Je, umewahi kuwaunganisha pamoja kimakosa watu wawili kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch na kisha baadaye ukatambua hukupaswa kufanya hivyo? Au je, jamaa mwenye shauku amekwenda kwenye shamrashamra za kuunganisha na wewe ukapewa kazi ya kurekebisha miunganiko isiyo sahihi? Vema, makala hii itakusaidia ukamilishe mchakato huo.
Kutafuta miunganiko kwenye Mti wa Familia

Kuna njia rahisi ya kutambua ikiwa mhusika wako ameunganishwa popote.
Wakati kumbukumbu mbili zinapokuwa zimeunganishwa, mojawapo inabakia kwenye Mti wa Familia wakati nyingine ikiwekwa kwenye makavazi. Mabadiliko haya na mengine hukusanywa na yanaweza kutazamwa.
Kwenye ukurasa wa mtu wa mtu yeyote aliyefariki kwenye Mti wa Familia, utaona menyu ya mtiririko Latest Changes kwenye upande wa kulia. Chini ya chombo Latest Changes unaweza kuona mabadiliko kwenye ukurasa wa mtu huyu. Mabadiliko yanaweza kujumuisha vyanzo vilivyoambatishwa, watoto walioongezwa, matukio ya wanandoa, makazi yaliyoongezwa na miunganiko.
Mabadiliko ya hivi karibuni yanaweza kuonekana kutoka kwenye skrini hii. Hata hivyo, mabadiliko yote yanaweza kuonekana kwa kubofya Show All.
Zaidi, utaweza kuona wakati badiliko fulani lilipofanywa na mtu aliyelifanya.
Kurekebisha Miunganiko Isiyo Sahihi kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch
Ikiwa muunganiko umefanyika karibuni, utaonekana kwenye kipengele cha Latest Changes .
Ili kubatilisha, bofya kwenye Merge Completed. Kwenye skrini inayofuata, bofya tu Unmerge upande wa kulia. Hakikisha unajumuisha kauli ya sababu ya kubadilisha muunganiko wa kumbukumbu.


Taarifa zote za zamani kisha zitarejeshwa kwa watu wote wawili anayebaki na aliyefutwa.
Kuunganisha au kubatilisha muunganiko inaweza kuwa ya kuleta mkanganyiko lakini ni mchakato muhimu na si miunganiko yote haiwezi kutenguliwa kwa kutumia njia hii. Kwa msaada zaidi kwenye mchakato wa kuunganisha au kusafisha mti wako wa familia, tafuta makala zifuatazo zenye usaidizi:
- Kuwaunganisha Watu kwenye Mti wa Familia wa FamilySearch
- Jinsi ya Kutumia Utambulisho Binafsi wa FamilySearch
- Ni kwa Jinsi Gani Ninaunganisha Kumbukumbu Zilizojirudia kwenye Mti wa Familia