“Maajabu” Kuhusu Ordinances Ready na Usasishaji Mpya

A group of youth attending the temple.

Tangu ilipotolewa mnamo mwaka 2018, aplikesheni ya Ordinances Ready imewazesha watu wengi kote ulimwenguni kupeleka majina ya familia zao wenyewe hekaluni na kufanya iwe rahisi kuhifadhi nafasi kwa ajili ya ibada kuwe rahisi.

Tunapokusanya Israeli jina kwa jina na kutembelea mahekalu yaliyo karibu nasi, usasisho mpya umetolewa ili kufanya uhifadhi nafasi ya ibada kuwa rahisi sana na wenye maana zaidi. Sasa Ordinances Ready itakupatia majina ya watu wa kata na kigingi kwa ajili yako wakati ndugu wa karibu zaidi anapokuwa hawezi kupatikana.

Je, umeshawahi kujiuliza jinsi gani Ordinances Ready inavyopekua majina na kwa nini unapata majina unayotafuta? Ufuatao ni mwonekano wa usasisho mpya na jinsi Ordinances Ready inavyotumia utaratibu maalumu wa kipaumbele ili kukuonyesha majina ya hekalu ambayo yanahusiana nawe—au yanaungana nawe kadiri inavyowezekana.

Kuwasaidia Watu katika Kata na Kigingi Chako Kutumia Ordinances Ready

Wakati Ordinances Ready inapopekua Mti wa Familia ili kupata fursa za hekaluni kwa ajili yako, programu hii hujaribu kupata majina yale ambayo ni bayana zaidi kwanza. Usasisho mpya zaidi kwenye aplikesheni hii huonyesha kwanza, watu wanaohusiana nawe, pili, majina yaliyopelekwa hekaluni na waumini wa kata yako na kigingi chako, na kisha tatu majina yanayotolewa na hekalu.

Screenshot of how to get to the temple menu on the Family Tree App

Screenshot of the Ordinances Ready button on an Android phone.

Screenshot showing successfully found reservations from the Ordinances Ready app

Jinsi Gani Ordinances Ready Inavyopata Majina

Mchakato unaotumiwa na Ordinances Ready hupekua orodha yako ya uhifadhi nafasi, Mti wa Familia na orodha zingine ili kupata uhifadhi nafasi wa ibada uliopo. Inatoa kipaumbele uhifadhi nafasi kwa utaratibu huu:

  1. Uhifadhi nafasi kutoka kwenye orodha yako ya Uhifadhi Nafasi Wangu
  2. Uhifadhi nafasi unaotokana na makundi ya familia yako
  3. Uhifadhi nafasi mwingine ambao umefanywa na wewe
  4. Ndugu zako ambao uhifadhi nafasi wao umefanywa hekaluni
  5. Ndugu zako kwenye Mti wa Familia ambao tayari wamehifadhi nafasi za ibada
  6. Uhifadhi nafasi ambao watu kutoka kata na kigingi chako wamefanya hekaluni
  7. Majina ya jumla ambayo yamepelekwa hekaluni na waumini kutoka kote ulimwenguni

Utakapokuwa unapanga kwenda hekaluni, Ordinances Ready ndiyo njia rahisi ya kupata majina na kuhifadhi nafasi. Inachukuwa dakika chache tu! Tafuta Ordinances Ready kwenye FamilySearch.org, au katika aplikesheni ya FamilySearch yako, bofya kwenye ikoni ya hekalu ili kuijaribu.


aboutContributorHeading