Jinsi ya Kuanza Mti wa Familia kwenye FamilySearch: Kuongeza Vizazi Vinne vya Kwanza

CWD_85328A2A-12EA-20D4-E053-CB02630A594D

Kama uko tayari kuanza kujifunza kuhusu mti wa familia yako, basi FamilySearch.org ni mahali pazuri pa kufanya hivyo. Kufungua akaunti yako mwenyewe bila malipo ni rahisi sana. Mara akaunti yako inapokuwa tayari, unaweza kujiuliza, “Sasa nini kingine?”

Njia nzuri zaidi kuanza ni kuongeza vizazi vinne vya kwanza vya familia yako. Kujenga mti wako mwenyewe kutakusadia kupata pale unapounganika na mti wa familia wa ulimwenguni kote wa FamilySearch. Kwa kiungo kimoja, mti wako mdogo wa familia ungeweza ghafla kupanuka kurudi nyuma mamia ya miaka!

Kukusanya taarifa za familia yako na kuziweka ndani ya mti wa familia pia kunaweza kukusaidia kuhifadhi kumbukumbu na taarifa kuhusu familia yako iliyo hai. Licha ya kuingiza tarehe na mahali katika mti wa familia yako, unaweza pia kupakia nyaraka za thamani za familia, kuhifadhi picha, au hata kuhifadhi klipu za sauti.

Kuunda mti wako mwenyewe wa familia ni rahisi! Hapa kuna hatua chache unazoweza kuchukua sasa hivi ili kuanza.

Anza na Wewe Mwenyewe

Katika menyu hapo juu ya ukurasa wa nyumbani wa FamilySearch, elekeza kielekezi cha panya juu ya Mti wa Familia, na, katika menyu ya kuteremka chini, bofya Mti. Mti wako wa familia utaonekana kwenye skrini. Jina lako, kama ulivyoliingiza wakati ulipofungua akaunti yako, linapaswa kutokea hapo katikati. Kumbuka kwamba FamilySearch hulinda usiri wa watu walio hai. Hakuna mtu mwingine atakayeweza kuona kile ulichoingiza kukuhusu wewe mwenyewe au wanafamilia wengine walio hai. Pia hautaweza kujikuta wewe mwenyewe mahali pengine popote kwenye mti—hata kama ndugu zako wengine wameingiza taarifa kuhusu wewe. Taarifa kuhusu watu walio hai lazima ziingizwe katika kila mti wa familia.

mfano ambao huonyesha jinsi ya kuongeza familia katika mti wa familia wa FamilySearch.

Bofya jina lako ili kwenda kwenye ukurasa wa mtu binafsi. Kutoka hapo, unaweza kuongeza taarifa zaidi kwenye ukurasa wako, ikijumuisha tarehe na mahali pamoja na mihutasari na kumbukumbu (kama vile picha, nyaraka na hadithi).

Ongeza Kile Unachojua kuhusu Familia Yako

Wewe mwenye ukiwa katika sehemu ya katikati kwenye mti wako, uko tayari kuanza kuongeza uhusiano wa kifamilia. Ili kumwongeza mama yako, kwa mfano, bofya Ongeza Mama.Kijisanduku kama hiki kitatokea:

kijisanduku cha “ongeza mama” ambacho kinatokea unapochagua “Ongeza mama” kwenye mti.

Ingiza taarifa nyingi iwezekanavyo katika fomu kadiri unavyojua.

Unaweza kuongeza taarifa kuhusu wanafamilia wengine—wenzi, watoto na wazazi—kwa njia hiyo hiyo. Lengo ni kumfikia mhenga aliyefariki. Unapoongeza mhenga aliyefariki kwenye mti, FamilySearch moja kwa moja itapekua mti wote mpana ili kukuunganisha na mti wa FamilySearch wa duniani kote.

Waulize Ndugu kwa ajili ya Taarifa Mpya

Unaposonga mbele kwenye mti wako, kuna uwezekano hautaweza kujaza kila nafasi tupu. Usiache taarifa ndogo zisizopatikana kukuzuia! Ingiza kila kitu unachojua, ukiacha sehemu za mti wako zilizo wazi kama inabidi. Mara unapomaliza kile unachojua, unakuwa tayari kusonga mbele kwenye awamu inayofuata—kupekua taarifa mpya.

Njia bora ya kuanza upekuzi wako kwa ajili ya taarifa mpya ni kuwauliza wanafamilia wako. Kama unakosa taarifa kuhusu watu walio hai, suluhu ya wazi ni kuwauliza wao! Ili kupata taarifa zinazokosekana kuhusu wahenga waliofariki, ni kuwauliza ndugu walio na umri mkubwa au ndugu ambao wanaweza kuwa waliwajua watu hao.

familia inaongea pamoja mlangoni pa nyumba.

Mara unapokuwa umekusanya kile ambacho familia yako inajua, ni wakati wa kupekua mkusanyiko mkubwa wa kumbukumbu za FamilySearch ili kujifunza zaidi kuhusu familia yako. Hakikisha umewaruhusu wengine kujua ambako umetoa taarifa zako kwa kuongeza vyanzo. Jifunze zaidi kuhusu jinsi ya kuongeza vyanzo hapa.

Unganika na Watu Wengine katika Mti wa Familia

Mara unapohama kutoka kuingiza taarifa kuhusu watu walio hai katika mti wako na kuanza kuingiza taarifa kuhusu mababu waliofariki, inawezekana kuungana na watu ambao tayari walishaingizwa katika Mti wa Familia wa FamilySearch. Kufanya muunganiko wa aina hii unaweza kuokoa muda sana. Badala ya kuingiza taarifa zote wewe mwenyewe, unaweza kufaidika na taarifa ambazo wengine wameziingiza.

Je, u tayari kuanza? Fuata maelekezo haya ili kuongeza vizazi vinne vya kwanza vya familia yako katika Mti wa Familia. Lakini kwa nini usimame katika vizazi vinne? Yawezekana ukaona kwamba kujenga mti wako kunafurahisha sana kwamba kuongeza vizazi vinne ndiyo mwanzo tu wa safari yako ya historia ya familia!

Soma Zaidi kuhusu Kujiunga na Mti wa Familia

authorBy  Sally Odekirk
February 21, 2025
Umeamua kujifunza kuhusu mababu zako na kuchangia kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch.Hongera! Kuwagundua mababu zako kunaweza kujawa na m…

aboutContributorHeading