Je, unajaribu kuwatafuta mababu au mwana familia aliyefariki? Ikiwa ndivyo, unapaswa kuchunguza Mti wetu wa Familia— mti mkubwa zaidi wa familia shirikishi ulimwenguni. Mti una zaidi ya majina bilioni moja. Ni wa bure na upo kwa ajili ya umma, na babu unayemtafuta yawezekana tayari yumo humu.
Kusanya kile unachokijua kuhusu jamaa yako aliyefariki—kama vile jina lake, taarifa za kuzaliwa na kifo na pengine jina la mzazi, mwenza au mtoto—na fuata hatua hapa chini kuona ikiwa yupo katika huu Mti wa Familia. Au bofya kitufe hapa chini na nenda moja kwa moja kwenye ukurasa wetu wa Kutafuta.
Kuchunguza Mti wa Familia—Njia ya Haraka ya Kuanza au Kuongeza Nasaba Yako
Ikiwa unataka kumtafuta jamaa ambaye yawezekana yuko kwenye Mti, nenda kwenye FamilySearch, na chini ya kichupo cha Tree Family , chagua Find. Jiandae kuingia au tengeneza akaunti ya bure ya FamilySearch. (Unaweza pia kufika kwenye ukurasa huu huu kwa kwenda kwenye kichupo cha Search , na kuchagua Family Tree.)

Mara uwapo kwenye Tree Find, ingiza kile unachokijua kuhusu jamaa yako aliyefariki. Ukurasa unafunguka na paneli ya utafutaji iliyorahisishwa, ambayo inafanya kazi kwa upekuaji wa mwanzo. Ili kupata matokeo bora zaidi, ni wazo zuri kufungua uzoefu wa upekuaji kamili kwa kubofya More Options.


Tafuta Mti huonekana na kufanya kazi karibu sawa na chombo cha Search Historical Records cha FamilySearch. Tulifanya hili kwa makusudi, ndiyo. Mikakati yoyote ya upekuzi uliyojifunza kwa ajili ya ukurasa huo itatumika hapa kwa usawa. Acha tupitie vichujio kimoja baada ya kingine na kuchunguza baadhi ya mbinu bora zaidi.

1. Majina
Zingatia mbinu bora zaidi za kujaza sehemu za jina:
- Ingiza jina la kwanza na la kati la mtu ndani ya sehemu ya Majina ya Kwanza.
- Ingiza jina la familia la mtu au jina la baba kwenye sehemu ya Majina ya Mwisho.
- Tumia kichupo cha Majina ya Mbadala kwa ajili ya majina ya mama kabla ya ndoa, majina ya utani, majina bandia, na herufi zingine, majina ya pili ya mwisho na mabadiliko yo yote ya majina ambayo yaweza kuwa yametokea katika kipindi cha maisha ya mtu.
2. Jinsia
Kuchagua Male au Female, ikiwa inajulikana, kunaweza kusaidia kupunguza matokeo ya upekuzi wako.

3. Matukio ya Maisha
Chini ya Ongeza Tukio la Maisha, ingiza kile unachokijua kuhusu wapi mtu aliishi kipindi cha uhai wao. Hakikisha kubadili kichujio kutoka Any kuwa Birth, Marriage, Residence, au Death. Kufanya hivyo kunaweza kufanya upekuzi wako uwe sahihi zaidi.
4. Wanafamilia
Chini ya Add Family Members, ingiza kile unachokijua kuhusu mwenza wa mtu, baba, mama au uhusiano mwingine. Unaweza kutumia miongozo na mbinu zile zile kwa ajili ya kuingiza majina hapa kama ulivyofanya awali.
5. Upekuzi Halisi
Moja kwa moja chini ya sehemu ya Mwanafamilia kuna kibanio kwa ajili ya Show Exact Search. Kuwa makini unapotumia uchaguzi huu, na utumie tu wakati unapopata matokeo mengi zaidi ya upekuzi kuliko unavyoweza kuzingatia. Data halisi kwenye Mti wa Familia zinaweza kuwa tofauti kidogo na majina, tarehe na mahala unapoingiza, hivyo kuweza kubadilika kulingana na vigezo vyako vya upekuzi daima ni wazo zuri.
Ni muhimu kukumbuka kwamba kugeukia kibanio kwa ajili ya Show Exact Search haishiriki upekuzi halisi mara moja. Badala yake, kinafungua kisanduku kando ya vichujio vyote vya skrini ya upekuzi, ambapo unaweza kuchagua au kuacha tupu. Imependekezwa sana kwamba uchague tu sehemu ambazo una hakika unataka kuwa mahususi na kwamba uanze na chache. Kwa maneno mengine, unaweza kufanya upekuzi mahususi kwa ajili ya tarehe fulani ya kuzaliwa lakini si kwa sehemu zako zingine.
Pale unapokuwa umeingiza taarifa unazozijua, bofya Find ili kupekua kurasa za mababu zako kwenye Mti wa Familia. Wakati matokeo ya upekuzi yanapotokea, bofya jina ili uone muhtasari wa taarifa ya mtu huyo. Kisha bofya kwenye jina ndani ya dirisha la kutokea ili kutafiti ukurasa wa mtu.
Vidokezo vya Kisasa vya Kumtafuta Mtu Sahihi
Matokeo Mengi
Tumia kitufe cha kijivu upande wa juu wa ukurasa ili kutuni vyema matokeo yako ya uchunguzi kwa haraka:

Kwenye uchunguzi uliooneshwa na picha hizi za skrini, mwanzo niliingiza jina la babu wa baba yangu. Kama unavyoweza kuona, uchunguzi huu mpana umerudisha majibu mengi—mengi sana kuanza kuchunguza yote. Ikiwa nitabofya kichujio cha Birth, hata hivyo, na nichague eneo maalumu la ulimwengu, ninaweza kwa haraka kufanya idadi hiyo iwe ndogo zaidi.


