Hifadhi ya Cloud ya Bure kwenye FamilySearch.org kwa ajili ya Kuhifadhi Picha Muhimu Sana za Familia Yako

happy young girls

Siku za Mapunziko, matukio mahsusi, na maisha ya kila siku yanaweza kutengeneza kumbukumbu nzuri sana ya kuwa na familia na kushiriki katika desturi za furaha. Kwa kutumia simu yako kupiga picha za kila kitu ambacho kinatokea imekuwa jambo la kawaida sana. Kweli, simu inaweza wakati mwingine kuwa ya kuudhi. Lakini, kwa kweli fursa za picha bado hazijaisha kama familia haijakusanywa na kutishiwa kusimama kimya wakata mpiga picha akifungua aplikesheni ya picha kwenye simu.

Baada ya kunasa kumbukumbu zako za thamani kwenye simu yako unahitaji sehemu ya pendwa ya kuhifadhia ili uwapendao waweze kuzifurahia kwa miaka, hata vizazi. Kitu kizuri ni FamilySearch ina hifadhi ya cloud ya bure kwa ajili yako kunufaika nayo! Kwa kutumia FamilySearch Memories, unaweza kulinda picha zako za thamani mno bila malipo!

Soma hilo kwa usahihi. Kama una akaunti ya FamilySearch (ambayo ni bure kwa kila mtu na siku zote itakuwa hivyo), una fursa ya hifadhi ya cloud ya bure kwa ajili ya kuhifadhi picha pendwa za familia yako, rekodi za kihistoria na nyaraka zinazorithiwa kizazi hadi kizazi. Hii siyo sehemu ya kutunza picha zako ZOTE (kama vile zile watoto wako wanazopiga wanapoiba simu yako na kupata picha 53 za wanasesere wao); tunataka utunze picha zako nzuri sana na zenye kumbukumbu bora.

mvulana anaendesha baiskeli, kumbukumbu ya kutunza kwenye hifadhi ya cloud ya FamilySearch

Jinsi ya Kutumia Hifadhi ya Cloud ya bure ya FamilySearch

Pamoja na hifadhi ya cloud ya bure ya FamilySearch, inawezekana kupakia picha kutoka chombo chako au kuzichukua kwa simu yako. Mbinu zote mbili zinachukua sekunde chache tu. Ngoja tuangalie kwa ukaribu jinsi inavyofanya kazi. Unaweza kushangazwa jinsi ilivyo rahisi kuanza kujenga historia ya familia yako.

Kupakia Picha kwenye Hifadhi ya Cloud ya Bure ya FamilySearch ambayo Tayari Imetunzwa kwenye Chombo Chako

Acha tuseme ulipiga picha wiki iliyopita, na sasa unataka kuipakia kwenye FamilySearch.org—ili siku zote uwe nayo na kujua wapi ilipo na wanafamilia miaka 50 kutoka sasa waweze kuifurahia. Fuata maelekezo hapo chini. (Kama wewe ni mtaalamu wa FamilySearch, unaweza kuwa na hatua zingine kwa ajili ya kukamilisha kazi hii. Hatua zilizotolewa hapa zitakupeleka sehemu ile ile!)

Kutoka kompyuta mpakato au kompyuta ya mezani

  1. Nenda kwenye FamilySearch.org, na ingia kwenye akaunti yako.
  2. Katika pao la menyu juu ya skrini, bofya Memories.
  3. Katika menyu ya kutiririka chini, bofya Gallery.
  4. Karibu na juu ya skrini, katikati ya ukurasa, bofya ikoni ya kijani ya ongeza (+).
  5. Bofya Choose Files.
  6. Chagua file unayotaka kupakia. Tunazungumza kuhusu kuambatanisha na kuipa picha jina katika muda mfupi.

