Kuanza Kufanyia Kazi Mti wa Familia Shirikishi wa FamilySearch

Smiling family standing together while watching photos in album.
Framestock - stock.adobe.com

Mti wa Familia wa FamilySearch ni mti mkubwa kabisa wa ulimwenguni mtandaoni. Ni mti shirikishi, wa wazi, ambapo washiriki wanaweza kuona jinsi wanavyounganika mmoja na mwingine, kujifunza kuhusu ukoo wao na kushiriki kile kinachojulikana kuhusu jamaa zao waliofariki.

Unapounganika kwenye mti shirikishi wa FamilySearch, unaweza kuwagundua mababu ambao hukujua kuwahusu na kujifunza mengi kuhusu wale ambao tayari unawajua. Unaweza hata kuona picha na kusoma hadithi za familia zilizopakiwa na vizazi vingine. Unapotengeneza wasifu wa mababu kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch, unatengeneza pia msingi kwa ajili ya wanafamilia wengine kujifunza zaidi na kushiriki kile wanachokijua kuwahusu mababu zako.

Jinsi ya Kuanza

Ili kujiunga na Mti wa Familia wa FamilySearch, nenda kwenye FamilySearch.org. Ingia au tengeneza akaunti ya bure. Chini ya kichupo cha Family Tree chagua Tree.

Picha ya skrini ya menyu yenye viungo vya FamilySearch.

Kisha, bofya Add Father au Add Mother, na ingiza kile unachokijua kuwahusu wazazi wako.

Picha ya skrini ya vitufe vya Ongeza Baba na Ongeza Mama kwenye FamilySearch.

Mababu Walio Hai dhidi ya Waliofariki

Ikiwa mzazi au jamaa mwingine unayemuongeza yu hai, FamilySearch itatengeneza wasifu wa siri, uliyolindwa ambao ni wewe pekee unaweza kuuona. Unapokuwa umeongeza taarifa za kifo kwenye wasifu, wasifu wa mtu huyo unakuwa ya wazi. Badiliko hili humaanisha kwamba wasifu unaweza kuonekana na wengine ambao wanatumia mti wa familia shirikishi.

Kuoanisha Wasifu wa Mababu na Ule ambao Tayari Upo kwenye Mti Shirikishi

Unapojaribu kumuongeza jamaa aliyefariki, FamilySearch kwanza itatafuta ili kuona ikiwa wasifu kwa ajili ya mtu huyo tayari upo kati ya wasifu bilioni 1.2 kwenye Mti wa Familia. Utaoneshwa wasifu wowote ulio na taarifa zinazofanana. Kwa mfano, acha tuseme unataka kumuongeza mwanamke mwenye jina Opal Collins aliyezaliwa mnamo 1918 huko Kentucky, Marekani. Kama ilivyooneshwa hapa chini, FamilySearch inakuambia kwamba wasifu sawa na huo tayari upo kwenye Mti wa familia.

Picha ya skrini ya kuongeza mfanano kwenye Mti wa Familia.

Ni juu yako kuamua ikiwa wasifu uliyopo sasa uliyooneshwa chini ya “Mifanano Yakini Iliyopatikana” (ikiwa na mwaka wa kuzaliwa 1917 eneo la Kentucky kwa wazazi waliooneshwa) ni Opal Collins yuleyule unayetaka kumuongeza.

  • Ikiwa taarifa za wasifu zinafanana na kile unachokijua kuhusu mababau zako, kubali kwa kuchagua uchaguzi wa 1, Add Match au Add Couple Match.
  • Ikiwa una hakika wasifu haufanani, tengeneza wasifu mpya ukitumia uchaguzi wa 2, Create Person.
  • Ikiwa huna hakika kama mojawapo ya wasifu zinafanana, unaweza kujaribu kubofya jina la wasifu ili kupata taarifa. (Kidokezo: Tumia Ctrl+bofya au Command+bofya ili kufungua ukurasa wa mtu kwenye kichupo cha kivinjari kipya ili kuepuka kuingilia mchakato wa kumuongeza jamaa yako.) Ikiwa unataka kuongeza utendeti zaidi kwenye utafutaji wako ili ubainishe vizuri zaidi wasifu wa jamaa yako, unaweza pia kuchagua uchaguzi wa 3, Refine Search.

