Kwenye mti wa familia wa umma na shirikishi, kuwa na chanzo kisicho sahihi kilichounganishwa kwa mababu zako si kitu cha nadra kutokea. Kwa bahati nzuri, chanzo kisicho sahihi kinarekebishika kwa urahisi. Hapa kuna baadhi ya njia za kusahihisha viungo visivyo sahihi kwenye FamilySearch.
Tengua viungo
Njia moja ya kushughulikia viungo visivyo sahihi ni kuviondoa tu. Sahihisho hili linaweza kufanywa katika hatua chache rahisi:
1. Nenda kwenye ukurasa wa mtu wa mababu.

2. Mara uwapo kwenye ukurasa wa mtu huyo, bofya kichupo cha Sources kilicho juu ya upau wa vyombo.

3. Utaelekezwa kwenye ukurasa wenye orodha ya vyanzo vya mtu. Ili kutazama chanzo, bofya kiungo cha View Source chini ya kichwa cha habari cha chanzo.

4. Baada ya kuwa umebofya View Source, ikiwa unaamini kwamba chanzo sio sahihi, bofya kiungo cha Detach ili kutengua chanzo kutoka kwa mababu.
Kuwa na hakikisho kwamba ikiwa baadaye utagundua kwamba chanzo kilikuwa sahihi, badiliko hili linaweza kutenguliwa kwenye kisanduku cha Latest Changes (kilichopo upande wa kulia wa ukurasa wa mtu huyo.)
Viungo vya Kuhamisha
Mara nyingi, kiungo kinakuwa kimeambatishwa kwenye mababu wasio sahihi kwenye familia ile ile. Ikiwa unaijua namba ya Utambulisho ya Mtu ya babu ambaye kumbukumbu hizo ni yake, unaweza kuhamisha chanzo kwenda kwenye orodha ya vyanzo ya mtu huyo.
1. Nenda kwenye ukurasa wa mtu wa mababu mwenye chanzo kisicho sahihi kilichoambatishwa na kisha kwenye kichupo cha Sources upande wa juu wa ukurasa wa mtu.
2. Tafuta chanzo kisicho sahihi kutoka kwenye orodha ya vyanzo. Bofya View Sources.
3. Chagua Review Attachments kutoka kwenye chaguzi zilizotolewa, ambazo hufungua ukurasa wa chanzo kinachounganisha.
- Tazama: ikiwa Review Attachments sio uchaguzi, basi sehemu ya “kiungo cha kuhamisha” hakipo kwa kumbukumbu hii, lakini unaweza kuambatisha kumbukumbu kwa babu sahihi kwa njia nyingine.
4. Kwenye kona ya juu kulia, bofya Not your family? Tafuta familia yako.

5. Dirisha la kutokea litaonekana ambalo linasomeka Tafuta Find a Match in Family Tree upande wa juu. Kutokea hapa, unaweza ama kuchagua babu wa karibuni kutoka kwenye History List, au unaweza kuingiza Utambulisho wa Mtu wa mababu unayetaka kumwaambatishia chanzo hiki.

Shiriki

Kwa kawaida unaweza kupata jina la mtu aliyetengeneza au aliyetoa kiungo. Unaweza kupata jina hili kwa kwenda kwenye ukurasa wa Mtu wa mababu, ukichagua kichupo cha Sources juu ya ukurasa, na kutafuta safu ya Created By upande wa kulia wa orodha ya chanzo.
Katika safu ya Created By, utapata jina linalohusiana na kila chanzo cha kumbukumbu. Chagua jina hili ili kupata taarifa yoyote iliyopo ya mawasiliano au tuma ujumbe mfupi kupitia FamilySearch. Mawasiliano haya yanaweza kuwa njia ya kutatua mkanganyiko wo wote au kutoelewana kunakotokea kwa mababu.
Kumbuka kuwa na staha na heshima wakati unaposhirikiana na wengine. Mojawapo ya mambo bora zaidi kuhusu nasaba ni nguvu yake ya kuzileta familia pamoja na fursa hii ya kuwasiliana inaweza kukuza roho hiyo ya umoja.