Katika Mti wa Familia, ikoni tofauti huwakilisha hali ya mtu ya ibada za hekaluni.
Ikoni | Maana |
![]() | Ibada hizo iwe zilishirikishwa na hekalu au kushirikishwa na kikundi cha familia ambacho wewe ni mshiriki wake. Unaweza kushikia nafasi ya ibada hizi, na hapo utakuwa na siku 120 za kuzitekeleza. |
![]() | Mtu huyo ana husiano na wewe, na ibada inapatikana ili kuombwa. Una miaka 2 ya kukamilisha ibada hizi. Kama mtu huyo alizaliwa ndani ya miaka 110 iliyopita, ni lazima uombe ruhusa ya ndugu wa karibu aliye hai kabla ya kufanya ibada hiyo. Tafadhali zingatia hisia za watu wengine. Je, kuna mtu mwingine mwenye uhusiano wa karibu zaidi kuliko wewe ambaye angeweza kufanya kazi hii? Pengine unaweza kuwaalika kushiriki. |
![]() | Ibada imeshikiwa nafasi. Ikoni inafuatiwa na tagi fupi yenye taarifa zaidi: Haijachapishwa. Imeshikiwa nafasi, lakini kadi ya jina bado haijachapishwa. Unaweza kujaribu kuwasiliana na mtu aliyeomba ibada hiyo na kuuliza kama anaweza kushiriki pamoja nawe. Imechapishwa Kadi ya jina la familia imechapishwa kwa ajili ya ibada hii mahususi. Kama utaamua kushiriki na wengine ibada hiyo, tafadhali haribu kadi ya jina la familia. Kuharibu kadi kunazuia ibada kutorudiwa. Inashirikishwa. Ulishikia nafasi ibada hii lakini kisha ukaishiriki na mtu mwingine au pengine na hekalu. Unaweza kuacha kushirikisha ibada hii isipokuwa hekalu limechapisha kadi ya jina au mtu mwingine ameishikia nafasi. Inasubiri. Kufanya ibada za hekaluni kwa utaratibu sahihi. Inaendelea inamaanisha kwamba ibada zingine za hekaluni lazima zikamilishwe kabla ya wewe kuweza kufanya ibada ya unayopendelea. |
![]() | Ibada hazipatikani. Mbali na ikoni, tafuta tagi fupi ambayo inaelezea: Taarifa Zaidi Zinahitajika. Kuna kitu kinakosekana. Taarifa lazima ziongezwe au kusahihishwa kwenye kumbukumbu ya mtu huyu kabla ya ibada kufanywa. Haiko Tayari. Mtu anayehitajika amefariki kwa muda usiozidi siku 30. Ibada za hekaluni bado haziwezi kufanyika. |
![]() | Ibada imekamilika au haihitajiki. |
![]() | Hali ya ibada ya mtu haipatikani, au hauhusiani na mtu huyo. Katika baadhi ya hoja, mhenga aliishi kabla ya miaka 200 B. K. Au sera ya faragha huzuia FamilySearch kuonyesha taarifa. Kwa ajili ya kuunganishwa hekaluni, pengine mhenga anakosa mwenzi au mzazi aliyeorodheshwa katika Mti wa Familia, au mwenzi bado anaishi. |
Makala zinazohusiana
Ninaombaje ibada kwa ajili ya mhenga aliyezaliwa katika miaka 110 iliyopita?
Ninawezaje kushiriki majina ya familia na hekalu?
Ninawezaje kushiriki majina ya familia yangu na familia na marafiki kwa barua pepe?
Ni katika hali gani mtoto anafikiriwa "kuzaliwa katika agano" (BIC)?
Hali ya ibada "Haiko Tayari" inamaanisha nini?
Katika Mti wa Familia, "Taarifa zaidi inahitajika" inamaanisha nini?
Kazi ya hekaluni kwa mtoto aliyezaliwa mfu