Kama umeshajaribu Ordinances Ready au umeshaulizwa kuhusu hili na waumini wa kata yako, tawi au kigingi, yawezekana unatafuta majibu kuhusu jinsi hiki kipengele kinavyofanya kazi au kwa nini kinafanya kazi kwa njia fulani.
Hapa kuna baadhi ya majibu kwa ajili ya maswali yanayoulizwa kila mara kutoka kwa washauri wa hekalu na historia ya familia na wengine walio na miito ya hekalu na historia ya familia kote duniani. Tunatumaini majibu haya yatakusaidia wewe katika wito wako unapowasaidia wengine kuwa na uzoefu wa kuvutia wa hekaluni.
Bofya Swali ili Kupata Majibu ya Hapo Chini
- Ordinances Ready ni Nini?
- Ni kwa jinsi gani ninaweza kuwasaidia wengine kutumia Ordinances Ready?
- Je, ninaweza kutumia Ordinances Ready kuhifadhi nafasi ya ibada zote kwa ajili ya mtu?
- Je, Ordinances Ready inakagua kama kuna kujirudia?
- Kwa nini Ordinances Ready inanipatia majina ya watu nisiohusiana nao?
- Je, Ordinances Ready inaweza kunisaidia kuwajua wahenga wangu vyema?
- Kwa nini Ordinances Ready inanipatia majina ya watu wasio na vyanzo?
- Je, ninaweza kutumia tarehe ya makadirio wakati ninapohifadhi nafasi ya ibada za hekaluni?
- Je, kukadiria tarehe hakutasababisha makosa?
- Na ni wakati gani mwafaka wa kukadiria tarehe?
- Ni kwa jinsi gani kukadiria tarehe kunaathiri upekuaji wa kujirudia?
- Je, ibada zote zinazopatikana kupitia Ordinances Ready huisha muda wake baada ya siku 90?
- Ni mapema kiasi gani nitapokea ujumbe kwamba muda wa ibada utaisha?
- Ni kwa jinsi gani nitafanya upya uhifadhi nafasi ambao unakaribia kuisha?
Je, una swali ambalo haukuliona hapa? Weka maoni hapo chini, au tembelea Kituo cha Msaada kwenye FamilySearch.
S: Ordinances Ready ni Nini?
J: Ordinances Ready ni chombo cha FamilySearch ambacho hurahisisha kupata majina kwa ajili ya hekalu. Hukusaidia kupata ibada zinazopatikana na kuzihifadhia nafasi, kujifunza zaidi kuhusu mtu unayemfanyia ibada na kuchapisha kadi za uhifadhi nafasi. Unaweza kuipata kwenye aplikesheni ya Mti wa Familia na kwenye FamilySearch.
Jifunze zaidi kuhusujinsi ya kutumia Ordinances Ready.
S: Ni kwa jinsi gani ninaweza kuwasaidia wengine kutumia Ordinances Ready?
J: Mojawapo wa njia bora za kuwafundisha wengine kuhusu Ordinances Ready ni kuwahimiza wao kuijaribu. Kwa njia hiyo, wanaweza kuhifadhi nafasi kwa ajili ya majina yao wao wenyewe na kuhisi kujiamini kwamba wanaweza kufanya hivyo tena kwa ajili ya safari yao ijayo.

Hali ya Msaidizi kwa ajili ya Ordinances Ready
Ordinances Ready pia ina hali ya msaidizi inayopatikana kwa washauri. Ili kupata hali hii, ingia kama msaidizi kwanza (ukitumia anwani ya barua pepe au namba ya msaidizi). Kisha nenda kwenye kichupo cha hekalu kwenye FamilySearch ili kutumia Ordinances Ready. Unapomaliza, ibada zitahifadhiwa nafasi katika jina la mtu ambaye unamsaidia.
Ili kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kutumia Ordinances Ready na jinsi ya kuhifadhi nafasi za ibada, tazama nyenzo hizi.
- Ni kwa jinsi gani ninapata majina ya familia kwa ajili ya hekalu yaliyo na Ordinances Ready?
- Jinsi Gani Ordinances Ready Inawahamasisha Waumini Ulimwenguni Kote

