Jihusishe
Jaribu shughuli hii kusaidia kuleta utofauti kwa ajili ya watafiti ulimwenguni kote.
Kufanya Faharasa ni nini?
Kufanya faharasa ni mradi wa kujitolea ambao hutengeneza picha za kumbukumbu za kihistoria—kama vile taarifa za sensa au tanzia—zipatikanazo mtandaoni. Ni njia nzuri ya kutoa kwa jamii ya vizazi na kufanya ugunduzi wa familia uwezekane.
Jinsi inavyofanya kazi
Picha isiyo na kielezo ya kumbukumbu ya kihistoria haiwezi kupatikana katika utafutaji. Hakuna maneno msingi yanayohusiana nayo yanayoweza kupatikana.
Mfaharasa wa kujitolea hutazama kumbukumbu katika programu ya faharasa na kuandika taarifa muhimu, kama majina, tarehe na mahali. Kama matokeo, picha yenye kielezo huongezwa kwenye kumbukumbu za kutafutwa zinazopatikana bure kwenye FamilySearch.
Kufanya Faharasa kumedhaminiwa na kuanzishwa na FamilySearch, huduma inayotolewa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.
Ujaribu
Tembelea ukurasa wa nyumbani wa Faharasa ili kuingia kwenye FamilySearch na chagua “kundi” la picha la kufanyia faharasa. Kuna miradi inayopatikana katika lugha nyingi tofauti. Tumia muda mwingi au mchache kwa kadiri ulivyo na nafasi. Kuna nyenzo za msaada zilizojumuishwa kwenye mfumo kwa ajili ya kujibu maswali.