Ni wapi ninaweza kutazama, kuchapisha, au kuhariri taarifa kutoka kwenye kijitabu changu cha Familia Yangu?

Share

Kijitabu "Familia Yangu: Hadithi Ambazo Hutuleta Pamoja" ni chombo cha kukusanya na kutunza hadithi yako ya familia. Kijitabu hiki kinapatikana katika muundo wa karatasi. Unaweza kupata kijitabu katika lugha ya

Kibulgaria, Kicheki, Kidenmaki, Kijerumani, Kigiriki, Kiingereza, Kiestonia, Kifiji, Kifini, Kifaransa, Kimalagasi, Kikroeshia, Kihaiti, Kihangari, Kiarmenia, Kiindonesia, Kiitaliani, Kiitaliano, Kiaisilandi, Khmer, Kilithuania, Kilatvia, Kimasedonia, Kimongoli, Kimalay, Kidachi, Kinorwei, Kipolishi, Kiromania, Kislovakia, Kisloveia, Kisamoa, Kialbania, Kiserbia, Kihispania, Kiswidi, Kithai, Kitonga, Kiukreini, Kivietinamu na Kichina kilichorahisishwa.

Unaweza kupata nakala katika sehemu nyingi:

Kijitabu cha kidijitali

Mnamo tarehe 4 Novemba 2019, FamilySearch ilisimamisha utoaji wa toleo la kidijitali la kijitabu. Unaweza kutazama na kuhariri taarifa kwenye FamilySearch.org. Huko unaweza pia kuchapisha chati za ukoo, chati za umbo duara na kumbukumbu za kundi la familia.

  • Picha na hadithi: Tafuta picha zako na hadithi katika Galeri yako ya Kumbukumbu na katika app ya simu ya Memories.
  • Wanafamilia: Tafuta taarifa kuhusu wanafamilia katika Mti wa Familia. Unaweza kuona Mti wa Familia mtandaoni, kwenye app ya simu ya Family Tree, na kwenye Family Tree Lite.
    • Kama huoni taarifa kwenye Family Tree, ziweke tena. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Hata kama ni lazima uwaongeze wanafamilia tena, picha na hadithi ziko katika Galeri yako.

Ili kuingiza data kutoka kwenye kijitabu kwenda FamilySearch, tunapendekeza kwamba utumie Mti mzima wa Familia kwenye tovuti ya FamilySearch.org au Family Tree Lite

Makala zinazohusiana

Ninawezaje kupakua app za simu za FamilySearch?
Ninawezaje kutumia kumbukumbu za FamilySearch kuhifadhi hadithi za maisha ya mababu zangu?
Ninawezaje kuchapisha chati za umbo la duara na chati za ukoo katika Mti wa Familia?
Ninawezaje kumuongeza mwanafamilia kwenye ukoo katika Mti wa Familia?

moduleTitle