Labda tayari umeshachunguza kumbukumbu zinazopatikana kwenye FamilySearch.org, ambazo hupatikana kwa kubofya mojawapo ya vichupo hapo juu ya ukurasa mkuu. Unaweza kuona chaguo inazotoa kwa ajili ya kuhifadhi picha, nyaraka, hadithi na sauti. Lakini ulijua kwamba kuna programu ya simu ambayo hufanya kuongeza kumbukumbu za familia yako kwenye FamilySearch.org kuwa rahisi na kufaa zaidi kuliko hapo awali?
Ili kupakua programu hii ya bure ya Memories, nenda kwenye FamilySearch.org/blog/sw/mobile. Mara ukiisha isanikisha kwenye simu yako, uko tayari kuendelea!
Unapofungua programu, utaweza kuona ikoni tatu—moja kwa ajili ya picha, moja kwa ajili ya hadithi na moja kwa ajili ya sauti. Ili kujaribu shughuli hizi, bofya mojawapo wa ikoni hizi tatu, na kisha katika kona ya juu kulia mwa programu hii, bofya alama ya + ili kuongeza kitu katika aina hiyo.

1. Picha. Unaweza kuchagua kutoka kwenye picha zilizo tayari kwenye simu yako, au unaweza kupiga picha mpya. Mara unapokuwa na picha kwenye skirini yako, ongeza kichwa cha habari au tagi watu kutoka kwenye mti wako. Kumtagi mtu kutaunganisha picha na mtu huyo kwenye mti. Picha hizo mpya pia zitaoekana katika galari yako ya Kumbukumbu ya FamilySearch.
2. Hadithi. Andika hadithi ya familia moja kwa moja kwenye simu yako. Unaweza hata kuambatanisha picha kuendana na hadithi hiyo, kama ukipenda. Watagi watu ambao hadithi hiyo inawahusu ili kuambatanisha kwenye kumbukumbu yao katika mti.
3). Sauti. Bofya tu ikoni ya + na kisha Anza Kurekodi ili kunasa hadithi ya familia, kumbukumbu, mawaidha au utani. Jaribu kuweka klipu ya chini ya dakika tano ili iwe rahisi kusikiliza (ingawa rekodi zinaweza kuwa ndefu). Mara nyingine tena, tambua klipu hiyo ya sauti inamhusu nani ili kuiunganisha na mtu huyo kwenye mti.

Mojawapo ya vitu muhimu kuhusu aplikesheni ya Memories ni kwamba alimradi umejiunga kwenye Intaneti, mara moja inaongeza habari hiyo mpya kwenye FamilySearch.org. Kama haujaunga kwenye Intaneti, mabadiliko yataongezwa wakati mwingine unapojiunga tena na intaneti.
Kuweza kufanya kazi hizi kutoka kwenye simu yako kunaongeza kiwango kipya cha kunyumbulika cha kuhifadhi kumbukumbu za familia yako. Kwa nini basi usiijaribu? Wakati wa chakula cha jioni kifuatacho, andika hadithi ya Bibi kuhusu kukutana kwake na Babu kwa mara ya kwanza ili vizazi vijavyo viweze kuisikia pia. Piga picha katika mahafali yajayo au hatua nyingine muhimu, na uzipakie kwenye mti ili kuzifanya sehemu ya matukio muhimu ya familia yako uliyoshirikishwa milele. Katika dakika chache tu, wewe unaweza kuhakikisha kwamba hizo kumbukumbu muhimu katika familia yako kamwe hazipotei.
Kwa nyenzo za ziada juu ya hili na mada nyinginezo nyingi, tafadhali tembelea mtandaoni kwenye Kituo cha Msaada.