Ni majina mangapi ya familia ninaweza kuyashikia nafas? Je, kuna kikomo cha kushikia nafasi?

Share

Orodha ya majina ya hekaluni ya familia yakoi ina kikomo cha kushikia nafasi cha safu ya maingizo 300. Ingizo linajumuisha jina la mhenga na ibada ulizo shikia nafasi.

Wakati orodha yako inapofikia kikomo hiki, huwezi kushikia nafasi ibada ya ziada mpaka orodha itakaposhuka chini ya kikomo.

Kikomo cha ushikajii wa nafasi kilitumika kwa mara ya kwanza mnamo 2021. Maswali na majibu yafuatayo yanaelezea kikomo kwa undani zaidi.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Kwa nini kikomo cha ushikiaji nafasi kimewekwa?

Katika barua iliyoandikwa 8 Oktoba 2012, Urais wa Kwanza uliwahimiza waumini wenye orodha kubwa “kuyaachilia majina haya kwa wakati muafaka ili ibada muhimu ziweze kufanywa.” Wengi wa wanafamilia wetu waliofariki wanasubiri fursa ya kupokea baraka za ibada kwa niaba ya wafu. Waumini wengi wanahudumu katika mahekalu kote ulimwenguni ili kusaidia katika kazi hii.

Kikomo kipya cha ushikiaji nafasi wa 300 hukuwezesha kusimamia kwa urahisi zaidi orodha yako ya kushikia nafasi. Mabadiliko yanawaruhusu waumini wa Kanisa kwa urahisi zaidi kupata fursa za hekaluni. Kwa nyongeza, huwasaidia wahenga kupokea ibada kwa wakati unaofaa zaidi.

Rais Russell M. Nelson na manabii wengine wa sasa wamesisitiza umuhimu wa kuharakisha kazi ya Bwana ya kukusanya Israeli. Tunao wajibu mtakatifu wa kutoa ibada kwa niaba ya wahenga wetu wenyewe. Kama Kanisa la ulimwenguni kote na washiriki wa familia moja kubwa ya binadamu, tunaweza kusaidiana kutimiza wajibu huu mtakatifu.

Hapa kuna hatua unazoweza kuchukua kama una fursa nyingi za hekaluni kuzimaliza hivi karibuni:

  • Shiriki majina ya familia na wanafamilia, marafiki, au kikundi cha familia
  • Shiriki ushikiaji nafasi na Hekalu Wengine wanaweza kupata jina kutoka Ibada Tayari na Mti wa Familia.
  • Kuacha kushikia nafasi kwa baadhi ya majina

Huwezi kushiriki ibada ambazo umezishikia nafasii kutoka kwenye orodha uliyoshiriki na hekalu. Unapojaribu, unaona ujumbe: "Ibada ambazo hapo awali ulizishiriki na hekalu haziwezi kutolewa tena." Unaweza kuacha kuzishikia nafasi ibada hizi. Unapokosa kushika nafasi ya majina haya, yanarudi kwenye orodha ya pamoja ya mtu ambaye awali aliyashiriki na hekalu.
Wakati orodha yako ya ushikiaji nafasi inapokuwa chini ya kikomo, unaweza kuacha kushiriki ushikiaji nafasi ambao ulikuwa umeshiriki hapo awali.

Huwezi kuacha kushiriki ibada katika hali hizi:

  • Ibada zimekamilika
  • Kadi zilizochapishwa na hekaluni
  • Mtu mwingine anashikia nafasi ya ibada kwa kipindi cha siku 120

Ni nini kinachohesabika kuelekea kikomo cha ushikiaji wa nafasi?

Kila safu kwenye orodha yako ya ushikiaji nafasi inahesabika mara moja, hata wakati safu inapowakilisha ibada kadhaa. Ili kuona namba yako, angalia mwambaa wa kushoto. Nambari baada ya "Ushikaji Nafasi Wangu" ni jumla yako.

Ubatizo, uthibitisho, ibada za mwanzo, endaumenti, na kuunganishwa kwa wazazi kwa ajili ya mtu huonyesha kwenye safu moja na kuhesabu kama ushikaji nafasi mmoja. Ibada ya kuunganishwa na mume au mke inaonyesha katika safu yake ya ushikaji nafasi na inahesabika kama ushikaji nafasi tofauti.

Nini kitatokea ikiwa orodha yangu ya ushikaji nafasi tayari iko juu ya kikomo?

