
Kuongeza watu kwenye Mti
Chagua kitufe cha (+) ili kumwongeza mtu kwenye mti.
Ongeza jina la mtu pamoja na tarehe na mahali pa kuzaliwa na kifo. Chochote unachojua au unachoweza kugundua. Kisha chagua inayofuata.
Unganika kwenye Mti wa jamii wa Familia
Kadiri unavyoongeza majina kwenye mti tutatafuta mfanano. Hivyo, kama bibi yako aliyefariki yuko tayari kwenye mti, tutamtafuta na kutengeneza muunganiko. Kutafuta mfanano ni jambo la kawaida—Mti wa Familia wa jamii umetengenezwa kwa michango kutoka kwa watafiti kote ulimwenguni, iliyoandaliwa kwa miaka mingi.
Tazama vidokezo vya kumbukumbu
Katika kuongezea kwenye utafutaji wa mfanano wa mababu katika mti wa familia, pia tutatafuta mkusanyiko wetu wa kumbukumbu za kihistoria kwa ajili ya mababu waliokufa unaowaongeza. Pale inapopata mfanano, tutakuonyesha “dokezo.” Unaweza kutambua kidokezo kwa ikoni ya rangi ya buluu inayojitokeza.
Fuata kiunganishi ili kwenda kwenye Mti wa Familia na kuanza. Bofya ikoni ya (?) juu ya ukurasa kama una maswali au unataka kujifunza zaidi kuhusu jinsi inavyofanya kazi.
Kidokezo: Rejelea vidokezo kuona kama vina mfanano. Kama ndio hivyo, ni njia nzuri ya kuongeza matawi mapya kwenye mti wa familia.