Hakuna Matokeo au Mifanano
Ikiwa upekuzi wako wa mwanzo umerudi patupu, tumia paneli ya upekuzi upande wa kulia wa skrini ili kurekebisha vigezo vyako vya upekuzi. Kumbuka: Kutegemeana na ukubwa wa skrini yako, paneli ya upekuzi inaweza isifunguke mwanzoni. Ikiwa ndivyo, bofya Search kwenye kona ya kulia ili kuifungua.
Ili kupanua upekuzi wako, fikiria kurekebisha cho chote ambacho kimekuwa cha kipekee sana, kama vile mwaka halisi. Kuongeza kipindi cha tarehe kwa tukio fulani la maisha kunaweza kusaidia. Unaweza pia kujaribu kubadili menyu ya Tukio la Maisha kuwa Birth au Residence badala ya Any. Ikiwa inawezekana, tumia sehemu ya Majina Mbadala kuingiza majina ya mama kabla ya ndoa, majina bandia au tahajia tofauti za neno. Kisha bofya Search.
Ikiwa baada ya kuhariri upekuzi wako, bado humpati mtu unayemtafuta, yaweza kuwa mtu bado hajaongezwa kwenye Mti wa Familia. Katika hali hiyo, unaweza kuendelea na kumuongeza mtu huyo wewe mwenyewe.
Ili kumuongeza mtu kwenye mti, utahitaji jina lake na kisha unaweza kuingiza taarifa nyingi za ziada zinazowahusu wao kadiri unavyoweza, kama vile mahali walipozaliwa au mahali walipoishi.
Dokezo: ikiwa unakosa taarifa kuhusu mababu zako, jaribu kuwatafuta kwenye kumbukumbu za kihistoria, kama vile cheti cha kuzaliwa, cheti cha ndoa, kadi ya kliniki au cheti cha kifo.
Kutumia Mapendeleo ili Kuboresha Matokeo Yako ya Upekuzi
Watafiti wazoefu wanaweza kushukuru kwa utendaji unaokuja na kitufe cha Pendeleo ambacho hutokea juu ya ukurasa wako wa matokeo ya uchunguzi. Kwa Mapendeleo, unaweza kufanya chaguzi muhimu kuhusu muundo na usafirishaji wa matokeo yako ya upekuzi.
Kwa mfano, uchaguzi wa kwanza chini ya Mapendeleo ni uchaguzi wa kuwasilisha matokeo yako ya upekuzi kwenye Karatasi ya Data au Jedwali Lililopangwa:

Ikiwa nilikuwa ninaangalia jibu la upekuzi ambao ulifanana na taarifa moja maalumu—tarehe fulani ya kuzaliwa, kwa mfano—ningetumia Karatasi ya Data. Mpangilio huifanya iwe rahisi kupandisha juu na kushusha chini na kupata matokeo yenye mfanano.

Ningetumia Jedwali Lililopangwa, kama kinyume chake, wakati nilipotaka kutazama kwa karibu matokeo machache ya upekuzi ambayo yote yanaonekana ya kufaa na kuona jinsi yalivyofanana na kila kitu nilichokijua kumhusu mtu.

Chini kabisa ya ukurasa wa Mapendeleo kuna sehemu yenye kichwa cha habari Chaguzi za Lugha. Hapa unaweza kuchagua kutazama taarifa jinsi zilivyoingizwa kwa uhalisia kwenye FamilySearch, au kuzitazama kwa kuhariri kidogo—kile tunachokiita “tafsiri”—ambayo huzifanya ziwe rahisi kusomeka. Mfano rahisi ungekuwa ingizo la “Jan 1855,” ambalo, likifafanuliwa au kutafsiriwa, litaonekana kama “Januari 1855.”
Cha mwisho tu, kwenye ukurasa wa Mapendeleo kuna uchaguzi wa kupakua matokeo yako ya upekuzi kwenye kompyuta yako mwenyewe. Pengine una mbinu yako ya kuchati na kuchuja taarifa. Ikiwa ndivyo, unaweza kupakua taarifa kwenye mpangilio wowote kati ya hii: XLS, XLSX, CSV, ODS, TSV, na ODS.
Watafute Mababu zako kwenye Mti wa Familia wa Family Search!
Je, uko tayari kujifunza jambo kuhusu mmoja wa mababu zako? Mti wetu wa Familia shirikishi una nafasi ndani yake kwa ajili ya kila mmoja ulimwenguni—na tunahitaji usaidizi wa kila mmoja ili kuujenga!
Mchague jamaa yako aliyefariki, na ona kama mtu huyo ni kati ya majina bilioni 1.2 kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch! Tafuta wasifu wa mtu huyo, na furahia hadithi, picha, mpangilio wa matukio na vitu vingine ambavyo vimeambatishwa. Kisha zingatia kile unachokijua kuwahusu na unaweza kuongeza kwenye wasifu wao. Jamaa zako wengine wanaweza kukushukuru katika siku za mbeleni!