Ikiwa utachukua muda kutafuta mfanano sahihi na kuuongeza kwenye mti wako—badala ya kutengeneza wasifu mpya kwa jamaa huyo—unaweza kugundua mengi zaidi kuhusu jamaa zako na unaweza kushiriki kile unachokijua kwa vizazi vingine vya mtu huyo. Ikiwa unaongeza mfanano ambao tayari una wazazi na mababu walioambatishwa, utafanya pia mchakato wa kujaza mti wako wa familia uwe rahisi zaidi. Wakati wasifu rudufu zinapokuwa zimetengenezwa kwa ajili ya mababu ambao tayari wapo kwenye Mti wa Familia, wasifu baadaye itaunganishwa na ule uliyopo tayari.

Kuongeza Mababu Zaidi

Baada ya kutengeneza au kupata wasifu wa wazazi wako, tumia njia hiyohiyo kutengeneza au kutafuta wa mabibi na mababu na jamaa wengine. Kumbuka kwamba unaweza kuongeza seti nyingi za wazazi, ikiwa ni pamoja na wazazi wa kambo, wazazi wa kibaiolojia na wazazi walioasili. Hapa kuna jinsi ya kufanya hilo.

Kuufanya Mti Shirikishi Ukue

Unapounganika na wasifu wa sasa kwenye Mti wa Familia, jamaa wengine waliofariki ambao tayari wameunganika nao kwenye mti wataonekana kiautomatiki. Mchoro wa mfano hapa chini unafafanua mchakato wa kuunganika kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch kwenye matawi tofauti tofauti ya mti wako:

  1. Ongeza wasifu kwa ajili ya jamaa walio hai, ambayo itabakia siri.
  2. Ongeza taarifa kuhusu jamaa aliyefariki na pitia mifanano yakini kutoka kwenye Mti wa Familia shirikishi. Wasifu wa wafu zitaonekana wazi.
  3. Ikiwa utapata mfanano kwenye mti, kurasa za ziada kwa ajili ya jamaa wengine zinaweza kuonekana kiautomatiki!
Vielelezo vikionesha jinsi ya kuunganika kwenye mti wa watu wote wa FamilySearch.

Unaweza kukuta makosa kwenye wasifu wa jamaa waliofariki au kwenye jinsi walivyounganishwa na wengine. Tunatumaini utasaidia kurekebisha makosa!

Nini cha Kufanya Ikiwa Hupati Mfanano

Baadhi ya watu yawezekana wasikute kwamba jamaa zao tayari wapo kwenye mti shirikishi wa FamilySearch. Ikiwa hili ni tatizo kwako, unayo changamoto na fursa ya kuongeza kile unachokijua. Kisha wewe na jamaa zako walio hai mnaweza kushirikiana ili mjifunze zaidi kuwahusu. Watu wengine ulimwenguni kote ambao wana uhusiano na watu hao wanaweza hatimaye kukugundua na kuunganika nawe kwenye mti wa watu wote wa FamilySearch

Nenda kwenye FamilySearch na utengeneze mahali pako kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch leo!

authorBy  Sally Odekirk
February 21, 2025
Umeamua kujifunza kuhusu mababu zako na kuchangia kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch.Hongera! Kuwagundua mababu zako kunaweza kujawa na m…
authorBy  Sunny Jane Morton
February 27, 2024
Tovuti ya bure ya FamilySearch ni nyumbani kwa mti wa familia ulio mkubwa zaidi wa mtandaoni ulimwenguni. Ukijulikana kama Mti wa Familia wa…

Jinsi ya Kuitafuta Familia Yako

authorBy  Rachel J. Trotter
May 21, 2024
Mti wa familia wa FamilySearch ni nyenzo ya ajabu. Kwa baadhi, kutumia Mti wa Familia wa FamilySearch kuitafuta familia yako inaweza kuoneka…

aboutContributorHeading