Kasha la wakati ni chombo kilichojaa vitu mbalimbali kutoka muda fulani ambalo limepangwa kufunguliwa baadaye. Kutengeneza kasha la wakati sio tu njia ya ubunifu na ya kukusaidia kusongesha muda, bali wapokeaji wa baadaye wa kasha la wakati—pamoja na wewe wa baadaye—watakuwa na shukrani kwa ajili ya vidokezo katika nyakati tofauti.
Ingawa unaweza kutengeneza kasha la wakati kutokana na kasha la kale la viatu na vipande vya gazeti vya sasa, kwa nini usilete kasha lako la wakati kwenye karne ya 21 na burudani hizi, mawazo ya kubuni ya kasha la wakati? Mawazo yafuatayo ya kasha la wakati sio ya burudani tu na bila usumbufu, lakini yaweza kufikiwa kwa haraka na kuhifadhiwa kidijitali milele (vile vile kuchapwa na kuhifadhiwa nyumbani kwako kama ukipenda).
Tengeneza Orodha ya Nyimbo
Wimbo unaweza kuturudisha nyuma kabisa kwenye safari ya familia ambako tuliusikia kwa mara ya kwanza, au unaweza kutukumbusha juu ya rafiki mpendwa aliyependa kuimba maneno ya wimbo kwa sauti. Kulingana na wataalamu, Muziki unaweza kurejesha kwa haraka kumbukumbu, hivyo kuufanya uwe kasha zuri la wakati kwa ajili ya uzoefu wetu.

Kutengeneza kasha la wakati la muziki hakuna usumbufu; unaweza kutengeneza orodha ya muziki wa kucheza kwenye jukwaa lako la muziki, au andika orodha ya nyimbo ambazo hugusa kipindi fulani cha muda. Wazo hili la kasha la wakati linaweza kunyumbulika na halina haja ya kujumuisha nyimbo unazozisikiliza sasa hivi, inaweza kuwa na dhima inayolenga watu fulani au uzoefu. Hapa kuna baadhi ya maswali ambayo yanaweza kukusaidia kujua cha kujumuisha.
- Ni nyimbo gani zinazojirudia unazozisikiliza sasa hivi?
- Ni nyimbo gani zinakukumbusha juu ya wazazi wako au rafiki wa karibu au mwanafamilia?
- Ni nyimbo gani unazozisikiliza unapokuwa na huzuni? Vipi kuhusu unapokuwa na furaha?
- Kama ungehitaji kuchagua nyimbo za mwezi uliopita au mwaka, zingekuwa zipi?
Tunza Jumbe za Mtandaoni Uzipendazo
Si kitu kisicho cha kawaida kutunza kadi za zamani za kuzaliwa na barua, lakini vipi mawasiliano kati ya familia na marafiki? Baadhi ya miingiliano ya thamani—na mabadilishano ya kuchekesha sana—yanaweza kutokea kwenye andiko au jumbe.

Mojawapo ya njia rahisi sana ya kutunza mazungumzo haya ni kutengeneza picha zake ndogo kutoka kwenye simu yako au kompyuta na kisha kuongeza picha kwenye albamu ya kidijitali. Iwekee albamu nembo kama “Jumbe za Maandishi Zinazopendwa” au “Jumbe za Familia Ambazo Zinanifanya Nitabasamu.”
Piga picha za Nyumba yako na Mahali Ulikozaliwa
Unaweza kuwa na mamia ya picha kutoka kwenye safari ya likizo, lakini vipi kuhusu maisha yako ya kila siku? Miaka mingi kutoka sasa, unaweza kutamani ungenasa sehemu zinazobadilika kila siku kama vile chumba cha kulala cha binti yako au gari la familia lenye sifa tele.
Tengeneza kasha la wakati la nyumba yako kwa kupiga picha chumba chako cha kulala au tengeneza video ya nyumba. Wazo la kasha la wakati halihitaji kukoma nyumbani kwako tu; chukua picha sehemu unazotembelea kuwinda, au chora ramani ya mji ulikozaliwa na andika muhtasari katika kingo za karatasi kuhusu mgahawa wako unaoupenda na sehemu unazotembelea.

Nasa Fasheni za Hivi Karibuni
Toa kamera yako na mavazi unayoyapenda na anza kupiga picha! Kwa sababu mielekeo ya fasheni siku zote inabadilika, kufungua kasha la wakati la fasheni kutakuwa na maana kubwa ukifananisha wakati huo na sasa. Utajikuta kesho yako ni ya kuchekesha na yenye furaha kwa mielekeo ya zamani na mavazi yaliyopitwa na wakati.
Unaweza pia kukusanya na kutunza picha za fasheni kutoka mtandaoni au kutoka kwenye magazeti, lakini picha za kupiga huwa za burudani zaidi na binafsi zaidi.
Andika kuhusu Kumbukumbu Zako Unazozipenda
Hujachelewa bado kutengeneza kasha la wakati, hata kuhusu vitu ambavyo vilikutokea miaka iliyopita! Anza kurekodi uzoefu na kumbukumbu ambazo kamwe hutaki kuzisahau. Ingawa unaweza kuandika kumbukumbu hizi kwenye karatasi na kuzihifadhi katika sehemu salama, kasha la wakati la kidijitali linahakikisha kwamba rekodi zako hazitaharibika kimwili kupotea nyumbani mwako.
Record My Memories sio tu inatoa ushawishi wa kuandika kwa ajili ya kasha lako la wakati, lakini unaweza kutunza kumbukumbu zako mtandaoni kwenye FamilySearch.org.

Gundua Kasha Lako la Wakati Ambalo Tayari Umetengeneza
Je, ulijua tayari kuna kasha la wakati huko lililotengenezwa kwa ajili yako tu? Uzoefu wa FamilySearch wa All about Me una taarifa za kasha la wakati wote unaohitaji. Kwa ajili ya nyakati tofauti katika maisha yako (kuzaliwa kwako, kwa mfano), uzoefu utakuonesha bei ya gesi, sinema zilizopendwa zaidi mwaka ule na muziki, na habari kuu za wakati ule. Gundua kasha lako la wakati leo!
