Ninawezaje kutazama uhusiano wangu na mtu katika Kumbukumbu?

Share

Tazama uhusiano wangu inahesabu uhusiano wako na mtu katika Mti wa Familia na kuonesha chati inayoonyesha jamaa wa moja kwa moja kati yako na mtu huyo. Juu ya chati, unaweza kuona uhusiano wako, kama vile Bibi yangu au Binamu Yangu wa Kwanza. Kama hakuna uhusiano uliopatikana, kitazama kinaonyesha "Uhusiano Usiojulikana."

Hatua (tovuti)

  1. Ingia kwenye FamilySearch, na bofyaKumbukumbu.
  2. Bofya Watu.
  3. Tafuta mtu ambaye unataka kuona uhusiano wake.
  4. Chini ya picha ndogo ya mtu huyo, bofya Tazama Uhusiano Wangu. Chati inajitokeza ili kuonyesha jinsi unavyohusiana na mtu huyo.
  5. Kukuza ndani au nje, bofya + au -.
  6. Ili kuonyesha ukurasa wao binafsi kwenye Mti wa Familia, bofya X ili kutoka nje ya tazama uhusiano.
  7. Bofya jina la mtu.

Hatua (app ya Simu ya Mkononi)

Aplikesheni za simu ya mkononi ya Mti wa Familia na Kumbukumbu zinakosa tazama uhusiano kwa ajili ya kumbukumbu. Badala yake tafadhali tumia tovuti.

Hatua (Family Tree Lite)

Family Tree Lite haionyeshi Kumbukumbu wala uhusiano wako na mtu. Badala yake tafadhali tumia tovuti.

Makala zinazohusiana

Ninawezaje kutazama uhusiano wangu na mtu katika Mti wa Familia?
Je, ni kwa jinsi gani tazama uhusiano wangu katika Mti wa Familia inaamua kama nina uhusiano?

moduleTitle