Mti wa Familia Ulio Mkubwa Zaidi Shirikishi Ulimwenguni

child-on-online-family-tree
ERIN BROOK PHOTOGRAPHY

Tovuti ya bure ya FamilySearch ni nyumbani kwa mti wa familia ulio mkubwa zaidi wa mtandaoni ulimwenguni. Ukijulikana kama Mti wa Familia wa FamilySearch, huu mti wa familia shirikishi ni nyumbanii kwa taarifa kuhusu mababu zaidi ya bilioni 1.2, ambazo zimetolewa na mamilioni ya wazao.

Je, "Mti wa Familia Shirikishi” ni nini?

Mti wa familia uliounganishwa wa FamilySearch unatofautiana na uzoefu wa ujengaji wa mti kwenye tovuti zingine nyingi. Badala ya kukita juhudi kwenye ujengaji binafsi wa miti yao wenyewe, wajengaji wa mti wa FamilySearch wanashirikiana kujenga mti mmoja, shirikishi ambao unakusaidia wewe pamoja na wengine kugundua zaidi kuhusu mababu na wanafamilia wengine.

Wasifu kwa ajili ya Mtu Aliyefariki

Mti shirikishi wa FamilySearch unajitahidi kuwa na wasifu mmoja tu wa umma kwa kila mtu aliyefariki ambaye aliwahi kuishi. Wazao wanaleta kile wanachokifahamu kuhusu mtu kwenye wasifu mmoja, na shikishi, badala ya kutawanya ufahamu wao kwenye wasifu mwingi kwenye miti mingi, ambao baadhi unaweza kuwa na vizuizi vya usiri.

Kumbuka: Kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch, taarifa za akaunti binafsi na maelezo yo yote kuhusu mtu aliye hai hufanywa siri. Ni watu wafu pekee ndio wenye wasifu wa wazi.

Kwa nini Kutumia Mti Shirikishi wa FamilySearch?

Mti wa Familia wa FamilySearch unaweza kukusaidia uunganike na familia yako kwa urahisi zaidi na ujenge historia yako ya familia. Hapa kuna njia tano za jinsi unavyoweza kukusaidia.

  1. Gundua Taarifa Mpya: Mti wa familia shirikishi unaweza kukusaidia ugundue taarifa mpya kuhusu mababu zako na hata kuwapata jamaa ambao ulikuwa huwafahamu. Kila kipande cha taarifa ambacho mtu huongeza—waraka, picha, kumbukumbu, eneo la mazishi—vinaweza kuangaza nuru kwenye utambulisho wa mababu au kwenye mapito ya maisha.
  2. Jenga Mti Wako kwa Urahisi: inaweza kuwa kazi ya kuchosha kujaza kila taarifa ya mababu kwa ajili ya mti wa familia yako wewe binafsi. Unapounganika kwenye mti shirikishi wa FamilySearch, baadhi ya mababu zako yawezekana tayari wana taarifa nyingi kwenye wasifu wao. Hata kama wewe ni wa kwanza kumuongeza babu au bibi kwenye mti shirikishi, FamilySearch inaweza kukuonesha kumbukumbu yamkini za babu au bibi huyo, na wanafamilia wengine wanaweza kukusaidia kwa kujaza kile wanachokifahamu.
  3. Pata Picha Iliyo Kamili Zaidi: Matokeo ya jumla ya mti shirikishi ulio na taarifa na vyanzo vya taarifa hizo yanaweza kuwa kamili na sahihi zaidi kuliko miti binafsi. Japokuwa taarifa zilizoingizwa na watumiaji zinaweza nyakati fulani kutofautiana na kile unachofahamu kuhusu mababu zako, Mti wa Familia wa FamilySearch unawawezesha wazao wote kushiriki taarifa ambazo wengine yaweza kuwa hawazifahamu na unaongeza vyanzo ili kuthibitisha taarifa sahihi.
  4. Unganika na Wazao Wengine: Kufanya kazi pamoja kwenye mti wa ulimwenguni kote pia kunawasaidia wazao kuungana wao kwa wao. Unaweza kumpata jama yako aliyetembelea makaburi hayo hayo, aliyeuliza kuhusu maswali hayo hayo—na hata aliyejifunza kupenda au aliyevutiwa na—mababu hao hao.
  5. Fanyia Kazi Historia Yako ya Familia bila Malipo: Unapoingia kwenye akaunti iya FamilySearch ya bure na kuunganika kwenye mti wa familia shirikishi, utaweza kuwaona mababu zako wote waliounganika kwenye mwonekano wa mti binafsi. Mti huu wa familia wa mtandaoni unakuruhusu kuongeza matukio ya maisha kwenye wasifu wa mababu zako, kutazama kwenye ramani ya maeneo ambapo yawezekana kuwa walitembelea, kutazama na kuongeza picha, kumbukumbu, na rekodi, na mengine mengi zaidi.

Ili kufanya ugunduzi kwa kutumia Mti wa Familia wa FamilySearch, ingia kwenye FamilySearch.org au kwenye programu ya simu ya Mti wa Familia.

Mgeni kwenye FamilySearch? Jiandikishe kwa ajili ya Akaunti ya Bure

Ona kile ambacho mti mkubwa kabisa shirikishi wa ulimwenguni unachoweza kukuambia kuhusu familia yako. Jiandikishe kwenye FamilySearch.org, au pakua programu ya Mti wa Familia kwa ajili ya iOS au Android.

Jifunze Zaidi kuhusu Mti Shirikishi

Ili kujifunza jinsi ya kuwapata mababu ambao yawezekana wapo tayari kwenye mti shirikishi, kuunganika na wanafamilia walio hai kwa kutumia FamilySearch na mengine zaidi, chunguza viungo hapa chini!

authorBy  FamilySearch
May 21, 2024
FamilySearch inakuruhusu kugundua mengi zaidi kuhusu familia yako, kuweza kufuatilia mti wa familia yako na kushiriki kile unachojua—yote bila malipo!
Washiriki wa FamilySearch wanaweza kuona jinsi wanavyounganika wao kwa wao, kujifunza kuhusu ukoo wao, na kushiriki kile kinachojulikana kuhusu jamaa zao waliofariki.
Watu wengi kwenye FamilySearch wanapata miunganiko kwa kuvumbua kumbukumbu na kuwatafuta mababu wapya au kupata taarifa mpya ambazo wengine wameziweka.
Kuwasiliana na watumiaji wengine wa FamilySearch kunaweza kuwa sehemu muhimu ya kujenga mti wa familia na kuunganika na familia yako—iliyopita na ya sasa.
Mti una zaidi ya majina bilioni moja. Ni bure na upo kwa ajili ya umma, na mababu unaowatafuta yawezekana tayari wamo.

aboutContributorHeading