Je, umewahi kumtumia mtu ujumbe mfupi kwenye FamilySearch.org au kuwa na mjadala kuhusu mababu kwenye ukurasa wao wa mtu binafsi?Kuwasiliana na watumiaji wengine wa FamilySearch kunaweza kuwa sehemu muhimu ya kujenga Mti wa Familia na kuunganika na familia yako—iliyopita na ya sasa.
Mti wa Familia wa FamilySearch unaziwezesha familia kote ulimwenguni ili wafanye kazi pamoja na kujenga mti wa familia. Wazao kutoka matawi mbalimbali ya familia mara nyingi huwa na picha, nyaraka na kumbukumbu tofauti za familia. Wale wanaotafiti katika lugha fulani, mkoa, hifadhi za nyaraka au kwenye tovuti tofauti wanaweza kugundua taarifa za kipekee.
Wakati wazao wanapochangia kile wanachokijua kwenye Mti wa Familia shirikishi na kufanya kazi pamoja ili kutafuta taarifa mpya, uelewa wao wa pamoja huwa wenye nguvu zaidi. Wanaweza kujifunza zaidi ya kile wanachoweza kupata wakiwa peke yao na wanaweza kuokoa muda kwa kuacha muhtasari na kuwatumia ujumbe mfupi watumiaji wengine.
Njia Rahisi za Kuwasiliana na Watumiaji wengine wa FamilySearch.org
Mawasiliano na watumiaji wengine wa FamilySearch.org yanaweza kuwa yenye kuleta vyote mwongozo wa kiungu na msaada. Pengine unataka kumshukuru mtu kwa kupakia picha au kushiriki hadithi yenye maana. Utataka kujua chanzo cha data ya mtu mwingine kama hakikuwa kimewekwa. Unaweza kuuliza maswali ikiwa mtumiaji mwingine ameingiza makosa. Au yawezekana ukataka tu kuunganika na mtu ambaye ana mapendeleo yanayofanana na yako kwa jamaa fulani.
Hapa kuna baadhi ya njia rahisi za kuwasiliana na watumiaji wengine wa FamilySearch wakati unapotumia Mti wa Familia.
Fafanua Kazi Yako
Mpaka sasa, aina muhimu kabisa ya mawasiliano kwenye Mti wa Familia ni kuandika kwa nini unadhani taarifa uliyoongeza ni sahihi. Wakati wo wote unapoingiza au kuhariri taarifa, utaona kisanduku kinachosema “Sababu ya Kwa Nini Taarifa Hii ni Sahihi.” Chukua muda kuelezea vyanzo na sababu za kina zilizokuongoza kuingiza taarifa hii. Kauli zako za sababu zinakuwa sehemu ya wasifui aa mababu na yanaweza kuwasaidia wazao wengine waelewe kwa nini badiliko lilifanywa na kuwasaidia wao katika utafiti wao.

Huna uhakika wa nini cha kusema? Hapa kuna jinsi ya kuandika kauli yasababu ifaayo. (Kumbuka pia kuambatisha vyanzo vya kihistoria vinavyounga mkono kile unachosema!)
Tumia Collaboration Tab
Kwenye kurasa za wasifu wa kila mmoja wa mababu zako kuna Collaborate tab. Hapa, unapata mahali pa kuongeza muhtasari na kuwa na mijadala.
Kwenye sehemu ya muhtasari, unaweza kuweka jumbe fupi kwa ajili ya wengine ambao yawezakuwa wanawafanyia utafiti mababu hao. Tumia miuhtasari kuratibu utafiti, kuwaambia wengine pale ambapo umeweza kupata au hukuweza kupata kumbukumbu au tengeneza muhtasari kuhusu kumbukumbu mahususi. (Ona mfano wa muhtasari hapa chini.) Miuhtasari kwenye sehemu hiki unaweza kutazamwa na kuhaririwa na mtu ye yote anayetumia Mti wa Familia.
Muhtasari Muhimu:Tab ya miuhtasari si mahala pa kuweka uhusiano mahususi au utendeti wa tukio, kama vile tarehe za kuzaliwa na kifo. Utendeti huu unakwenda kwenye tab ya Details kwa ajili ya mababu zako. Hadithi na kumbukumbu pia vina mahala pake, chini ya Memories.

Kwenye sehemu ya Mjadala, unaweza kuanzisha au kujiunga na mjadala kuhusu mababu zako (Mfano: “Je, Charles alimuoa mtu mwingine tofauti na Valeria?”) Majibu yako wazi na yanabakia yakionekana isipokuwa mtu aliyeanzisha mjadala ayafute. Kipengele hiki ni njia nzuri ya kuwa na mazungumzo na wazao wengi.

Wasiliana na Mtumiaji Binafsi
Kila mtumiaji aliyechangia kipande cha taarifa kwenye Mti wa Familia anaunganishwa na jina la skrini ya mtumiaji ambaye amewasilisha taarifa hiyo. Ili kuona majina yaliyounganishwa, tafuta kitufe cha Detail View juu ya kila kipengele na kibofye ili kutazama taarifa.

Unaweza pia kuona orodha ya miuhtasari ya mabadiliko ya siku za karibuni kwenye wasifu wa mababu (na mtu aliyefanya mabadiliko hayo) chini ya Detail tab, ambao unasema Latest Changes; bofya Show All ili uone historia kamili.
Wasiliana na mtumiaji kwa kubofya kwenye jina la skrini ya mtu huyo, popote linapoonekana. Kama ilivyooneshwa hapa, dirisha jipya litatokea ambalo litakuruhusu utume ujumbe. (Ili kuangalia ujumbe wako mwenyewe, ingia na bofya jumbe cha Messages upande wa juu kulia wa skrini ya FamilySearch.org . Unaweza pia kupokea ujumbe wa barua pepe wakati mtumiaji mwingine wa FamilySearch.org anapokutumia ujumbe mfupi.)

Mara moja moja, unaweza kugundua kwamba mtumiaji amewasilisha makosa kadhaa. Baadhi ya watumiaji hawana uzoefu au maarifa kama wengine. Baadhi wanaweza wasiwe na taarifa kamili au sahihi. FamilySearch inamkaribisha kila anayetaka kukuza Mti wa Familia na inatumaini kwamba watafiti wenye weledi zaidi wanaweza kuwasaidia wanafunzi walioradhi kuboresha michango yao.
Ili kuanza au kuboresha ushirikiano wa sasa na wazao wengine, bofya hapa ili uende kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch!