FamilySearch.org ni makazi ya mti mkubwa kabisa wa ulimwenguni wa mtandaoni, na una kumbukumbu ya zaidi ya watu bilioni moja. Gundua mengi zaidi kuhusu jamaa zako—au ongeza kwenye kile ambacho tayari kinajulikana kuwahusu—kwa kutafiti kurasa zao binafsi.
Ukurasa wa Mtu wa FamilySearch Ni Nini?
Ukurasa wa mtu ni muhtasari wa taarifa za wasifu na za nasaba kuhusu mtu mmoja. Kurasa za watu waliofariki ni za wazi na zinaweza kutazamwa au kubadilishwa na yeyote; hata hivyo, kurasa za watu walio hai ni za faraghakwa mtumiaji ambaye amezitengeneza.
Kurasa za umma za mtu ni hazina ya maarifa ya ushirikiano kwa ajili ya vizazi vya mtu. Watumiaji wa FamilySearch huongeza kile wanachokijua, huambatisha kumbukumbu za kihistoria kama ushahidi na huunganisha kurasa hizi kwenye kurasa za wazazi, wenza, kaka na dada na watoto wa mtu huyo.
Kwa mfano, hebu tuseme kwamba mtu katika ukoo ametengeneza ukurasa wa mtu kwa ajili ya babu yake mkuu wa pili , lakini alifahamu jina lake na maelezo ya ubatizo pekee. Baadaye, mzao mwingine kuupata ukurasa huu, akapakia picha, na kuongeza mwenza. Mtu wa tatu akaingiza data za kifo zilizoelezwa kwenye jiwe la kaburi na akatengeneza kurasa kadhaa za watu kwa ajili ya watoto wao.
Pale watumiaji wa FamilySearch wanapoleta pamoja maarifa yao, kurasa hizi hufunua hadithi za maisha ya mababu zetu na uhusiano wao kwa familia zao. Ushirikiano huu humsaidia kila mmoja ashiriki, agundue na ahifadhi historia yao iliyounganika ya familia.
Jinsi ya Kupata Ukurasa wa Mtu wa Jamaa
Mti wa Familia wa FamilySearch hauna kurasa za watu kwa ajili ya kila mtu aliyefariki, lakini ina thamani kutafuta kurasa za watu zaidi ya bilioni 1.6 ambazo zimetengenezwa.

Ikiwa tayari umeunganishwa kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch, unaweza kumtafuta jamaa kwenye mwonekano wa mti. Ingia ukitumia akaunti yako ya bure ya mtumiaji na chagua kichupo cha Tree Kisha tafiti kupitia mababu zako mpaka ujue ni wapi taarifa za jamaa zako zinapaswa kuwa. Ikiwa utapata jina la mtu, libofye, kisha bofya Tazama Mtu ili kwenda kwenye ukurasa unaomhusu mtu huyo.
Ikiwa huwezi kumpata jamaa fulani kwa urahisi kwenye mti, au bado hujaunganishwa na mtu kwenye mti, unaweza pia kutumia pekua kurasa za mtu aliye hai. Kwenye menyu upande wa juu wa ukurasa, bofya Mti wa Familia, na kisha bofya Tafuta. Ndani ya visanduku vya kupekua, ingiza kile unachokijua kuhusu mtu huyo. Kisha bofya Tafuta.
Unaweza kuona majibu kadhaa ya upekuzi ya kurasa za mtu yakiwa na taarifa zinazofanana na kile ulichoingiza. Kwa umakini pitia tena mifanano yenye uwezekano. Yawezekana kwamba ukurasa zaidi ya mmoja wa mtu umetengenezwa kwa ajili ya jamaa yako. (Ikiwa una hakika kwamba kuna rudufu, unaweza kuunganisha kurasa). Kuna uwezekano pia kwamba ukurasa haujatengenezwa kwa ajili ya jamaa yako. Ikiwa ndivyo, unaweza kuongeza ukurasa.
Kuelewa Ukurasa wa Mtu wa FamilySearch
Ukurasa wa Mtu wa FamilySearch umesanifiwa ili kushikilia kiasi kikubwa cha taarifa kuhusu mababu zako. Kulingana na kiasi gani kimeongezwa, ni kama kutembelea maktaba ndogo—maktaba ambayo imewekwa wakfu kabisa kwa mababu zako!
Kuelewa jinsi ukurasa wa mtu ulivyopangwa kutakusaidia kujua jinsi ya kuendesha kila kitu kilichopo hapo na kupata hasa kile unachokitafuta.
Bango la Jina
Kitu cha kwanza unachokiona unapoenda kwenye ukurasa binafsi wa mababu zako pengine ni bango la jina, lililo juu ya ukurasa.