Pakia Picha Iliyopo au Moja Unayokaribia Kupiga na Simu Yako

Unaweza kupakia picha zilizo tayari kwenye simu yako wakati wowote, au kama uko karibu kupiga picha bora ya wakati muhimu, unaweza kuipiga ndani ya aplikesheni na kupakia mara moja. Hivi ndivyo unavyofanya kwa:

Kutoka simu yako

  1. Fungua Mti wa Familia wa FamilySearch au Memories app.
  2. Tafuta Ikoni ya kijani ya ongeza (+), na bofya. Kama unatumia aplikesheni ya Family Tree, fungua menyu, na bofya Memories, na kisha bofya ikoni ya kijani ongeza ya (+) Unaweza pia kuongeza kumbukumbu kwa babu mahsusi kwa kwenda ukurasa wa mtu, kwa kuchagua Memories tab na kugonga ikoni ya kijani ya ongeza (+).
  3. Bofya Add Photo
  4. Picha zilizopo: Bofya Camera Roll, na chagua picha unayoitamani; bofya Add, na kisha bofya Save.
  5. Picha mpya: Bofya Take Photo, sema “cheese,” na piga picha wakati ule.
    1. Kupakia picha kwenye FamilySearch.org, bofya Use Photo.
    1. Kupiga picha tofauti, bofya Retake.
  6. Unaweza kupunguza au kuipindua, na kisha bofya Save.

Kutagi na Kuipa Picha Jina

Baada ya picha kuwa imetunzwa kwenye ukurasa wako wa FamilySearch Memories unaweza kufanya vitu vingi ili kuifanya kuifanya iwe maana zaidi ya historia ya familia yako.

  • Kwa kuanza , unaweza kuipa picha kichwa cha habari. Kichwa cha habari huongeza muktadha, huwafanya watu wajue nini wanachokitazama, na husaidia unapojaribu kuipekua hapo badaaye.
  • Unaweza kuwa umetagi watu walio kwenye picha ili watu miaka 100 kutoka sasa wawajue ni kina nani.
  • Unaweza kuipa picha tagi ya mada, na picha itatokea wakati watu wengine wakipekua mada hiyo. (Ili kutengeneza picha isionekane kwenye upekuzi nenda kwenye Memories gallery katika tovuti ya FamilySearch. Bofya menyu ya kutiririka chini karibu na Public, na badili mpangilio kwenda Private.)
  • Unaweza kuongeza sauti—kumbukumbu yako au wengine wakizungumza.
  • Unaweza kutengeneza onyesho la slaidi ya kumbukumbu zako ili kushiriki kwenye mitandao ya kijamii au kwenye tukio kama vile dhifa ya kuzaliwa, ndoa au kukutana kwa familia yote.

Kisha tena, labda hii ni zaidi kuliko ulivyotaka kujua. Chaguzi hizi hazimaanishi kukuzidia kabisa. Kusudi lake tu ni kukusaidia wewe na wale unaowapenda kugundua furaha na msukumo kutoka kwenye historia ya familia yako. Zitumie unavyofikiri ni vyema kwako!

Watoto watatu wamekaa na mikono yao kumzunguka kila mmoja

Picha Ina Thamani ya Maneno Elfu

Mara nyingi tunapofikiri juu ya historia ya familia, tunafikiria juu ya miswada mirefu, vitabu na sura nyingi ndani yake, na wasifu wa kila kitu. Picha, ingawa, inaweza kuwa tu yenye kutia moyo, kama vile kuwa na utambuzi. Sehemu muhimu ni, inachukua muda mchache kuongeza moja kwenye Memories gallery.

Kidogo kidogo, picha hizi zinaongezeka. Historia ya familia yako inaanza kuonekana. Pale mwanzo ulifikiri kamwe hutaweza kuwa na muda kutengeneza historia ya familia yenye maana, ya kueleweka, sasa una albamu yote yenye orodha za matukio ya familia —vile vile uhakika kwamba kile ulichokitengeneza kitatunzwa kwa ajili ya vizazi vingi, vingi vinavyokuja baadaye kufurahia.

Hiki ndicho hifadhi ya Cloud ya bure ya familySearch inamaanisha. Tunategemea utanufaika nayo.

aboutContributorHeading