
Aplikesheni ya Mti wa Familia
- Jenga mti wako wa familia kwa kutumia simu.
- Tumia vidokezo vya kumbukumbu kujifunza zaidi kuhusu familia yako.
- Ona jinsi unavyohusiana na watumiaji wengine wa FamilySearch.
- Gundua zaidi kuhusu wewe binafsi na familia yako na shughuli za burudani.

Aplikesheni ya kumbukumbu
- Rekodi matukio ya familia na kumbukumbu muhimu.
- Hifadhi picha za familia na zijumuishe kwa watu kwenye mti wako wa familia.
- Kusanya maelezo ya upishi, shajara na kumbukumbu za familia vyote katika sehemu moja.
- Ongeza sauti kwenye picha zako.
Jinsi ya Kupata Aplikesheni
Aplikesheni za Mti wa Familia wa FamilySearch, Kumbukumbu na Jihusishe zinapatikana kwa ajili ya upakuaji kwenye majukwaa mengi.
- Kwa ajili ya iOS au Simu za Apple au Kishikwambi, bofya hapa: Family Tree app, Memories app, na Get Involved.
- Kwa ajili ya Simu za Android au vishikwambi, bofya hapa: Family Tree app, Memories app, na Get Involved.
- Kwa ajili ya Chromebook, bofya hapa: Family Tree app, Memories app, na Get Involved.
- Kwa ajili ya Vishikwamvi vya Kindle au Amazon Fire, kwanza pakua, aplikesheni ya Google Play. Unaweza kupakua the Family Tree app, the Memories app, na the Get Involved app kupitia Google Play.
Vipengele vya Ziada
Kama una muda mchache, aplikesheni za Mti wa Familia, Kumbukumbu, na Jihusishe ni vyombo vizuri sana vya kushiriki katika historia ya familia. Unaweza kuwa umekaa ndani ya ofisi ya daktari au ukingojea chakula cha usiku kiive! Kwa simu yako tu au kifaa cha mkononi, unaweza kuleta utofauti.
Aplikesheni za FamilySearch pia zina vipengele vya ziada ambavyo vinaweza kuwa vya burudani kufanya pamoja na kundi la vijana au kupata uzoefu wa mababu zako.