Dhumuni la jumla la Mti wa Familia ni kukusaidia kugundua familia yako na, kwa upande mwingine, kugundua kiasi fulani kuhusu wewe mwenyewe.
- Mti wa Familia ni tofauti na tovuti zingine za nasaba. Mti wa Familia ni mti mmoja, wa umma unaounganishwa pamoja katika familia. Tovuti zingine zinaruhusu tu watumiaji kutengeneza na kusimamia miti yao binafsi. Katika Mti wa Familia, kila mtu anafanya kazi pamoja kwenye data sawa. Dhumuni letu ni kumuunganisha kila mshiriki wa familia ya mwanadamu.
- Mti wa Familia unafananisha kumbukumbu za kihistoria na watu kwenye mti ili kukusaidia kupata vyanzo kwa ajili ya mtu huyo.
- Mti wa Familia hulinganisha watu wanaofanana kwenye mti ili kukusaidia kupata watu rudufu, ambao unaweza kuwaunganisha.
- Mti wa Familia hutoa zana za ujumbe na ushirikiano, vile vile simu ya bure na usaidizi wa barua pepe, ili kukusaidia kutatua makosa.
- Mti wa Familia huchota kutoka kwenye hifadhidata kubwa na inayokua ya FamilySearch ili kutoa vidokezo vya kumbukumbu. Vidokezo vinakusaidia kuunganisha kwenye vizazi vya awali.
- Sehemu ya Kumbukumbu inaweza kusaidia kukuza muunganiko wa kina kwa mababu. Unaweza kuhifadhi na kushiriki picha na historia.
- Tunataka Mti wa Familia uweze kufikiwa na watu wengi kadiri iwezekanavyo. Kwa kuongezea kwenye tovuti nzima, unaweza kutumia app zetu za simu au tovuti ya Family Tree Lite.
Tumaini letu ni kwamba kupitia Mti wa Familia, tunaweza kufanya kazi pamoja kutengeneza mti wa familia ulio na chanzo kizuri, na wa umma. Tunataka kuwasaidia wanafamilia kuunganika na ndugu waliofariki na walio hai.
Ili kujifunza zaidi kuhusu FamilySearch, au kama unahitaji msaada, tembelea FamilySearch.org/about.
Makala zinazohusiana
Ni kwa jinsi gani ninatuma ujumbe kwa mtu aliyechangia kwenye Mti wa Familia au Kumbukumbu?
Ninawezaje kutumia kumbukumbu za FamilySearch kuhifadhi hadithi za maisha ya mababu zangu?