Niinawaalikaje watu ili kujiunga na kundi la familia?

Share

Kwanza, tengeneza kundi la familia. Kisha, kama msimamizi wa kundi, waalike watu hadi kufikia 99 ili kujiunga.

Wakati unapomwalika mtu mmoja kwenye kundi, FamilySearch hutengeneza kiungo ambachp utatuma kwa mpokeaji mmoja au zaidi ukitumia baruapepe, chati ya kundi, WhatsApp, kundi la mtandao wa kijamii, na kadhalika. Ili kujiunga, mpokeaji anabofya kiungo, anaingia katika FamilySearch, na kufuata maelekezo mtandaoni.

Viungo vya kujiunga haviishi muda. Kama kiungo hakitahitajika kutumika tena, msimamizi wa kundi anaweza kukifuta.

Kabla haujaanza

Kama kundi la familia lina mti wa kundi la familia, kila mtu anayealikwa anapaswa kuongezwa kwenye mti wa kundi kwanza.

Hatua (tovuti)

  1. Kwenye FamilySearch.org, bofya jina lako.
  2. Chagua Makundi ya Familia.
  3. Bofya Tazama Kundi.
  4. Bofya Alika.
  5. Ikiwa unajaua anwani ya barua pepe ya mtu huyu, unaweza kutuma mwaliko kwa njia hiyo.
    1. Bofya Barua Pepe.
    2. Katika programu yako ya barua pepe, ingiza anwani ya barua pepe ya mtu huyo unayemwalika, na utume. Baada ya mpokeaji kukubali mwaliko, jina hutokea kwenye orodha ya kuidhinisha.
  6. Unaweza kumtumia mtu huyu kiungo.
    1. Bofya Nakili Kiungo. Kiungo hutokea.
    2. Bofya Nakili.
    3. Bandika kiungo kwenye mkondo wowote wa mawasiliano wa mtandaoni ambao unashiriki na mtu uliyemwalika.
  7. Subiri mpokeaji akubali mwaliko ule.
  8. Idhinisha ombi la kujiunga:
    1. Fungua kundi.
    2. Tafuta mtu ambaye unasubiri kuidhinishwa. Hii hutokea katikati ya sehemu ya Kuanza na mpasho wa kundi.
    3. Bofya Idhinisha.

Hatua (app ya simu ya mkononi)

  1. Katika app ya simu ya mkono ya Mti wa Familia, gusa ikoni ya laini 3. Kwenye skrini ambayo hutokea, fungua kipengele cha makundi ya familia.
    • iOS ya Apple—chini kulia
    • Android—juu kushoto
  2. Gusa Makundi ya Familia.
  3. Pata kundi ambalo kwalo wewe ni msimamizi, na uguse Tazama Kundi.
  4. Juu ya orodha ya washiriki, gusa ikoni ya mtu.
  5. Utaona orodha ya mawasiliano vile vile njia mbali mbali za kutuma mwaliko. Gusa mtu au mbinu ya mwaliko.
  6. Tuma mwaliko.
  7. Wakati anapokubali mwaliko huu, jina linatokea katika kundi kwa ajili ya kuidhinisha.
  8. Idhinisha ombi la kujiunga:
    1. Fungua kundi.
    2. Tafuta mtu ambaye anasubiri kuidhinishwa.
    3. Gusa Idhinisha.
    4. Gusa Idhinisha tena.

Makala zinazohusiana

Makundi ya familia ya FamilySearch ni nini?
Je, ninatengenezaje kundi la familia?
Je, ninajiungaje na kundi la familia?
Je, ninamuondoaje mtu kutoka kwenye kundi la familia?

moduleTitle