S: Je, ninaweza kutumia Ordinances Ready kuhifadhi nafasi ya ibada zote kwa ajili ya mtu?
J: Kipengele cha Ordinances Ready hutafuta nafasi za kutosha zilizohifadhiwa kwa ajili ya kipindi kimoja cha hekalu (ubatizo mara 4–5, Endaumenti 1, na kadhalika.)
Kama ukihifadhi ibada moja kwa ajili mtu aliye na Ordinances Ready na ungependa kuhifadhi zingine pia, unaweza kubofya kwenye jina la mtu huyo ili kujua zaidi kuhusu mtu huyo katika Mti wa Familia. Kutoka kwenye Mti wa Familia, unaweza kuhifadhi nafasi ya ibada zingine ambazo zinaweza kupatikana.
S: Je, Ordinances Ready inakagua kama kuna kujirudia?
A: Ndio. Ordinances Ready hukagua kwa ajili ya kujirudia kwa taarifa ya majina inayopata, isipokuwa uhifadhi nafasi utokane na orodha binafsi ya uhifadhi nafasi (katika hali hiyo, ukaguzi unaohitajika unapaswa kuwa tayari umekamilika). Maelezo ambayo hutokea kwa kujirudia yamkini yakiwa yanaoana kwa karibu sana hayataonyeshwa katika Ordinances Ready.
Katika baadhi ya hali, maelezo ya kujirudia yanaweza kuwa yaliongezwa kwenye Mti wa Familia baada ya ukaguzi wa taarifa za kujirudia kufanywa. Kama unapata hali kama hii katika uhifadhi nafasi wako, unaweza kuunganisha maelezo ya kujirudia ili kuhakikisha kwamba ibada kwa niaba ya wahusika zinafanywa mara moja tu.
S: Kwa nini Ordinances Ready inanipatia majina ya watu nisiohusiana nao?
J: Wakati Ordinances Ready inapokuwa haiwezi kupata nafasi ya hekalu kwa ajili ya mojawapo wa jamaa zako, inakusaidia kuandaa safari yako ijayo ya hekaluni kwa kupata uhifadhi nafasi ambayo waumini wengine wa Kanisa wameshiriki na hekalu.
Kipengele cha Ordinances Ready hutafuta nafasi za hekalu kwa utaratibu huu:
- Orodha yako binafsi ya uhifadhi nafasi ya hekalu na uhifadhi nafasi uliofanywa na hekalu.
- Uhifadhi nafasi kwa ajili ya jamaa zako ambao umefanywa hekaluni na wengine.
- Watu mnaohusiana katika upande wako (au mti) ambao wameomba ibada zinazopatikana.
- Uhifadhi nafasi ambao waumini wengine wamefanya hekaluni.

Kama Ordinances Ready haipati jina la familia linalohusiana kwa ajili yako, unaweza kujaribu baadhi ya hatua hizi ili kujua zaidi kuhusu mababu zako mwenyewe na kugundua kama wana taarifa za kutosha za utambulisho ili kazi zao za ibada zikamilike:
- Kama haujajiunga mwenyewe na mababu zako katika Mti wa Familia wa FamilySearch, Ordinances Ready inaweza isipate mababu zako. Jifunze jinsi ya kujaza katika mti wako wa familia kwenye FamilySearch.
- Chunguza mti wako wa familia kwenye FamilySearch, na utafute ikoni za hekalu za rangi ya machungwa. Ikoni hizi zinaonyesha mababu zako ambao bado wanahitaji taarifa za ziada kuongezwa katika maelezo yako kabla ibada hazijaombwa kwa ajili yao. Unaweza kutumia vidokezo vya kumbukumbu nambinu za msingi za utafiti ili kugundua zaidi kuhusu mababu hawa na kujaza taarifa zinazohitajika.
- Labda baadhi ya mababu zako hawapatikani kutoka kwenye mti wako? Unaweza kutumia chati yenye mwonekaono wa feniili kuona nafasi kwa urahisi (mpaka vizazi 7) pahali ambapo huenda pako wazi katika mti wako. Jifunze jinsi ya kuongeza vizazi vyako vinne vya kwanza kwenye mti, au kujaza mapengo kurudi nyuma kwa kupata kumbukumbu zisizopatikana.
S: Je, Ordinances Ready inaweza kunisaidia kuwajua mababu zangu vyema?
J: Kutumia Ordinances Ready na FamilySearch, unaweza kuona historia ya maisha, hadithi, matukio ya maisha na hata picha kwa ajili ya mtu ambaye unakamilisha ibada kwa niaba yake (kutegemeana na kile kilichoongezwa katika Mti wa Familia). Hii inamaanisha unaweza kuwajua watu hawa kama ni ndugu zako au jina ambalo mtu mwingine ameshiriki na hekalu. Hivi ndivyo jinsi unavyofanya:
Baada ya kubofya kitufe cha kijani cha Ordinances Ready, kipengele hiki kitakupatia orodha ya watu ambao kwa ajili yao unaweza kuhifadhi nafasi za ibada. Bofya Tazama Uhusiano chini ya jina ili kuona jinsi mnavyohusiana, na ubofye Tazama Mtu ili kuona matukio ya maisha, kumbukumbu na picha katika Mti wa Familia.

hakikisha kwamba: Mara unapobofya Endeleakatika Ordinances Ready, au kama tayari una ibada zilizohifadhiwa nafasi, unaweza kubofya jina la mtu katika orodha yako ya uhifadhi nafasi ili kujifunza zaidi kuhusu mtu huyo kwenye FamilySearch.
S: Kwa nini Ordinances Ready inanipatia majina ya watu wasio na vyanzo?
J: Ordinances Ready hutumia viwango rasmi vya uhifadhi nafasi vya hekalu. Kabla ya ibada za hekaluni kuhifadhiwa nafasi kwa ajili ya mtu, taarifa za kutosha lazima ziongezwe kwenye Mti wa Familia ili kwa kipee kabisa kuweza kumtambua mtu huyo. Jina, tarehe husika, mahali husika, na taarifa zingine lazima ziwepo, lakini chanzo hakihitajiki.

