Kuongeza vizazi hai kunakuunganisha wewe na mababu zako waliofariki. Kwa mfano, kuongeza wazazi wako walio hai kunakuruhusu kuunganika tena na mababu zako waliofariki.
Kabla haujaanza
Unapoingiza taarifa kuhusu ndugu walio hai, tafadhali fuata miongozo hii:
- Usiingize taarifa yoyote kuhusu watu walio hai bila ruhusa yao.
- Usijumuishe taarifa yoyote ambayo inaweza kuchukuliwa kuwa nyeti. Ili kukusaidia katika juhudi hii, tumezima pia uga kadhaa ambazo zingeweza kufikiriwa kuwa ni nyeti. Haya ni majadiliano, kitambulisho cha kitaifa, rangi, jina la tabaka, jina la ukoo, kabila, bar mitzvah, bat mitzvah, na uhusiano wa kidini.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali pia tazama makubaliano ya mawasilishoya FamilySearch.
Wapi pa kuongeza ndugu walio hai
Tunapendekeza yafuatayo:
- Mti binafsi (Mti wa FamilySearch). Kama unadumisha mti binafsi, ongeza familia yako hai ya kutosha ili kwamba uweze kuunganika na mababu zako waliofariki. Ni wewe pekee unayeweza kuwaona ndugu walio hai kwenye mti wako binafsi.
- Mti wa kundi la Famila. Kama unataka kuongeza taarifa zaidi kuhusu wanafamilia wako walio hai, tunapendekeza kufanya hilo katika mti wa kundi la familia. Hapo, unaweza kuunda kikundi cha familia ili kushiriki taarifa na kukuza ushirikiano na muunganiko kati ya wanafamilia wako.
Taarifa inayohitajika
Ili kuongeza mtu mpya, lazima uingize angalau jina la kwanza au la mwisho, kuonyesha jinsia ya mtu huyo, na kuangalia amefariki au anaishi.
Hatua (tovuti)
- Wakati ukiingia kwenyeFamilySearch.org, bofyaMti wa Familia, na kisha bofya Mti.
- Kama itahitajika, tumia swichi kunjuzi kwenye upande wa juu kulia ili kuchagua mwonekano wa mti ambao unataka kutumia. Kisha endelea chini ya hatua hizi katika sehemu inayohusiana na mwonekano wa mti wako.
- Miti ya kikundi cha familia kwa sasa haiwezi kuonyeshwa kwa kutumia mwonekano wa Babu wa Kwanza, mwonekano wa Uzao, au mwonekano wa Chati ya Feni.
Mionekano ya Wima, Chati ya Feni, Chati ya Uzao
- Bofya jina la mwanafamilia wa karibu.
- Katika maelezo ambayo yanajitokeza, bofya jina la mtu huyo tena.
- Bofya kichupo cha Maelezo ya kina.
- Biringisha kwenye sehemu ya Wanafamilia.
- Bofya kiungo sahihi (Ongeza Mwenza, Ongeza Mtoto, au Ongeza Mzazi).
- Tumia kichupo sahihi kumuongeza mtu huyo:
- Kwa Jina. Ingiza maelezo, bofya Anaishi, kisha bofya Inayofuata. Thibitisha taarifa na bofya Tengeneza mtu.
- Kutoka Mti wa FamilySearch. Bofya kichupo hiki ili kunakili mtu kutoka kwenye mti wako binafsi kwenda kwenye mti wa kundi la familia. Kisha bofya jina la mtu huyo. (Chaguo hili linapatikana wakati wa kuongeza mtu kwenye mti wa kundi la familia.)
- Kwa Namba ya Utambulisho. Kama unajua namba ya utambulisho ya mtu, na kama mtu huyo yuko kwenye mti wako binafsi au mti wa kikundi cha familia ambao wewe ni sehemu yake, bofya kichupo hiki, ingiza namba ya Utambulisho na bofya Inayofuata.
Mwonekano wa Wima
- Tumia mishale kupanua mti ili kuonyesha jina la mwanafamilia unayetaka kumwongeza.
- Fungua chaguo sahihi la ongeza:
- Wazazi. Bofya ikoni ya ^ juu ya kigae cha mtu. Kisha bofya Ongeza Baba au Ongeza Mama.
