Ongeza Kumbukumbu za Umpendae kwenye FamilySearch

Asian woman looking at a photograph, ready to gather family photos

Kushiriki kumbukumbu za uwapendao waliofariki inaweza kuwa mchakato wa uponyaji hasa. Inafariji kufungua mti wako wa familia kwenye FamilySearch, kubofya kitufe cha jina na kumbukumbu ya umpendaye, na ona kumbukumbu zako za thamani zikitokea. Pia inaleta hisia nzuri kuongeza kumbukumbu hizo wewe mwenyewe na ona jinsi ulivyoongeza kwenye mti na ulivyoshiriki upendo wako.

Kuna njia nyingi za kushiriki kumbukumbu za uwapendao kwenye FamilySearch. Unaweza kurekodi kumbukumbu zako kwa simulizi, kuandika kumbukumbu zako na kuzipakia kwenye FamilySearch, pakia matangazo ya tanzia, au ongeza picha. Unaweza hata kuongeza programu ya msiba au kumbukizi unayoweza kuwa nayo ya mpendwa wako, kama vile tuzo na vyeti, au hata mapishi maalumu.

Utakapoongeza tofauti yoyote ya hizi kumbukumbu, unalo chaguo la kuruhusu umma kuziona, au unaweza hata kuzifanya za faragha.

Mkusanyiko wa mawe ya kumbukumbu na mshumaa

Hapo chini, tutashiriki mafunzo ya jinsi ya kufanya chaguzi hizi tofauti.

Mwanzo

FamilySearch ina aina tofauti za faili ambazo zinaweza kupakiwa kwenye Memories. Zinajumuisha picha, sauti na nyaraka. Unaweza kupakia hizi kupitia Memories Gallery kwenye tovuti ya FamilySearch, moja kwa moja kutoka mti wako wa familia, au kutumia Memories mobile app. Maelekezo kwa ajili vitu hivyo 3 yatatolewa hapa.

Muhimu: Kabla ya kuanza kupakia kitu, ni muhimu kusoma makubaliano ya kuwasilisha. Hii inakutaarifu jinsi picha zako ulizopakia zinaweza kuoneshwa na taarifa nyingine muhimu.

  1. Nenda sehemu ya juu kwenye FamilySearch.org, na bofya Memories. Kisha kutoka kwenye mtiririko, chagua Gallery
  2. Ingia, au tengeneza FamilySearch akaunti (ni bure). 
  3. Mara unapokuwa ndani ya Memories gallery yako, ndani ya duara la kijani, bofya alama ya ongeza (+).
  4. Kokota na achia maudhui kutoka kompyuta yako kwenda kwenye skrini, au kuchagua faili kwenye kompyuta yako bofya Choose Files.

Pakia Kumbukumbu kutoka Ukurasa wa Umpendaye katika Mti wa Familia:

  1. Nenda kwenye Family Tree kwenye FamilySearch.org, na tafuta mwanafamilia au wanafamilia wako katika mwonekano wa mti wako. (Kama bado hujawaongeza kwenye Mti wa Familia ni rahisi!)
  2. Bofya juu ya jina la mpendwa wako na kisha, kutoka kwenye kinachojitokeza, bofya kwenye jina tena kufungua ukurasa mzima.
  3. Kuongeza kumbukumbu zako, bofya Memories tab.
  4. Bofya Upload Photo au Upload document, na chagua faili kutoka kompyuta yako. 
  5. Kuongeza kitu kwenye ukurasa wa mpendwa wako ambacho tayari umekipakia, bofya Select from Gallery

Pakia kumbukumbu ukitumia Aplikesheni za Simu:

Unaweza kupakia kumbukumbu kutoka kwenye aplikesheni ya simu ya kumbukumbu na aplikesheni ya simu ya Mti wa Familia. Hivi ndivyo unavyofanya kutoka kwenye aplikesheni ya simu ya Kumbukumbu:

  1. Bofya alama ya ongeza (+) katika duara. 
  2. Bofya Add Document au Add Photo
  3. Chagua kati ya chaguzi 2:
    1. Chagua file kutoka chombo chako, na bofya Upload
    2. Tumia vipengele vya kamera kupata maudhui. Hariri picha, na bofya Save

Hivi ndivyo unavyofanya kutoka aplikesheni ya simu ya Mti wa Familia:

  1. Bofya kwa mtu binafsi kufungua ukurasa wa taarifa wa mtu.
  2. Bofya Memories.
    1. Bofya ikoni ya alama ya ongeza (+).
    2. Bofya Add Document au Add Photo.
    3. Chagua kati ya chaguzi 2 tofauti:
      1. Chagua file kutoka chombo chako, na bofya Upload.
      2. Tumia kipengele cha kamera kudaka maudhui. Hariri picha, na bofya Save.

Memories App Inakusaidia Kurekodi na Kupakia Wakati Uleule, Popote Ulipo.