Kumbuka kwamba: Katika sehemu fulani ulimwenguni, kumbukumbu za kihistoria za karatasi na za kidigitali hazikuhifadhiwa mara kwa mara. Utunzaji kwa ajili ya taarifa sahihi na kamili daima unapaswa kufanyika kabla ya kufanya kazi ya ibada, lakini taarifa sahihi za utambulisho zinatosha.
S: Je, tarehe ya kukadiria inaweza kutumiwa wakati ninahifadhi nafasi ya ibada za hekaluni?
J: Wakati tarehe kamili kwa ajili ya mojawapo ya matukio muhimu ya mtu (kama vile kuzaliwa, ndoa na kifo) haijulikani, tarehe ya kukisia inaweza kuingizwa.
S: Je, kukadiria tarehe hakuwezi kusababisha kukosekana kwa usahihi?
J: Wakati nyaraka za kihistoria, shajara na vyanzo vingine vinaweza kusaidia kutambua tarehe mahususi, nyenzo hizi hazipatikani kwa kila mhenga. Wakati unapohifadhi nafasi ya ibada za hekaluni, unaweza kuchukua hatua kukisia kwa usahihi.
Unapokuwa unajua vya kutosha kuhusu mababu na kuwatambua kwa njia ya kipekee lakini hauna tarehe mahususi, FamilySearch hukuruhusu wewe kuongeza tarehe kwa kukisia na kuandika “kabla,” “baada,” au “karibia” pamoja na tarehe ili kuonyesha ni kukisia.
Wakati unapokisia tarehe, tumia kile unachoweza kupata au tayari unajua kuhusu babu yako ili kupata tarehe sahihi ya karibu sana kadiri inavyowezekana. Hivi ni baadhi ya vidokezo vya kukisia tarehe kwa usahihi wa juu.

S: Ni wakati gani mwafaka wa kukadiria tarehe?
J: Kwa ajili ya msaada wa kujua wakati wa kukisia tarehe na jinsi ya kuingiza tarehe ya kukisia katika Mti wa Familia, soma makala hii.
S: Ni kwa jinsi gani kukadiria tarehe kunaathiri upekuaji wa kujirudia?
J: Mti wa Familia wa FamilySearch huchukulia tarehe za kukisia kama rafu. Kwa mfano, “karibia 1880” itachukuliwa kama Januari 1, 1880 hadi Desemba 31, 1880. Katika mfano huu, FamilySearch ingeweza kutafuta kujirudia ambako kunaoana na rafu hiyo ya tarehe.
S: Je, ibada zote zinazopatikana kupitia Ordinances Ready huisha muda wake baada ya siku 90?
A: Ibada ambazo unahifadhi nafasi ukitumia kipengele cha Ordinances Ready kiujumla huisha muda wake baada ya siku 90. Huu muda wa uhifadhi nafasi unajumuisha uhifadhi nafasi wa ibada unaotolewa kutoka katika orodha ya hekalu (wakati mwingine inaitwa majina ya hekaluni) na uhifadhi wa nafasi ambao jamaa yako yawezakuwa alishiriki na hekalu.
Wakati Ordinances Ready inapopata nafasi za hekalu katika mti wa familia yako na hukusaidia kuzihifadhia nafasi, uhifadhi nafasi huu unaisha ndani ya miaka 2.
Wakati uhifadhi nafasi unafanywa nje ya Ordinances Ready, tarehe tofauti tofauti za kuisha muda hutumika.
S: Ni mapema kiasi gani nitapokea ujumbe kwamba ibada itaisha?
A: Wiki tatu kabla ya uhifadhi nafasi kuisha, FamilySearch itatuma ujumbe wa kukumbusha kuhusu muda wa mwisho. Utapokea ujumbe mwingine baada ya uhifadhi nafasi kuisha muda wake. Kama pia unataka kupokea taarifa kwenye barua pepe, washa chaguo la Jumbe katika mipangilio ya taarifa kwenye FamilySearch yako.

S: Ni kwa jinsi gani nitafanya upya uhifadhi nafasi ambao unakaribia kwisha?
A: Ni muhimu kukamilisha ibada ulizozihifadhia nafasi katika wakati uliopangiwa kama unaweza, badala ya kuhifadhi nafasi ya ibada tena. Kama hauwezi kukamilisha ibada, unaweza kushiriki na hekalu ili kuwaruhusu wengine kusaidia kutoa baraka hizi.
Unapokaribia siku unayoweza kuhudhuria hekaluni, unaweza kutumia Ordinances Ready tena kutafuta kuhifadhi nafasi kwa ajili ya jamaa au mtu fulani mwingine ambaye anahitaji ibada kukamilishwa.
Kumbuka kwamba: Ikiwa uhifadhi nafasi wa ibada unaisha muda wake, sio kwamba muda huo umepotea. Uhifadhi nafasi unatolewa kwa hekalu ili wengine waweze kukamilisha ibada. Unaweza kufuta uhifadhi nafasi wa ibada na kuhifadhi nafasi tena, lakini kuna uwezekano kwamba ibada hazitapatikana tena.