Kama orodha yako tayari ina zaidi ya idadi inayoruhusiwa ya kushika nafasi, zinabaki kwenye orodha yako hadi tarehe yao ya mwisho kutumika. Wakati ushikiaji nafasi unapoisha, ibada zinashirikiwa na hekalu. Jamaa wanaweza kuyapata na kuyashikia nafasi katika Mti wa Familia au kupitia Ibada Tayari.

Kama orodha yako ya ushikiaji nafasi iko chini ya kikomo na hakuna aliyechapisha au kukamilisha kazi, unaweza kuacha kushiriki jina.

Ninawezaje kujua kama orodha yangu ya ushikiaji nafasi inafikia kikomo?

Ili kuangalia orodha zako za ushikaji nafasi, ingia FamilySearch.org, na bofya Hekalu. Bofya Ushikiaji Nafasi Wangu Upande wa kushoto, Ushikaji Nafasi Wangu unaonyesha ni ushikaji nafasi kiasi gani unao. Namba shirikishi haitumiki kwa kikomo chako.

Ikiwa unajaribu kuhifadhi nafasi ya ibada baada ya kufikia kikomo, unaona taarifa kwamba umefikia kikomo.

Ni nini hutokea wakati ninapofikia kikomo cha ushikiaji nafasi?

Unapofikia kikomo, huwezi kushika nafasi ya majina ya ziada ya familia. Ili kutengeneza nafasi kwenye orodha yako, unaweza kushiriki ushikaji nafasi uliopo pamoja na hekalu. Waumini wengine wa Kanisa wanaweza kutumia Ibada Tayari na kukusaidia kukamilisha ibada hizo. Wakati kazi imekamilika, unapata taarifa katika Arifa zako za FamilySearch.

Unaweza kurudisha majina shirikishi ambayo yanabaki bila kukamilika mara tu unapokuwa na nafasi zaidi katika orodha yako ya ushikaji nafasi. Ikiwa ushikaji nafasi wa pamoja unajumuisha ibada ambazo zimechapishwa au kukamilishwa, ibada hizo haziwezi kutoshirikiwa.

Je, kushiriki majina ya familia na hekalu uhesabika kwenye kikomo changu?

Unaposhiriki jina la familia na hekalu, ushikaji nafasi hauhesabiki kwenye kikomo chako.

Je, kushiriki majina na kundi la familia kunahesabu kuelekea kikomo changu?

Unaposhiriki jina la familia na kikundi cha familia, ushikaji nafasi unahesabika kuelekea kikomo chako. Tarehe za kawaida za kuisha muda wa matumizi zitatumika baada ya mahekalu kufunguliwa tena kikamilifu katika awamu ya 4.

Ni kwa jinsi gani kushiriki majina ya familia na ndugu au muumini mwingine wa Kanisa kunahesabika kuelekea kikomo changu?

Unaweza kushiriki majina ya familia na ndugu au marafiki kwa barua pepe au kutuma ujumbe kwa njia ya FamilySearch. Barua pepe au ujumbe wa FamilySearch unaonyesha majina na ibada zinazohitajika. Ikiwa wanakubali ushikiaji nafasi huo, ushikaji nafasi unahamia kwenye orodha yao ya ushikiaji nafasi. Ushikiaji nafasi hauonekani tena kwenye orodha yako, na hauhesabiki kuelekea kikomo chako.

Kama ninashiriki majina ya familia na hekalu, ni kwa muda gani lazima nisubiri wao kukamilishwa?

Ni vigumu kutabiri ni kwa haraka ya jinsi gani kazi ya ibada kwa ajili ya majina yaliyoshirikishwa na hekalu itavyokamilika. Vipengele vinajumuisha idadi ya ibada ambazo wengine wanashiriki na idadi ya waliohudhuria hekaluni. Kwa sasa, endaumenti za wanaume huchukua muda mrefu zaidi kukamilika. Ibada zingine (ubatizo, uthibitisho, na ibada za mwanzo) kwa ajili ya wanaume au wanawake kwa kawaida hazichukui muda mrefu.

Pamoja na Ibada Tayari, wanafamilia na waumini wa Kanisa kote ulimwenguni wanaweza kupata majina kwa urahisi zaidi na kamili ambayo yametolewa kwa hekalu. Pamoja na mahekalu zaidi kujengwa ulimwenguni kote, waumini wengi pia wanaweza kushiriki katika kufanya kazi ya ibada kwa niaba ya waliofariki. Maboresho yanayoendelea kwa taratibu za kushiriki na michakato ya usambazaji pia yatasaidia kufupisha muda wa kukamilika.

