Jiunge na Mti wa Familia wa FamilySearch

Portrait of grandmother collecting puzzle with her granddaughter

Umeamua kujifunza kuhusu mababu zako na kuchangia kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch.Hongera! 

Kuwagundua mababu zako kunaweza kujawa na milima na mabonde yasiyotarajiwa, kama vile kufanyia kazi kitu kilichofichika au chamsha bongo. Na, kama lilivyo chamsha bongo, inasaidia kujua wapi pa kugeukia ili kupata majibu ya maswali yako.

Mara unapokuwa umetengeneza mti wako, unaweza kujiuliza wapi pa kupata majibu ya maswali yako na unaweza kutaka kujua nini cha kufanya kama hatua inayofuata. 

Maswali kadhaa yanaweza kuibuka wakati ukifanyia kazi Mti wa Familia wa FamilySearch. Unaweza kujiuliza: 

  • Ni kwa namna gani ninaunganika kwenye mti wa jamaa zangu?
  • Kuna taarifa nyingi zinapatikana. Naanzia wapi?
  • Vipi ikiwa siwezi kupata taarifa yoyote?
  • Ni kwa namna gani ninachangia ikiwa wanafamilia wamefanya kazi yote?
  • Ni kwa namna gani ninatumia tovuti shirika na programu zingine za historia ya familia sambamba na FamilySearch.org?

Maswali haya na mengine yanayofanana na haya yanaweza kufanya kuanza historia ya familia kuonekane kuwa jambo la kuchosha, hata wakati mwingine la kukanganya. Lakini msaada unapatikana!
Vipengele kadhaa vinapatikana kwenye FamilySearch.org ambavyo vinaweza kufanya mti wako wa familia ukue. Kwa mfano, unapokwenda kwenye menyu ya mtiririko ya Msaada kwenye ukurasa mkuu, utapata Help Center kwa ajili ya maelekezo ya hatua kwa hatua ya jinsi ya kutumia FamilySearch.org na menyu ya Getting Started ili kusaidia kujibu maswali ya msingi, sambamba na kurasa kadhaa za nyenzo ambazo hutoa taarifa za ziada.

Kuongezea kwenye menyu ya mtiririko ya Msaada, kurasa hapo chini zimejaa ushauri wenye umaizi na maelekezo yenye msaada ya jinsi ya. Vitafute na uone jinsi ilivyo rahisi kuanza kwenye historia yako ya familia! 

August 15, 2023
Kama uko tayari kuanza kujifunza kuhusu mti wa familia yako, basi FamilySearch.org ni mahali pazuri pa kufanya hivyo. Kufungua akaunti yako …
authorBy  Jan Mayer
August 7, 2023
Wakati unapojaribu kuleta maana ya miunganiko ya kifamilia, kuona ni kuamini. Kila moja ya mionekano minne ya ukoo wa Mti wa Familia wa Fami…
authorBy  Sunny Jane Morton
September 14, 2023
Mti wa Familia wa FamilySearch ni mti mkubwa kabisa wa ulimwenguni mtandaoni. Ni mti shirikishi, wa wazi, ambapo washiriki wanaweza kuona ji…
authorBy  Sunny Jane Morton
October 29, 2023
FamilySearch.org ni makazi ya mti mkubwa kabisa wa ulimwenguni wa mtandaoni, na una kumbukumbu ya zaidi ya watu bilioni moja. Gundua mengi z…
authorBy  FamilySearch
May 21, 2024
Mti wa Familia wa FamilySearch unakuruhusu ugundue mengi zaidi kuhusu familia yako, uweze kufuatilia mti wa familia yako na kushiriki kile u…

aboutContributorHeading