Ninawezaje kupakia kumbukumbu kwenye FamilySearch?

Share
0:00 / 0:00
videoCompanion
How to add photos to a person in a few easy steps | FamilySearch

Unaweza kupakia picha, faili za sauti au nyaraka kwenye FamilySearch Memories, iwe ni kitu kimoja au kama kundi la vitu.

Kabla haujaanza

Kwa uangalifu soma Makubaliano ya Uwasilishaji.

Fomati na ukomo wa ukubwa wa faili

  • Nyaraka: .faili za fomati ya pdf hadi MB 15. Geuza fomati za nyaraka nyingine kama vile faili za .doc na faili .docx ili kuwa .pdf kabla ya kupakia.
  • Picha: fmati za .jpg, .png, .tif na .bmp hadi MB 15.
  • Sauti: .mp3, .m4a, na .wav hadi MB 15

Tafadhali fahamu

  • .pdf ni aina pekee ya faili inayokubalika ambayo inaweza kujumuisha kurasa nyingi.
  • Hariri kumbukumbu, kama vile kupogoa picha, kabla ya kupakia. Baada ya kupakia kitu, huwezi kukihariri.

Hatua kutoka Kumbukumbu (tovuti)

  1. Ingia kwenye FamilySearch.org
  2. Katika upau wa menyu juu ya skrini, bofya Kumbukumbu.
  3. Bofya Galeri.
  4. Bofya alama ya ongeza (+) katika duara.
  5. Buruza na udondoshe maudhui kutoka kwenye kompyuta yako kwenda kwenye skrini, au bofya Chagua Faili.
  6. Gusa picha moja moja. (Ona makala yanayohusiana hapa chini kwa msaada wa ziada.)

Hatua kutoka ukurasa wa Mtu (tovuti)

  1. Ingia kwenye FamilySearch.org
  2. Kwenye upau wa menyu, chagua Mti wa Familia.
  3. Chagua Mti.
  4. Chagua mtu binafsi, kisha chagua Mtu ili uuone ukurasa wa mtu huyo.
  5. Bofya kichupo cha Kumbukumbu .
  6. Bofya Ongeza Kumbukumbu.
  7. Bofya aina ya kumbukumbu:
    1. Sauti: Rekodi sauti yako ili kusimulia hadithi. Unaweza kurekodi hadi dakika 5 kwa kila kumbukumbu ya sauti. Bofya kitufe cha kurekodi ili kurekodi. Unapomaliza, bofya Imekamilika. Kisha bofya Hifadhi.
    2. Hadithi: Pakia hadi picha 10 kutoka Kwenye Kifaa Chako au kutoka kwenye Galeri Yako. Ingiza kichwa cha habari na hadithi. Hadithi zimewekwa kama Umma kwa chaguo-msingi. Ili kutengeneza hadithi kuwa ya faragha, bofya Binafsi. Bofya Hifadhi.
    3. Faili: Pakia faili. Bofya ili kupakia kutoka kwenye Kifaa Chako, Galeri Yako, au Google Photos.

Hatua za kupakia mafaili mengi au picha

Chagua Faili Mfululizo:

  1. Tafuta na bofya kipengee cha kwanza.
  2. Bonyeza kitufe cha Shift kwenye kibodi yako.
  3. Kwa Kitufe cha Shift kikiwa kimebonyezwa, bofya kitu cha mwisho ambacho unataka kupakia.
  4. Unaona orodha ya viambatisho vilivyoangaziwa na tayari kupakia. Fuata maelekezo kwenye skrini na pakia picha.

Chagua Faili Zisizo Mfululizo:

  1. Ili kuchagua picha zisizo mfululizo kutoka kwenye folda, tafuta na bofya picha ya kwanza.
  2. Bonyeza na shikilia Kitufe cha Control (Ctrl).
  3. Na Kitufe cha Control kikiwa kimebonyezwa, bofya vitu vyote ambavyo unataka kupakia. Kisha fuata vishawishi kwenye skrini ili kupakia.

Hatua (app ya simu ya Kumbukumbu)

  1. Gusa alama ya ongeza (+) katika duara.
  2. Gusa Ongeza Nyaraka au Ongeza Picha.
  3. Gusa chaguo unalopendelea kutumia:
    1. Android: Kamera au Faili
    2. Apple iOS: Piga Picha, Mkanda wa Kamera, au Faili Zangu

Chagua faili kutoka chombo chako, na gusa Pakia. Au tumia vipengele vya kamera kupata maudhui. Hariri picha, na gusa Hifadhi.

Hatua (app ya simu ya Mti wa Familia)

  1. Bonyeza ili kufungua ukurasa wa maelezo ya mtu.
  2. Gusa Kumbukumbu.
  3. Gusa ikoni ya alama ya ongeza (+).
  4. Gusa Ongeza Nyaraka au Ongeza Picha.
  5. Gusa chaguo:
    1. Android: Kamera, Faili, au Galeri ya FamilySearch
    2. IOS ya Apple: Piga Picha, Mkanda wa Kamera, Mafaili Yangu, au Galeri ya FamilySearch Yangu.

Chagua faili kutoka kwenye kifaa chako, au kutoka kwenye Galeri, na gusa Pakia. Au tumia vipengele vya kamera kupata maudhui. Hariri picha, na gusa Hifadhi.

Family Tree Lite

Kwa sasa, Family Tree Lite haijumuishi kipengele cha Kumbukumbu. 

Baada ya kumaliza

Kama rangi zinaonesha kugeuzwa (kama hasi) katika FamilySearch, tafadhali ondoa picha. Ibadilishe kuwa fomati tofauti ya faili na ipakie tena.

Tagi kila picha na nyaraka kibinafsi ili iunganishe na mtu binafsi katika Mti wa Familia. Ongeza kichwa cha habari, tarehe ya tukio, mahali pa tukio, na maelezo ili kitu chako cha kumbukumbu kiwe rahisi kupatikana. 

Katika Mti wa Familia, kumbukumbu za mtu zinaonekana katika utaratibu ulioongezwa. Huwezi kubadilisha utaratibu huo.

Makala zinazohusiana

Ninawezaje kuongeza au kuhariri kichwa cha habari cha picha, hadithi, nyaraka au faili la sauti?
Kwa nini picha yangu au hati yangu bado haijapakiwa?
Je, ninawezaje kutagi kumbukumbu za mababu au jamaa zangu kwenye Mti wa Familia?
Ni sheria zipi zinatumika katika kupakia kumbukumbu kwenye FamilySearch.org?

moduleTitle