Unapopakia kumbukumbu za wapendwa wako kwenye aplikesheni ya simu, kitu ulichokipakia kitajionesha pia katika toleo la tovuti la kumbukumbu zako. Mojawapo ya vipengele bora kabisa kwenye programu hii, hata hivyo, ni uwezo wa kupakia rekodi za simulizi za historia katika muda halisi. Cha kufanya ni kufungua programu, ingia na bofya Alama ya ongeza kwenye kona ya kulia. Chagua ikoni ya add audio, na skrini itakuja juu ikikutaka uchachague mada—au unaweza pia kubofya Begin Recording ili kurekodi kwa uhuru kuhusu chochote unachokipenda.

Hii ni sehemu ambapo utachagua kuzungumza kuhusu wapendwa wako. Unaweza kushiriki hadithi fupi kuwahusu, unaweza kushiriki kitu fulani walichoandika au kumbukumbu yoyote unayochagua. Una dakika 5 kurekodi kumbukumbu hiyo na kisha itunze kwa jina lolote unalochagua. Mara unapokuwa umefanya hivyo, kisha unaweza kuiambatanisha kwenye kitufe cha memories kwa kubofya kwenye rekodi na kuwatagi wao.

Unaweza pia kubofya kwenye picha ya umpendaye na kuongeza simulizi ya sauti.

Kwenye aplikesheni ya Memories, picha zinaweza kupakiwa kutoka Facebook, instagram, au picha zako mwenyewe. Hii ni njia kubwa kusaidia mchakato wa kuomboleza wakati unahisi kutokuwa na furaha na una dakika chache za kupitia picha — kuziongeza kwenye aplikesheni yako ya memories yako hufanya hivyo ili wengine waweze kuziona picha na kuziweka zote kwenye sehemu moja kwa ajili yako kuziangalia na kufurahi pia.

Jifunze zaidi kuhusu Memories app hapa.

Alamisha Kumbukumbu Zako, Weka Baadhi ya Kumbukumbu Ziwe za Faragha, na Ongeza Taarifa

Unaweza pia kualamisha kumbukumbu zako unazozipenda za wapendwa wako kupitia Memories app au Memories tab ili uweze kuupata ukurasa wa wapendwa wako kwa urahisi na kwa haraka. Jifunze jinsi ya kufanya hivyo hapa.

Kunaweza pia kuwa baadhi ya kumbukumbu unazotaka kuzifanya kuwa za faragha kwa ajili ya muda mrefu mpaka utakapohisi kuwa tayari kuzishiriki. Kwenye kompyuta yako ya mezani, mchakato ni rahisi.  Bofya kitufe cha kulia cha kipanya ukiwa kwenye picha na menyu itakuja juu ikiwa na orodha ya chaguzi—bofya Make Private kutoka kwenye menyu. Jifunze zaidi kuhusu kufanya kumbukumbu kuwa za faragha hapa.

Mojawapo ya njia bora kabisa ya kufuatilia kumbukumbu zako, ziwe za wazi kwa kila mtu au za faragha, ni kuwatagi wapendwa wako kwenye picha ili iweze kutunzwa kwenye kurasa zao za Memories kwenye Mti wa Familia pia. Wakati kumbukumbu ikiwa ni kwa umma, hii inawaruhusu watu wengine kufurahia kumbukumbu pia. Kuwatagi unaoweza kuwatambua kwenye picha kutakusaidia kufuatilia nani alikuwa nani, na vile vile kusaidia kufanya kumbukumbu iwe na maana zaidi kwa wengine kuiona wanapovinjari Mti wa Familia.

Chaguo jingine linalopatikana kwenye Memories ni kuongeza maelezo kwa kila picha. Unaweza kutoa taarifa za ziada kuhusu nini kinachotokea kwenye picha, shiriki hadithi za burudani zinazohusiana na picha, au andika kuhusu nini picha inamaanisha kwako.

Fanya Onyesho la Slaidi ya Mpendwa Wako

Watu wengi wanafurahia chaguo la kufanya onyesho la slaidi kwa kutumia kumbukumbu za wapendwa wao. Hiki ni kipengele kikuu kinachopatikana kwenye Memories tab au Memories app. Kwenye Memories tab ya mpendwa wako, chagua albamu ambayo ungependa kutumia kutengenezea onyesho lako la slaidi, na picha tofauti au kumbukumbu zitakujia kwa ajili yako kuweka katika utaratibu utakaoupenda. Unaweza pia kushiriki maonyesho ya slaidi! Bofya hapa kujifunza zaidi.

Kama unavyoona, kuna njia nyingi za kuongeza kumbukumbu na kushiriki maisha ya mpendwa wako. Kwa kutenga muda mchache ili kupitia kumbukumbu zako kwenye Memories app au Memories tab kwenye tovuti yetu kutakusaidia kumkumbuka mpendwa wako kwa upendo na kukusaidia kukumbuka nyakati za kipekee ulizokuwa nazo na wapendwa wako.

aboutContributorHeading