Bango la jina linajumuisha taarifa na viungo vifuatavyo:
- Jina kamili la babu yako.
- Tarehe za kuzaliwa na kifo za babu yako (taarifa nyingi kama zinavyojulikana).
- Namba ya Utambulisho wa Mti wa Familia ya mababu zako, ambayo unaweza kuitumia kwa haraka kuipata ukurasa huu tena katika siku zijazo. Unaweza pia kushiriki namba ya utambulisho na mtu mwingine ili aweze kupata ukurasa kwa haraka.
- Kiungo cha kuwatazama mababu zako ndani ya chati ya ukoo ya FamilySearch inayojulikana kama Mti wa Familia.
- Kiungo cha kuangalia chati ya ukoo iliyokuzwa, iliyorahisishwa ambayo inaonyesha jinsi wewe na babu yako mnavyohusiana.
- Kiunganishi cha kufuata ukurasa binafsi wa mababu zako. Unapomfuata babu, unapokea taarifa wakati wowote mtu anapoongeza taarifa au kuhariri ukurasa wa mtu wake.
Vichupo vya Urambazaji
Chini ya bango la jina ni safu ya vichupo vya urambazaji. Kwa njia moja, hii ni sehemu muhimu zaidi ya ukurasa wa mtu. Hiyo ni kwa sababu kichupo chochote ulichochagua huamua kila kitu unachoona chini ya bango la jina.
Kama umewahi kutembelea ukurasa binafsi wa mababu zako na vitu vinaonekana tofauti na mara ya mwisho ulipokuwepo, pengine ni kwa sababu unatazama kichupo tofauti.



Kichupo cha Ushirikiano ni kwa ajili ya kuzungumza na watu wengine kama wewe mwenyewe kuhusu ukurasa binafsi wa mababu zako. Hapa ni mahali pazuri pa kuacha maswali au kuanza majadiliano kuhusu jambo unalojaribu kujifunza au kufikiria.
Kichupo cha Memories kinakupeleka kwenye Memories Gallery ya babu yako, ambapo unaweza kuvinjari picha, rekodi za sauti, na nyaraka zingine ambazo watu wamepakia kuheshimu na kumkumbuka babu yako.


Kidokezo: Tumia kichujio cha tukio, kilicho juu ya mpangilio wa muda, ili kuchagua ni matukio gani unataka kuona yanaonyeshwa kwenye ramani. Baada ya hapo, unaweza kuonyesha njia chini ya ramani, na mstari wa nukta utaunganisha matukio katika mpangilio wa wendo. Matokeo hayo ni ramani ambayo inakuonyesha safari ambayo babu yako alikuwa akichukua wakati matukio yalipofunuliwa katika maisha yake.
Gundua Kitu Kipya
Tafiti kurasa za watu za mababu zako. Ikiwa tayari umeunganishwa kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch, anza kufanyia utafiti tree view. Vinginevyo, pekua mti kwa ajili ya jina la jamaa aliyefariki, na uone kile unachogundua!
Katika FamilySearch tunajali kuhusu kukuunganisha na familia yako, na tunatoa uzoefu wa ugunduzi wa kufurahisha na huduma za historia ya familia bila malipo. Kwa nini? Kwa sababu tunathamini familia na kuamini kuwa kuunganisha vizazi kunaweza kuboresha maisha yetu, sasa na milele. Sisi ni shirika lisilo la faida linalofadhiliwa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Ili kujifunza zaidi kuhusu yale tunayoyaamini, bofya hapa.