Mawazo 7 ya Shajara ya Kukusaidia Kuandika Hadithi Yako

Woman taking notes in a planner
Portrait of a beautiful mixed race woman sitting in an armchair, taking notes in a planner
Impact Photography - stock.adobe

Tunaishi katika nyakati nzuri sana! Tunapopata uzoefu wa kile kinacholetwa na maisha, kuweka kumbukumbu ya shughuli zetu na matukio ya sasa kutatusaidia, vile vile mababu zetu, kuelewa uzoefu wetu. Siku hizi, njia za kutunza shajara zimeongezeka maradufu. Fikiria baadhi ya mawazo ya shajara yafuatayo, na jaribu moja kwa ajili yako!

1. Shajara za karatasi—Utaratibu wa Kawaida

Kama unapenda zaidi desturi ya uzoefu wa shajara, tumia shajara ya kawaida au daftari kuandika hadithi yako. Hata kama unaandika sentensi moja au mbili tu kwa muda, michango yako huleta tofauti kwa mababu zako na kwa ustawi wako binafsi.

Ungeweza pia kujumuisha kalenda, kutengeneza orodha, makala zilizokatwa za magazeti, na vipande kutoka kwenye barua na parua pepe, kuongeza mvuto—takribani kama kitabu cha picha! Weka kumbukumbu kutoka matukio maalumu, kama vile tiketi kutoka maonesho ya muziki, au michezo. Sio tu kumbukumbu hizi zitafanya shajara yako kuwa changamfu, lakini vitu vilivyobuniwa pamoja na sentensi chache kuhusu tukio itafanya kumbukumbu yako iwe hai!

2. Shajara ya Dijitali: Shajara Kiganjani

Shajara haiwezi kuwa tu kalamu na karatasi—shukrani kwa vifaa vya mkononi, shajara yako inaweza kuwa siku zote ndani ya mfuko wako. Moja ya manufaa ya kutunza shajara ya kidijitali ni kwamba unaweza kuandika ukiwa katika mwendo, ukiandika matukio kama yanavyotokea ukitumia simu yako ya kiganjani au kompyuta yako mpakato.

Kuandika shajara kidijitali kunaweza kuwa rahisi kama kufungua nyaraka na kuandika mawazo yako. Fikiria kuongeza orodha, masomo uliojifunza na picha kuifanya shajara lako kuwa hai. Unaweza pia kufanya shajara maalumu ambayo inafokasi kwenye mada moja, kama vile shajara ya shukrani au shajara ya safari.

Hakikisha kuhifadhi faili zako mara kwa mara na zichapishe mara chache. Hatua hizi zitazuia shajara yako kupotea.

Aplikesheni za shajara ya kidijitali zinapatikana ambazo zinakuruhusu wewe kuongeza hali ya hewa na taarifa za sehemu yako, taarifa zilizoandikwa, video na vipengele vingine. Jaribu kutumia aplikesheni za kufuatilia lengo, blogi na akaunti za mitandao ya kijamii kutunza kumbukumbu ya maisha yako. Kuwa mbunifu na ufurahie; uwezekano wa kufanya shajara ya kidijitali ya kipekee kwako hauna mwisho.

mwanaume anaandika shajara kwenye benchi katika chombo chake cha kuandika shajara kidijitali.

3. Shajara ya Kijiografia: Unakwenda Wapi, na Unapenda Kufanya Nini?

Utafiti unaonesha kwamba kizazi kinachoinukia mara nyingi kinahusika zaidi kwenye uzoefu kuliko vitu vinavyoshikika. Kama unapenda kupanda mlima, kuendesha baisikeli, kutembea, au kukimbia polepole, jaribu kurekodi uzoefu wako. Kutunza shajara ya kijiografia ni wazo la shajara ambalo litakufanya uwe hai na kukusaidia kutunza kumbukumbu zilizothaminiwa!

Wataalamu wanaamini kwamba kufuatilia matukio haya na kuyaacha kwa ajili ya vizazi vijavyo kuyaona hutengeneza muunnganiko imara kuliko mtu kusoma tu maneno yako.

