Mahusiano ya kibaiolojia, wa kambo, wa kuasiliwa na wa kulea ni katika Mti wa Familia

Share

Aina ya uhusiano inatambulisha uhusiano wa mtoto kwa mzazi. Kwa sasa, Mti wa Familia hutoa aina 5 za uhusiano:

  • Kuasiliwa
  • Kibaiolojia
  • Ulezi
  • Uangalizi
  • wa Kambo

Unapomuunganisha mtoto na mzazi, Mti wa Familia unachukulia uhusiano huo ni wa kibaiolojia. Kama sivyo, unaweza kuubadilisha.

Hatua (tovuti)

  1. Kwenye menyu ya juu, bofya Mti wa Familia, na kisha bofya Mti.
  2. Mtafute mtoto wa uhusiano unaotaka kuhariri.
  3. Bofya jina la mtoto Katika maelezo ambayo yanajitokeza, bofya tena jina la mtoto. Utaongozwa hadi kwenye ukurasa wa mtu huyo.
  4. Bofya kichupo cha Maelezo ya kina.
  5. Biringisha hadi kwenye sehemu ya Wanafamilia .
  6. Chini ya Wazazi na Ndugu, tafuta jina la mtoto, na bofya ikoni ya Hariri
    1. Kama uhusiano unaonyesha, bofya Hariri kwa ajili ya mzazi. Bofya mshale chini ili kuona chaguzi. Bofya uhusiano sahihi. Elezea sababu ya mabadiliko yako, na kisha bofya Hifadhi. Unaweza pia kubofya Futa na uondoe aina ya uhusiano.
    2. Unapoona hakuna aina ya uhusiano, bofya Ongeza Aina ya Uhusiano. Chagua aina ya uhusiano, elezea sababu ya badiliko lako, na ubofye Hifadhi.
    3. Ili kuona muhtasari wa maelezo yote ya uhusiano kwa mtoto, bofya Zana, kisha bofya Ona Mabadiliko Yote.

Hatua (Simu ya Mkononi)

  1. Katika app ya simu ya mkononi ya Mti wa Familia, nenda kwenye ukurasa wa Mtu wa mtoto mwenye aina ya uhusiano usio sahihi.
  2. Gusa kichupo cha Wazazi.
  3. Tafuta jina la mtoto, na gusa ikoni ya hariri.
  4. Gusa mshale kunjuzi kwa ajili ya ama mzazi ili kuona aina ya uhusiano wa sasa. 
    • Kubadilisha aina ya uhusiano wa sasa, gusa Hariri.
    • Ili kuondoa aina ya uhusiano wa sasa, gusa Futa Aina ya Uhusiano.
    • Ili kuingiza aina ya uhusiano, bofya Ongeza Aina ya Uhusiano.
  5. Gusa mshale wa chini kwa ajili ya aina ya Uhusiano. Gusa uhusiano sahihi.
  6. Elezea sababu ya mabadiliko yako, na gusa Hifadhi.

Hatua (Family Tree Life)

  1. Ingia kwenye Family Tree Lite.
  2. Nenda kwenye ukurasa wa Mtu wa mtoto mwenye wazazi wasio sahihi.
  3. Chini ya jina la mtu binafsi, bofya Tazama Familia.
  4. Chini ya Wazazi na Ndugu, tafuta jina la mtoto, na gusa Ikoni ya Hariri.
    • Ili kubadilisha aina ya uhusiano wa sasa andika, gusa. Gusa Hariri. Gusa mshale wa chini na kisha gusa uhusiano. Unaweza kuongeza tarehe kwa ajili ya tukio ambalo liliunda uhusiano. Elezea sababu ya mabadiliko yako, na gusa Hifadhi.
    • Kama huoni uhusiano, gusa Ongeza Aina ya Uhusiano. Chagua aina ya uhusiano, elezea sababu ya mabadiliko yako, na kisha bofya Hifadhi.

Makala zinazohusiana

Je, ni kwa jinsi gani ninaweza kuona ni mabadiliko gani yalifanywa kuhusu mtu katika Mti wa Familia?
Je, ni kwa jjnsi gani ninaongeza au kubadilisha taarifa za ndoa katika Mti wa Familia?
Je, ni kwa jinsi gani nitatengua badiliko lisilo sahihi katika Mti wa Familia?
Je, ni kwa jinsi gani ninaongeza wazazi wa kambo, wa kuasiliwa na wazazi waangalizi kwa mtoto katika Mti wa Familia?

moduleTitle