Wakati unapojaribu kuleta maana ya miunganiko ya kifamilia, kuona ni kuamini. Kila moja ya mionekano minne ya ukoo wa Mti wa Familia wa FamilySearch hufunua mwonekano mpana wa mababu. Kwa kubofya kwenye jina husika, unaweza kugundua taarifa za mtu na historia ya familia inakuja kwenye maisha.
Mionekano mbalimbali ya Mti wa Familia huwasaidia wanaoanza waone jinsi mnyororo wa mababu unavyokaa pamoja. Inatoa pia maarifa kwa ono pana la wapi pa kwenda baada ya hatua hiyo.
Jinsi ya Kuanza
Pale unapokuwa umeingia kwenye FamilySearch.org, bofya Mti wa Familia. Kwenye kona ya kushoto kuna mtiririko ambao utakuruhusu ubadilishe mionekano. Kila mwonekano una taarifa zinazofanana lakini mpangilio tofauti.
Kabla hujatazama kwenye mionekano mbalimbali, hapa ni jinsi ya kutafiti kila moja ya mionekano minne.

- Ili kufunga minyororo yako yote iliyotawanywa na kurejea kwako, bofya ikoni ya nyumbani.
- Ili kusoma maelezo kuhusu mtu kwenye mti, bofya jina la mtu. Kisanduku cha muhtasari kitafunguka. (Ili kuona ukurasa wa mtu, bofya jina lililoangazwa ndani ya kisanduku.)
- Ili kuongeza mnyororo wa familia kwa vizazi vingine viwili, bofya mshale mwishoni mwa mnyororo huo.
- Ili kumhamisha mtu tofauti kwenda kwenye sehemu kuu, bofya jina lake na kisha kwenye kisanduku cha muhtasari, bofya Mti.
- Ili kuacha wazi minyororo yote iliyoongezwa na kurudi kwa yule mtu wa mwanzo, bofya ikoni ya kuweka upya katikati chini ya kitufe cha nyumbani.
Paneli ya Chaguzi

Paneli ya Options upande wa juu kulia wa skrini inakupa njia kadhaa za kubadilisha kile unachokiona kwenye mti wako. Chaguzi zake zinatofautiana kulingana na mtazamo wa mti unaoutumia.
- Chagua ikoni inayoonesha vidokezo vya kumbukumbu, mapendekezo ya utafiti, na matatizo ya data ili uone taarifa hii ikiakisiwa kwenye mti.
- Ili kuonesha au kuficha picha, chagua Portraits.
- Ili kubadilisha mpangilio wa rangi kutoka angavu kuwa ya giza,bofya Invert Colors.
- Ili kuchapisha vizazi, bofya Options, na kisha bofya Print.
Mionekano ya Mti wa Familia
Mwonekano wa Chati ya Feni
Chati ya Feni ni nyenzo yenye rangi, yenye mvuto kwa vijana na wazee vile vile. Inaonesha hadi kufikia vizazi 7. Upande wa kulia wa mtiririko wa mwonekano wa chati, unaweza kuchagua vizazi vingapi ungependa kuviona.

Vipengele vingi vyenye matumizi kwenye chati ya feni hutoa vidokezo na misaada ambayo hufanya iwe rahisi kutambua wapi mnyororo wako unaishia. Mwonekano huu pia unajumuisha orodha ya uchaguzi wa mwonekano wa chati. Kwa kutumia orodha hii, unaweza kuchagua kutoka mionekano anuai, yenye msimbo wa rangi ambayo inanururisha aina tofauti tofauti za taarifa kwenye mti wako. Taarifa hii hujumuisha yafuatayo:
- Minyororo yako ya familia.
- Nchi walizozaliwa mababu zako.
- Idadi ya vyanzo vilivyoambatishwa kwa kila jamaa.
- Idadi ya hadithi zilizoambatishwa kwa kila jamaa.
- Idadi ya picha zilizoambatishwa kwa kila jamaa.
Jina lako linaonekana chini katikati ya chati ya feni, pamoja na mwenza wako na watoto kwa chini. Mababu upande wa mama wanaonekana upande wa kulia na mababu upande wa baba wanaonekana upande wa kushoto. Mababu wa mwenza wako hawataonekana kwenye mwonekano huu isipokuwa kama unaangalia chati ya feni ya mwenza wako.
Mwonekano wa Kushuka
Descendancy view inaweza kukusaidia kutafuta wazao wa mababu zako. Ni muhimu sana ikiwa una mti wa familia uliojaa sana. Mwonekano huu huonesha zaidi ya wazazi, bibi na babu na bibi na babu wa wazazi; kwa mwonekano wa wazao, unaweza pia kuwapata mashangazi, wajomba, na binamu wa mbali pia!

Mwonekano wa Mlalo
Landscape view huwekwa kwa namna ya mlalo. Wewe upo katikati, wazao wako upande wa kushoto, na mababu upande wa kulia. Katika mwonekano huu, unaweza kuwaona watoto wa wanandoa kwa kubofya Children upande wa chini wa kisanduku cha wanandoa. Bofya mshale tena ili kurudi kwenye mwonekano wa mwanzo.

Mwonekano wa Wima
Portrait view huonesha mti wa familia kwenye nafasi ya wima, wewe na wazao wako mkiwa chini na mababu zenu wakiwa juu yenu.

Mionekano ya Mti wa Familia Hutusaidia Tuone Yaliyopita
Matokeo ya kuonekana ya kuzipanga familia kwenye mti wa familia yawezekana kukachochea hamu kubwa katika utafiti na pengine kujenga hamu yenye kuugeuza moyo ili kujifunza zaidi kuhusu wapendwa hao—urithi wako—kitu ambacho kitaongoza kwenye miunganiko iliyopita, ya sasa na hata ya baadaye.