Kama wanafamilia wako wanakwenda sehemu zile zile ulizokwenda, wanasoma maneno yako, na kuangalia picha zako, watakuwa na muunganiko imara sana na wewe ambao hauwezi kuwepo kwa njia nyingine yoyote. Unaweza kushiriki shughuli hizi kwenye aplikesheni za mitandao ya kijamii katika njia ambayo inawatia moyo wengine kwenda na kufanya kile ulichofanya. Unaweza hata kufikiri kufuatilia upya safari za mababu zako tena na kuandika kuhusu uzoefu wako.

albamu ya picha ikionesha picha za kihistoria

4. Shajara za Picha: Picha Ina Thamani ya Maneno Elfu Moja

Kuna njia dazani za kutunza shajara ya picha—na, kama kawaida, njia kubwa nzuri ni njia ambayo inafanya kazi kwa ajili yako! Kutumia utaratibu wa kale wa albamu ya picha ni njia moja, kuchapisha kitabu cha picha ni njia nyingine Unaweza pia kutengeneza shajara ya picha ya kidijitali kwa kutengeneza albamu mtandaoni! Sehemu bora ? Kila kitu unachohitaji kipo kwenye simu yako.

Upigaji picha wa kidijitali unafanya iwe rahisi kuendelea kufuatalia lini na wapi picha ilichukuliwa. Unaweza pia kuongeza sentensi moja au mbili kuelezea hadithi kuihusu picha hiyo.

ukurasa kutoka shajara ya doodle

5. Shajara za Doodle: Kuchanganya Maneno na Michoro

Kama unafurahia kuchora, kwa nini usitumie doodle zako kama utaratibu wa kutunza shajara? Becky Christensen, mama na bibi anayefundisha shule huko Japan, anafurahia kuijuza familia yake kuhusu maisha yake kupitia shajara ya doodle.

Chora vitu muhimu ambavyo vilitokea siku nzima, fanya matukio madogo ya kuchekesha ambayo yalitokea, au chora tu mawazo yako. Chochote unachokifanya, fanya shajara yako kuwa ya binafsi na kipekee kwako!

6. Vitabu vya Kumbukumbu vya Mtandaoni: Uwezekano hauna mwisho

Shajara haina ulazima wa kuhitaji kutumia maneno yaliyoandikwa. Kuna njia nyingine nyingi za kutunza kumbukumbu zako, nyingi kati yake ni za bure na rahisi kupatikana kupitia intaneti. Jaribu kufanya Pinterest‑board ya binafsi au orodha ya YouTube ambayo huifadhi nyakati fupi fupi katika maisha yako.

Usiogope kurekodi vitu vya upuuzi, kama vile memes au utani wa kifamilia! Ingawa vinaweza visionekane vya ndani sana, ni sehemu za muhimu za maisha yako ambazo zinahifadhi nafsi yako, moyo wako wa kupenda kujua, na sehemu ya kile ulimwengu ulikuwa wakati wa maisha yako!

shajara ya babu

7. Shajara za Mababu: Kupata Mtazamo wa Kale

Je, una shajara ya babu katika miliki yako? Isome na ujikute umerudishwa kwenye muda wa kale. Kisha jifunze kuhusu kipindi ilipoandikwa kukusaidia kuelewa mazingira ya kile kilichokuwa kinatokea. Unaweza kupata baadhi ya mawazo ya shajara kutoka uzoefu wa mababu zako walioshiriki!

Fikiria kuziweka kidijitali shajara za mababu zako na kuziongeza kwenye FamilySearch Memories ili kuzitunza na kuzishiriki na jamaa.

Vyovyote uamuavyo kutunza shajara, kitu muhimu ni kwamba unarekodi uzoefu wako. Oprah Winfrey wakati mmoja aliandika, “Kuweka shajara kutabadili maisha yako katika njia ambazo kamwe haujawahi kufikiria” Jaribu moja ya mawazo ya shajara hizi kwa ajili yako mwenyewe na kwa wale wanaokuja baada yako.

Baadhi ya makala za mada hii zilichukuliwa kutoka  Matt Misbach’s class, “Geo Journaling,” kwenye Roots Tech Salt Lake City 2020 Convention.

RootsTech inafanyika kila mwaka na ina madarasa kwa wataalamu wa nasaba wa viwango vyote. Kujifunza zaidi kuhusu RootsTech, tembelea mtandao wao au soma makala hii ya blogi.

tagsLabel
aboutContributorHeading