Wasaidie Mababu Kupokea Ibada Takatifu

famiglia tempio fogli delle ordinanze giovani donne
Mark Romesser

“Hamu yetu tuliyozaliwa nayo ya muunganiko wa familia inakamilishwa pale tunapounganishwa na mababu zetu kupitia ibada takatifu za hekaluni”

(Russell M. Nelson, “Generations Linked in Love,” Ensign and Liahona, May 2010, 92).

Yesu alifundisha kwamba watu wote lazima wabatizwe ili warejee kwenye ufalme wa mbinguni. Unapobatizwa, unaagana na Mungu kufuata mafundisho na mfano wa Kristo. Baada ya kubatizwa, unaweza kuwasaidia mababu zako kufanya ibada takatifu pia. Makala hii itakuongoza wakati kwa maombi unapokusanya taarifa zinazohitajika kuhusu jamaa zako na kutembelea hekalu ili kubatizwa kwa niaba yao.

Unapojiandaa kwenda hekaluni, unaweza kusaidiana na askofu wako ili upate kibali cha hekaluni. Kibali hiki kitakuruhsu kuingia hekaluni na kufanya ubatizo. Punde tu baada ya kuthibitishwa, unaweza kukutana na askofu wako ili upate kibali cha hekaluni.

A missionary helping a new member learn about her ancestors.

Tambua Wanafamilia Gani wa Kuwatumikia

Tafakari kuhusu mababu zako na wanafamilia wa karibu ambao walifariki pasipo fursa ya kubatizwa kwa mamlaka sahihi. Kwa maombi tafakari ni jamaa gani kati ya hawa ungependa kuwatumikia wakati wa matembezi yako ya kwanza hekaluni.

Ndani ya hekalu, wanawake wanaweza kubatizwa kwa niaba ya mababu wa jinsia ya kike na wanaume kwa niaba ya wale wa jinsia ya kiume. Utaweza kufanya ibada kwa ajili ya wale ambao ni wa jinsia sawa na yako, na wanafamilia wengine na marafiki wanaweza kusaidia kufanya ibada kwa ajili ya jamaa zako wengine.

Tumia fursa hii kujifunza zaidi kuhusu jamaa unaowatumikia na tafakari juu ya maisha yao. Unapojiandaa kuwatumikia ndani ya hekalu, unaweza kurejelea kumbukumbu na kushiriki hadithi kuwahusu wao au tafuta hadithi na picha ambazo wengine wanaweza kuwa nazo.

Andaa Taarifa Zinazohitajik

Unaweza kutumia FamilySearch.org ili kukusaidia kukusanya taarifa kuhusu jamaa zako na kuomba kuwafanyia ubatizo.

Illustration showing how to create an account, add family members and print temple cards.

1. Kutengeneza Akaunti ya FamilySearch

FamilySearch.org na program ya Family Tree hutoa akaunti za bure kwa kila mmoja kujifunza kuhusu na kuunganika na familia. Hakikisha unaonyesha kwamba wewe ni muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho unapotengeneza akaunti yako. FamilySearch kisha itakuomba Namba ya uumini wa Kanisa. Unaweza kupata namba hii kwa kuangalia kibali chako cha hekaluni, kumuuliza karani wako wa kata au kumuuliza mshiriki wa uaskofu wako.

2. Kuongeza Wanafamilia kwenye FamilySearch.org

FamilySearch hutumia Family Tree ili kukusaidia kutunza kumbukumbu ya jamaa ambao wamekwishapokea ibada zao na wale ambao bado.

Family Tree, hukuunganisha na vizazi kati yako na jamaa unaotaka kuwatumikia hekaluni. Kwa mfano, kama unataka kufanya ibada kwa niaba ya babu au bibi, kwanza ongeza jina la babu au bibi yako, na kisha muongeze babu au bibi huyo. Ili kuomba kufaya ibada kwa ajili ya mtu fulani, utahitajika kujaza jina la mtu huyo, jinsia, na tarehe na mahali kwa angalau tukio moja, kama vile kuzaliwa, ndoa au kifo.

Screenshot of how to add generations  on FamilySearch Family Tree.

Unapoongeza jina la marehemu, FamilySearch itatoa majibu yanayolandana kama jamaa yako amewahi kuongezwa kwenye Family Tree. Majibu haya yanayolandana yanaweza kukusaidia kuona kama ibada zimekwishakamilishwa kwa ajili ya mtu huyo.

3. Kuomba Kadi ya Jina la Familia

Ndani ya hekalu, kadi za kawaida (ziitwazo “family name cards”) zinatumika kuonyesha ni mtu gani unamfanyia ibada. Baada ya kumuongeza ndugu yako kwenye Family Tree, bofya kitufe cha Ordinances kwenye ukurasa wa mtu huyo ili kuomba ibada kwa ajili yake. (ona mfano hapa chini.)

Requesting ordinances on FamilySearch.

Kama ndugu amefariki ndani ya miaka 110 iliyopita, tafadhali omba ruhusa kutoka kwa wanafamilia wa karibu walio hai wa mtu huyo kabla ya kuandaa kadi ya jina la familia.

Kumbuka: Ni muhimu kuheshimu matakwa ya wanafamilia wengine walio hai pale unapomtumikia jamaa ambaye ni ndugu yenu nyote. Unapoomba ruhusa, inaweza kusaidia kuelezea kwamba huduma ya hekaluni kwa ajili ya wengine hutolewa kwa upendo, na kwamba wale waliofarikiwanaweza kuchagua ikiwa wanakubali ibada hiyo.

Mara baada ya kuomba jina la familia, FamilySearch itakusaidia kuchapisha kadi ya jina la familia au kukupa taarifa ya kupeleka hekaluni kama utahitaji kuchapisha kadi hiyo huko.

Two women serving their ancestors at the temple.

Huduma ndani ya Hekalu

Mahekalu ni sehemu takatifu ambapo tunafaya maagano, kuwatumikia ndugu zetu na kuwa karibu na Mungu.

Ili kufanya uzoefu wako wa kwanza hekaluni kuwa wenye shangwe zaidi, anza kujiandaa kiroho kwa kufunga na kusali na kujifunza kuhusu jamaa utakaowatumikia. Pia unaweza kuwaalika familia, marafiki na washiriki wa kata wahudhurie hekaluni pamoja nawe.

Unapoitumikia familia yako hekaluni, unawea kupokea baadhi ya baraka ambazo mitume wa leo wameahidi:

“Upendo wako na shukrani zako kwa mababu zako utaongezeka. Ushuhuda na uongofu wako kwa Mwokozi utakuwa wa kina na wa kudumu. Na ninakuahidi kwamba utalindwa dhidi ya ushawishi unaoongezeka wa adui”

(David A. Bednar, “The Hearts of the Children Shall Turn,Ensign or Liahona, Nov. 2011, 26–27).

aboutContributorHeading