Wakati mwingine mtumiaji anapojaribu kutazama mahusiano, kitazama uhusiano kinasema "Uhusiano Haujulikani." Hapa ni baadhi ya sababu ya hili kutokea na marekebisho yamkini:
Ruhusa lazima ziwezeshwe
Wakati watumiaji wanapounganika kwa kutumiana jumbe, wanaweza kuona uhusiano wao kwa kila mmoja. Ili kuweza kuona uhusiano, watumiaji wote wawili watahitaji kuwezesha kutazama uhusiano. Nenda kwenye Mipangilio yako, na uwashe Wezesha Kutazama Uhusiano. Hii itakuruhusu wewe na watumiaji wengine kuona uhusiano wao kwako, vilevile mababu wowote wa pamoja. Ruhusa hii haiathiri utazamaji wa uhusiano kati yako na watu katika mti wako wa familia.
Mti wako wa familia unahitaji data zaidi
Kama bado hujaiongeza familia yako kwenye mti, hatutaweza kuwapata ndugu wowote. Utahitaji kuanza moja ili kwamba Mti wa Familia uweze kuwa na taarifa za kutafuta kuhusu wewe.
Kama umeanza mti wa familia, unaweza kuhitaji tu kuongeza vizazi vingine vichache ili kwamba tuweze kupata uhusiano wako kwa wengine. Jaribu kuchukua mojawapo ya ukoo wa familia yako (mababu wa mmoja wa wazazi wako) kurudi nyuma vizazi vichache. Hii itafungua uwezekano zaidi wa uhusiano wa kifamilia na watumiaji wengine.
Hakuna miti ya kutosha
Huenda kusiwe na miti ya kutosha ya familia iliyowasilishwa kutoka sehemu yako mahususi ya ulimwengu. Hii inafanya iwe vigumu kwa Mti wa Familia kuweza kupata muunganiko. Unaweza kusaidia kwa kuwahimiza wengine wenye asili sawa na yako ili kuingiza taarifa zao katika Mti wa Familia wakati ukiendelea kufanyia kazi mti wako mwenyewe.
Mababu zako wa pamoja hawapo katika upeo wa kile kilichohesabiwa
Tazama uhusiano inahesabu uhusiano ndani ya upeo maalumu wa data katika ukoo wako wa familia. Kwa mfano, kama mababu wa pamoja wanaokuunganisha na mtu mwingine walizaliwa kabla ya mwaka 1500 B.K, uhusiano hautapatikana kwa sababu uko nje ya upeo huo.
Ikiwa unaamini kwamba tazama uhusiano inapaswa kuonyesha uhusiano kwa sababu upo ndani ya upeo uliobainishwa, tafadhali wasiliana na Msaada wa FamilySearch.
Makala zinazohusiana
Ninawezaje kutazama uhusiano wangu na mtu katika Mti wa Familia?
Utazamaji wa Uhusiano: Nitawashaje au kuzima uchaguzi wa kuona uhusiano wangu kwa watumiaji wengine?
Ninawezaje kutazama uhusiano wangu na mtu katika Kumbukumbu?
Je, ni kwa jinsi gani mtazamaji wa uhusiano katika Mti wa Familia anaamua kama nina uhusiano naye?