Ninapendelea kushiriki kadi za majina ya familia zilizochapishwa pamoja na wanafamilia. Je, ninaweza kupata utofauti wa kikomo cha ushikiaji nafasi?

Kikomo cha ushikiaji nafasi hutumika kwa watumiaji wote.

Fikiria kushiriki majina ya familia pamoja na jamaa zako kwa kutumia kipengele kipya cha kikundi cha familia badala yake. Katika kundi la familia, jamaa wanaweza kuchapisha kadi wakati wakiwa tayari kutembelea hekaluni. Majina unayoshiriki na kundi la familia yanahesabiwa kuelekea kikomo chako. Lakini unaweza kuona ibada kwenye orodha yako na nani alizichapisha. Unaweza kufuatilia maendeleo kwenye mtandao na kupokea taarifa wakati ibada zinapokamilika.

Ikiwa nitashiriki ushikiaji nafasi kwa ajili ya ibada fulani kwa ajili ya mhenga, ni kwa jinsi gani ibada ninazozishika zinahesabika kuelekea kikomo hicho?

Kila safu kwenye orodha yako ya ushikiaji nafasii inahesabiwa mara moja, hata kama inajumuisha ibada nyingi. Vivyo hivyo inatumika ikiwa unashiriki sehemu ya ushikaji nafasi hiyo na wengine.

Ibada ya kuunganishwa na mwenza kwa ajili ya mtu binafsi imejumuishwa kwenye safu tofauti na ibada zingine na daima inahesabiwa peke yake. Ibada zingine zote kwa ajili ya mtu binafsi zimejumuishwa katika safu moja ya ushikaji nafasi. Ushikaji nafasi kwa ajili ya mtu mmoja ambao unajumuisha ibada zote utahesabika kama ushikiaji nafasi 2.

Ni nini kitatokea kama nitashiriki jina la familia pamoja na wengine kwa barua pepe au kutuma ujumbe, lakini inazidi kikomo cha mpokeaji?

Orodha ya kila mtu ya ushikaji nafasi ina kikomo sawa. Waumini wanaweza kukubali majina ya kushiriki wakati orodha yao inapokuwa iko chini ya kikomo.

Kama orodha ya mpokeaji imejaa, majina yanabaki kwenye orodha yako. Unaweza kushiriki ushikiaji nafasi huu pamoja na hekalu au kikundi cha familia.

Kama ninatumia programu nyingine kushika nafasi ya ibada, je, bado kuna kikomo?

Baadhi ya programu ya wahusika wengine hufanya kazi na FamilySearch ili kuwasaidia washiriki kushika nafasi kwa majina ya familia. Programu zinafanya kazi na Mti wa Familia wa FamilySearch na huwa na kikomo sawa.

Baada ya kufikia kikomo, ninawezaje kufuatilia majina ya familia ambayo ninataka kuyashikia nafasi baadaye?

Tumia orodha yako ifuatayo kuwawekea alama wahenga ambao ibada zao unataka kuzishikia nafasi katika siku zijazo. Ili kuwafanya wawe rahisi kupatikana katika orodha, unaweza kuongeza lebo ya Ushikiaji Nafasi wa Hekaluni.

Kwa nini hekalu linatunza kadi yangu ya jina la familia baada ya kukamilisha ibada kwa ajili ya mhenga? 

Kuacha kadi za majina ya familia hekaluni kunawaruhusu wafanyikazi wa hekaluni kuhakikisha kwamba kazi ya ibada hairudiwi na kwamba ibada zinarekodiwa kwa usahihi. Mazoea haya pia husaidia kuzuia kuenea kwa vijidudu na kuondoa muda wa kusubiri baada ya ziara yako ya hekaluni.

Makala zinazohusiana

Ninawezaje kushiriki majina ya familia na hekalu?
Ninawezaje kushiriki majina ya familia yangu na familia yangu kwa barua pepe?
Ni kwa jinsi gani ninaondoa kuhifadhi nafasi au kuachilia majina ya familia kutoka kwenye orodha yangu ya hekaluni?
Ukomo wa muda wa kushika nafasi kwa ajili ya ibada ya hekaluni
Ni kwa jinsi gani ninatumia orodha ifuatayo katika Mti wa Familia kuwafuatilia wahenga wanaohitaji ibada za hekaluni?
Blogi ya FamilySearch
Ninawezaje kushiriki majina ya familia kupitia ujumbe wa FamilySearch?
Je, ninashirikije ibada hizi na kundi la familia?

    moduleTitle