Mti wa familia wa FamilySearch ni nyenzo ya ajabu. Kwa baadhi, kutumia Mti wa Familia wa FamilySearch kuitafuta familia yako inaweza kuonekana kazi ya kuchosha, lakini kuna miongozo ya kufanya upekuzi wako uwe rahisi zaidi. Kutumia Mti wa Familia wa FamilySearch kutatoa matokeo ya kuridhika na shangwe si tu kwako, bali kwa vizazi vingi vijavyo.
Mti wa Familia wa FamilySearch ni wa bure na hata kama hujawahi kutumia FamilySearch hapo mbeleni, unaweza kuunganika nayo kwa urahisi.
Makala hii inatoa viungo ambavyo vinaweza kukupitisha kwenye maswali unayoweza kuwa nayo wakati unapotumia Mti wa Familia wa FamilySearch. Tazama na uanze kuitafuta familia yako!
Mwongozo wa Mwanafunzi wa Kupekua Kumbukumbu
Kuna kumbukumbu nyingi za thamani zinazoomba kupatikana kwenye FamilySearch. “Mwongozo wa Mwanafunzi wa Kupekua Kumbukumbu” . Jifunze ni aina ipi ya kumbukumbu itakusaidia kuwapata mababu zako na mchakato wa hatua kwa hatua wa kupata matokeo.
Kumtafuta Mtu Mahususi
Wakati unapowatafiti mababu unaweza kutaka kumtafuta mtu mahususi – au pengine kutafuta historia maalumu, tarehe mahususi au kuwaunganisha wengine kwenye mti wako. Jifunze baadhi ya njia za haraka zaidi za kumtafuta mtu huyo na jinsi ya kuhakikisha yeye ndiye mtu hasa unayemtafuta.
Jinsi ya: Vidokezo vya Kumbukumbu

Mfumo wa FamilySearch mara zote hutafuta kumbukumbu za kidijitali, zilizo na vielezo ambazo zinaweza kufanana na watu kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch. Ikiwa mfanano yakini umepatikana, dokezo la kumbukumbu hutengenezwa. Vidokezo hivi vya kumbukumbu hutofautiana kuanzia kuunga mkono tarehe sahihi zaidi hadi kwenye kukusaidia wewe ugundue majina yaliyokamilika zaidi na mengine mengi zaidi. Jifunze zaidi kuhusu jinsi ya kutumia vidokezo vya kumbukumbu kwa ajili ya mafanikio bora zaidi.
SOMA MAKALA
Kuanza Kufanyia Kazi Mti wa Familia wa FamilySearch
Mti wa Familia wa FamilySearch ni mti mkubwa zaidi ulimwenguni wa mtandaoni. Unapounganika kwenye mti shirikishi wa FamilySearch, unaweza kuwagundua mababu ambao hukuwa ukiwajua na kujifunza mengi kuhusu wale ambao tayari unawajua. Jifunze jinsi ya Kuanza!
Jinsi ya: Kuwaunganisha Watu

Mara nyingi, kuna ukurasa zaidi ya mmoja kwa ajili ya mtu yule yule. Hii inaweza kuleta mkanganyiko, na hii ndiyo sababu kurasa za kuwaunganisha watu zinakuwa muhimu. FamilySearch ina nyenzo “inayowezekana kuwa nakala” ambayo inakusaidia uone kama unahitaji kuunganisha kurasa; lakini hata ikiwa mfumo hauwezi kutambua mfanano, bado unaweza kuunganisha.
SOMA MAKALA
Kutumia Mti wa Familia wa FamilySearch ili kutafuta familia yako kunaweza kuwa mchakato wenye baraka na wa kusisimua ambapo unaweza kugundua, kukusanya, na kuunganika na wakati uliopita, uliopo na ujao. Kwa kufuata baadhi ya makala zilizounganishwa hapo juu, utakuwa kwenye njia yako ya kujenga mti wenye mafanikio na wenye maana.