- Mtoto, mwenza au ndugu. Bofya + ambayo iko kwenye picha ya mtu huyo na uchague chaguo sahihi. (Ili kumuongeza ndugu, mtu huyo lazima aunganishwe na mzazi kwanza.)
- Bofya kichupo sahihi ili kuongeza mtu huyo:
- Kwa Jina. Ingiza maelezo, bofya Anaishi, kisha bofya Inayofuata. Thibitisha taarifa na bofya Unda mtu.
- Kutoka Mti wa FamilySearch Bofya kichupo hiki ili kunakili mtu kutoka kwenye mti wako binafsi kwenda kwenye mti wa kundi la familia. Kisha bofya jina la mtu huyo. (Chaguo hili linapatikana wakati wa kuongeza mtu kwenye mti wa kundi la familia.)
- Kwa Namba ya Utambulisho. Kama unajua namba ya utambulisho ya mtu, na kama mtu huyo yuko kwenye mti wako binafsi au mti wa kikundi cha familia ambao wewe ni sehemu yake, bofya kichupo hiki, ingiza namba ya Utambulisho, na bofya Inayofuata.
Mtazamo wa Babu wa Kwanza
- Mtafute mtu aliye na wanafamilia walio hai unayetaka kumuongeza.
- Juu ya picha ya mtu huyo, bofya ikoni ya +:
- Ili kuongeza mtoto, bofya Ongeza Mtoto.
- Ili kuongeza mwenza, bofya Ongeza Mwenza.
- Ili kuongeza mzazi, bofya Ongeza Mzazi.
- Bofya kichupo sahihi ili kuongeza mtu huyo:
- Kwa Jina. Ingiza maelezo, bofya Anaishi, kisha bofya Inayofuata. Thibitisha taarifa na bofya Tengeneza mtu.
- Kwa Namba ya Utambulisho. Kama unajua namba ya utambulisho ya mtu, na kama mtu huyo yuko kwenye mti wako binafsi au mti wa kikundi cha familia ambao wewe ni sehemu yake, bofya kichupo hiki, ingiza namba ya Utambulisho, na bofya Inayofuata.
Hatua (aplikesheni ya simu ya Mkononi)
- Fungua Katika aplikesheni ya simu ya Family Tree.
- Kama itahitajika, badili kwenye mti ambapo unataka kumuongeza mtu huyo.
- Nenda kwenye ukurasa wa Mtu wa mwanafamilia wa mtu aliye hai.
- Gusa kichupo sahihi (Wenza kwa ajili ya wenza na watoto au Wazazi kwa ajili ya wazazi na ndugu).
- Gusa kiungo sahihi (Ongeza Mtoto, Ongeza Mwenza, Ongeza Mzazi, au Ongeza Ndugu).
- Ingiza taarifa kuhusu mtu huyo, na kisha gusaEndelea.
- Onyesha kwamba mtu huyo Anaishi.
- Ingiza taarifa yoyote ya kuzaliwa, na kisha gusa Endelea.
- Gusa Ongeza au Ongeza Mtu Huyu.
Hatua (Family Tree Lite)
- Katika Family Tree Lite, nenda kwenye ukurasa wa mtu wa mwanafamilia wa mtu aliye hai.
- Bofya Tazama Familia.
- Bofya kiungo sahihi (Ongeza Mwenza, Ongeza Mtoto, Ongeza Mzazi, au Ongeza Ndugu).
- Ingiza taarifa kuhusu mtu huyo. Onyesha kwamba yeye anaishi.
- BofyaInayofuata.
Makala zinazohusiana
Notisi ya Faragha ya FamilySearch
Je, ninaweza kuongeza kumbukumbu kuhusu ndugu zangu wanaoishi kwenye Mti wa Familia?
Je, ni kwa jinsi gani Mti wa Familia unalinda faragha ya watu wanaoishi?
Je, nani anaweza kuwaona ndugu zangu walio hai katika Mti wa Familia?
Ninawezaje kubadilisha hali kutoka aliyekufa kwenda anaishi katika Mti wa Familia?
Je, ninaunganishaje kumbukumbu rudufu kwenye Mti wa Familia?