Nasaba kwa ajili ya Wanaoanza: Njia 3 Rahisi za Kuanza Sasa

genealogy-for-beginners

Acha tukabiliane nayo: nasaba inaweza kuwa vigumu kuandika, achilia mbali kuifanya. Huenda unaona kama jambo la kutisha. Huenda siku zote umefikiri kwamba ulipaswa kuwa mtaalamu au uwe na mtaalamu afukuwe mizizi ya mti wako wa familia. Hiyo isingeweza kuwa mbali na ukweli. Unaweza kutenda hivyo pia—sasa hivi.

Wakati ni kweli kwamba matawi fulani ya mti wako yatahitaji kupandwa na wakati ni kweli kwamba baadhi ya yale yaliyozeeka na kuviringika yanaweza kuwa ya kutisha, hiyo sio vyote katika kugundua hadithi ya familia yako.

Unaweza kufanya vitu rahisi leo ili kuanza kufunua—na kusimulia—hadithi ya familia yako. Hata hivyo, taarifa ndogo za kila siku, tunazogundua kuhusu babu zetu huleta tofauti.

1. Anza Pale Ulipo

Wakati inapokuja kwenye nasaba kwa ajili ya wanaoanza, kumbuka kwamba nasaba yako inaanza na wewe. Usiogope kuanza kidogo kidogo Hapa kuna maswali ya kuanza nayo:

  1. Ni kumbukumbu gani ulizonazo kuhusu familia yako?
  2. Ni kumbukumbu gani familia yako ya karibu wanayo kuhusu jamaa zako?
  3. Ni kwa jinsi gani babu na bibi yako walikutana?
  4. Ni wapi wazazi wako walienda shule?
Msichana akifanya kazi ya nasaba na bibi yake.

Unaweza kustaajabu ni kwa kiasi gani unaweza kujifunza kwa kuchukua muda tu kukaa na mtu fulani kukumbuka mambo yaliyopita. Hakisha kwamba unapata njia kurekodi hadithi hizi, kama unatumia kalamu na karatasi, video ya kamera kwenye simu yako au chombo cha kurekodi. Utafurahi ulifanya.

Mara utakapokuwa umerekodi hadithi za familia yako, hakikisha kuzitunza kwenye Family Search Memories. Kufanya hivyo kutazitunza sio tu kwa ajili yako, bali kwa ajili ya familia yako yote kuziona.

2. Peleleza Vyanzo vya Sehemu Yako

msichana mdogo kwenye kompyuta

Hauhitaji kwenda popote kuanza utafiti wako. Kama una simu au kompyuta mpakato na intaneti unaweza kuanza sasa hivi!

Je, unavyo vitabu vyovyote ambavyo vimerithishwa kwako? Waulize wanafamilia kama wana picha ya zamani yoyote, nyaraka, au shajara zozote. Unaweza pia kupeleleza maktaba ya mahali unakoishi.

Hata kama familia yako siyo ya kutoka eneo lile, fikiria kupeleleza kitabu ambacho kina matukio ya kihistoria au kipindi cha muda ambacho unafikiri kinaweza kuwa na matokeo ya babu—au hata ya wazazi au maisha—ya babu/bibi. Au kirahisi pekua mtandao kwa ajili ya maana ya jina lako la mwisho. Hata hatua hizi ndogo zinaweza kukusaidia kuanza kuunga vipande pamoja vya wapi ulitokea.

Ukitumia kile ulichogundua, unaweza pia kufikiria kupekua mkusanyiko wa kumbukumbu ya FamilySearch. Kwa hata kipande kidogo cha taarifa kuhusu babu yako, unaweza kugundua dazeni za kumbukumbu kuhusu familia yako.

3. Endeleza Urithi

Si sawa kwamba watu kwenye mti wako wa familia walidhamiria kuwa mababu wa kuvutia sana kwenye sensa. Kama wewe, walikuwa wanaishi tu maisha yao. Leo, tunaishi katika ulimwengu wenye shughuli nyingi. Usisahau kuchukua muda kutengeneza tabia za familia, hata kama ni za kawaida kama kula aiskrimu siku ya Jumamosi mchana.

Kumbuka kuwepo katika maisha ya wale wanaokuzunguka na kuandika matukio ya familia yako. Kuchukua muda kujifunza kuhusu familia, iwe ni ya zamani au ya sasa, inaongeza ladha zaidi na maana kwenye maisha.

kikundi kinacheza mpira wa kikapu pamoja

Kwa hiyo usifanye kiholela, unaweza kuwa mzuri zaidi katika hili kuliko unavyojifikiria. Hata hivyo, hakuna mtu ambaye ghafla anaamka siku moja kama mwananasaba mahiri. Njia pekee ya kujifunza zaidi ni kuchagua sehemu ya kuanzia.

Je, unahitaji mawazo zaidi? Peleleza FamilySearch Discovery Center, na kumbuka kwamba kitu muhimu zaidi kuhusu nasaba kwa wanaoanza ni kuanza.

aboutContributorHeading