Kwenye FamilySearch.org, una njia nyingi za kupata uzoefu wa shangwe wa historia ya familia. Sasa kwa vile una akaunti, ni wakati wa kuanza kutafiti baadhi ya vitu vizuri unavyoweza kufanya.
Hapa kuna shughuli tano zinazostahili kujaribiwa.
1. Anza Mti Wako wa Familia
Kama msemo usemavyo, sisi sote tuna uhusiano kama tukirudi nyuma vya kutosha. Kupitia Mti wa Familia wa FamilySearch, unaweza kuona kwa namna gani hili hutimia.
Anza kwa kuingiza jina lako binafsi ndani ya mti, likifuatiwa na wazazi wako. Ongeza taarifa kuhusu babu na bibi yako na hata babu na bibi zao, kama unayo taarifa hiyo. Lengo ni kuunganisha familia yako na ya mtu mwingine.
Unapofanya muunganiko huu FamilySearch itakuongeza kiautomatiki kwenye mti mkubwa wa familia wa watu wote ulimwenguni. Utaweza kuona majina na taarifa unazoshiriki za mababu zako.
Kwa njia hii, Mti wa Familia unakusaidia ugundue historia ya familia yako. Na unapoingiza taarifa kuhusu wewe binafsi na familia yako, unaweza kuwa unawasaidia wengine wagundue historia zao pia—nani ajuwaye!
2.Tafuta Kweli za Burudani kuhusu Wewe kupitia Uzoefu wa Ugunduzi
Sehemu ya historia ya familia ni kujifunza kuhusu wewe mwenyewe—kuona jinsi unavyounganika kwenye ulimwengu unaokuzunguka, kwa washiriki wa familia yako na kwa watu waliokuwepo kabla yako.
Shughuli za FamilySearch za ugunduzi wa mtandaoni zinaongeza ubora wa muunganiko huu kwa nyakati zilizopita. Utajihisi vipi utakapofahamu tabasamu lako juu ya sura za babu aliyepotea siku nyingi, au kusoma maneno kwenye kaburi la babu mkuu?

Kwa kubofya tu kipanya, mkusanyiko wetu wa shughuli za ugunduzi utakupa wewe uzoefu huu na mwingine, kama vile Pata Picha ya Urithi Wangu au Yote Kuhusu Mimi. Shughuli hizi ni za burudani mno unapomwalika mtu mwingine—kama rafiki wa karibu au mwanafamilia—kuzifurahia pamoja nawe.
3. Pekua Kumbukumbu Zetu
Historia ya Familia inakuwa na uhai kwa uwepo wa taarifa, sababu ambayo itakufanya utumie muda kupekua mikusanyo ya nyaraka za kihistoria kwa ajili ya marejeo kwa familia yako na mababu.
Vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya ndoa, matangazo ya tanzia, ripoti za sensa, kumbukumbu za kanisa, kadi—hivi vyote ni vitu muhimu vya familia. Ni ushahidi halisi wa maisha ya mababu zako na ya maisha ya wengine waliochangamana nao.
Kumbukumbu pia zinatoa ishara kuhusu uzoefu wa kila siku wa mababu zako. Kwa kumbukumbu sahihi za kihistoria, unaweza kuwa na uwezo wa kugundua shughuli za mababu, kuona wapi bibi au babu aliishi, na kujua kwa usahihi urefu, uzito na rangi ya jicho.
Unapopata nyaraka ya kihistoria ambazo zinataja mtu unayehusiana naye, hakikisha unaiambatanisha na maelezo yake katika Mti wa Familia kwa ajili ya watu wengine kufurahia.
4. Andika au Pakia Kumbukumbu ya Familia
Sehemu ya historia ya familia ni kutengeneza historia yako mwenyewe—picha, hadithi na hata sauti zilizorekodiwa—kwa ajili ya vizazi vijavyo kufurahia. Kwenye FamilySearch, tunaita vitu hivi “Kumbukumbu,” na tunataka tukusaidie kuvitunza.

Aplikesheni ya FamilySearch Memories na kichupo cha Memories kwenye FamilySearch.org vyote vimetolewa kukusaidia wewe kutengeneza, kupakia, kutazama na kuhifadhi kumbukumbu hizi. Mara zinapohifadhiwa, zinakwenda kwenye kusanyiko lilelile la “Kumbukumbu” ili uweze kuziangalia popote pale.
Kwa kuwa sasa una akaunti, jaribu kupakia picha yako mwenyewe au ya mpendwa wako. Bofya kiunganishi hapo chini kujifunza jinsi ya kufanya hivyo.
5. Saidia Wengine
Hatimaye, ukuwa na akaunti yako ya FamilySearch iliyotengenezwa unaweza kutoa muda na ujuzi wako kwa kufanya faharasa ya kumbukumbu za kihistoria.
Unapokuwa umefanya faharasa ya kumbukumbu za kihistoria, unatazama picha ya kidijitali ya nyaraka halisi—kwa mfano cheti cha ndoa—na ingiza taarifa zake katika mifumo yetu. Unapofanya faharasa ya kumbukumbu, nyaraka na taarifa zake zinakuwa zinaweza kupekuliwa katika Mkusanyiko wa Kumbukumbu wa FamilySearch. Kwa nyenzo hii, watumiaji wengine wanaweza kunufaika na kupata taarifa kuhusu familia zao.
Kufanya faharasa ya kumbukumbu ni njia kubwa mno ya kumsaidia mtu fulani afanye ugunduzi wa historia ya familia. Bofya kiunganisho hapo chini ili kujaribu kufaharisisha—hakika utaleta utofauti chanya kwa wengine.