Jinsi ya Kutumia Utambulisho Binafsi wa FamilySearch

girl-and-grandpa-on-john-deere

Unapotafiti mti wa familia yako, unaweza kuwa umeona muunganiko wa herufi na namba chini ya kila jina la mwanafamilia.

Hizi ni namba za utambulisho binafsi (ID), na kuelewa hivi ni vitu gani na jinsi gani unaweza kuvitumia inaweza kuwa rasilimali kubwa sana kwako unapofanya historia ya familia yako!

Utambulisho Binafsi ni nini na Wapi Ninaweza Kuupata?

Kila mtu katika Mti wa Familia wa FamilySearch ana Utambulisho Binafsi, unaojitokeza kama mfuatano wa herufi na namba. Utambulisho huu Binafsi ni wa kipekee kwa kila mtu aliyefariki.

Unaweza kupata namba ya utambulisho chini ya jina la mtu kwenye mti wako wa familia au upande wa juu wa ukurasa wa mtu.

Utambulisho Binafsi katika Mti wa Familia

Ni jinsi Gani Ninaweza kutumia Utambulisho Binafsi?

Kunakili Utambulisho Binafsi

Inaweza kuwa yenye msaada kujua Utambulisho Binafsi wa mababu, hususani kama unapanga kurudi kwenye taarifa za mtu huyo (zaidi kuhusu hili litakujia baadaye). Ili kunakili Utambulisho Binafsi kwa haraka, fuata hatua hizi:

1. Bofya au gusa kwenye person ID, ambayo unaweza kuipata chini ya jina la mtu huyo katika mti wa familia au kwenye ukurasa binafsi wa mababu.

2. Ujumbe utakuja unaosema “Copy ID.” Kunakili Utambulisho Binafsi, bofya kiunganishi hiki.

Picha ya skrini ya kipengele Copy ID

3. Weka namba ya Utambulisho kwenye nyaraka au popote unapotunzia kumbukumbu za Utambulisho Binafsi.

Zilizotazamwa Karibuni

Unaweza kutumia kipengele cha Recents katika Mti wa Familia na Utambulisho Binafsi wa mababu ili kurudi kwa haraka kwenye ukurasa wa mababu. Inachukuwa hatua chache rahisi tu.

Picha ya skrini ya kipengele cha Recents katika mti wa familia.

1. Kwenye mti wako wa familia, bofya au gusa kwenye kichupo cha Recents kwenye upande wa juu kushoto wa skrini.

2. Menyu tiririka itatokea na kukupa uchaguzi wa kuandika au kuweka jina la mwanafamilia au Utambulisho Binafsi. Ingiza Utambulisho Binafsi.

3. Bofya Go. Kama namba ya utambulisho ni sahihi, ukurasa ule wa mababu utafunguka.

Tafuta

Kama tayari unajua Utambulisho Binafsi wa mwanafamilia mahususi unaweza pia kutumia Utambulisho Binafsi kutafuta ukurasa wake binafsi:

1. Gusa au vinjari juu ya Family Tree Upande wa juu kushoto wa skrini, na chagua Find , kutoka chaguzi za menyu.

2. Gusa au bofya Find by ID, na ingiza namba ya utambulisho binafsi katika eneo lililotolewa. Kisha bofya Find. Jina la mtu aliyepangiwa utambulisho huo mahususi litatokea kwenye skrini inayofuata.

Picha ya skrini ya kipengele cha tafuta kwa utambulisho kwenye Mti wa Familia.

3. Kutoka kwenye skrini hii, una uchaguzi wa kubofya majina yoyote yanayohusiana zaidi, ambayo kisha yatakupeleka kwenye ukurasa huo wa mababu.

Ukurasa wa matokeo ya Tafuta kwa Utambulisho.

Unganisha

Wakati mwingine, badala ya kutegemea kifaa cha Rudufu Yamkini, unaweza kutumia utambulisgo binafsi kuunganisha pamoja watu rudufu katika mti. Kufanya hivi, utatumia uchaguzi wa Merge by ID kutoka kwenye kipengele cha Tools upande wa kulia wa ukurasa wa mtu.

Picha ya skrini ya kipengele cha Unganisha kwa utambulisho kwenye ukurasa wa mtu.

1. Nakili au andika utambulisho binafsi ya kumbukumbu ambayo hutaki kuitunza.

2. Kutoka kwenye ukurasa wa mtu ulio na kumbukumbu sahihi zaidi, shuka chini, na katika chaguzi za menyu kulia, bofya au gusa Merge by ID katika kipengele cha Tools .

3. Katika eneo lililotolewa, ingiza namba ya utambulisho binafsi uliyonakili au kuandika. Kumbuka, huu ndiyo utambulisho binafsi ambao una taarifa chache zilizo sahihi. Bofya au gusa Continue.

Picha ya skrini ya Unganisha kwa Utambulisho.

4. Mpaka hapa, utaona maelezo mafupi kutoka kwenye kumbukumbu zote mbili kwa pamoja na utaweza kufananisha zote mbili, na kunakili taarifa yoyote unayopenda kuitunza. Rejea upya taarifa yote.

5. Mara utakapokuwa umepitia akaunti zote mbili kwa umakini, bofya au gusa Continue Merge chini ya skrini.

6. Utatakiwa kuelezea sababu za kwa nini kumbukumbu hizi mbili zinapaswa kuunganishwa. Utakapokuwa umeingiza sababu za maelezo yako, bofya au gusa Finish Merge.

7. Sasa umekamilisha mchakato wa kuunganisha mtu rudufu kwa kutumia utambulisho binafsi.

Tafiti Mti Wako

Kwa kuwa sasa unajua utambulisho binafsi ni kitu gani na nini unaweza kukusaidia ufanye, tembelea mti wako wa familia na tafuta njia za kuweka elimu yako ya utambulisho kwenye matumizi!

Mengi Zaidi kuhusu Jinsi ya Kutumia Mti wa Familia

authorBy  FamilySearch
May 30, 2023
Mti wa Familia wa FamilySearch ni nyenzo ya kustaajabisha inayoweza kukusaidia upange taarifa zinazohusu familia yako na ujifunze zaidi kuwa…

aboutContributorHeading