Mti wa Familia hufuatilia mabadiliko yote kwenye taarifa ya babu, ikijumuisha taarifa kuhusu uhusiano. Ikiwa haukubaliani na badiliko, unaweza kulipitia upya na kufanya masahihisho yoyote unayofikiri ni muhimu.
Hatua (tovuti)
- Wakati ukiwa umeingia kwenye FamilySearch, nenda kwenye ukurasa wa Mtu binafsi unayetaka kumwona.
- Ikiwa hauoni Vya Muhimu karibu na juu ya ukurasa, bofya kichupo cha Maelezo.
- Kutengua mabadiliko yaliyofanywa kuhusu mtu huyo, fuata hatua hizi:
- Tafuta kisanduku cha Mabadiliko ya Hivi Karibuni.
- Bofya Onyesha Yote.
- Ili kutengua mabadiliko katika uhusiano wa wanandoa kwa ajili ya mtu huyo, fuata hatua hizi:
- Nenda chini kwenye sehemu ya Wanafamilia.
- Watafute wanandoa, na bofya ikoni yao ya Hariri.
- Bofya Ona Mabadiliko Yote.
- Kutengua badiliko la uhusiano wa mzazi na mtoto kwa ajili ya mtu, fuata hatua hizi.
- Nenda chini kwenye sehemu ya Wanafamilia.
- Mtafute mtoto, na bofya ikoni ya Hariri kwa ajili ya uhusiano wa mzazi na mtoto.
- Bofya Ona Mabadiliko Yote.
- Tafuta badiliko ambalo unataka kutengua. Kama neno Rejesha linatokea upande wa kulia, unaweza kulitengua.
- Bofya Rejesha.
- Kwenye ujumbe unaotokezea ghafla, pitia upya taarifa.
- Bofya Rejesha.
- Kama neno Rejeleo linatokea upande wa kulia, maelezo zaidi yanapatikana:
- Bofya Rejeleo.
- Ili kuona kama chaguo la Rejesha linapatikana, rejelea orodha inayopatikana.
- Ili kuwasiliana na mtumiaji wa FamilySearch ambaye alifanya mabadiliko hayo, bofya jina lake la mawasiliano. Kisha unaweza kutumia mfumo wa ujumbe wa FamilySearch ili kuwasiliana.
Hatua (app. ya simu ya mkononi)
- Kwenye ukurasa wa wasifu wa mtu binafsi, gusa nukta tatu za kulia juu. Kwenye kifaa cha Android, ruka hadi hatua ya 3.
- Kwenye kifaa cha iOS cha Apple, gusa Zaidi.
- Gusa mabadiliko ya hivi karibuni.
- Kama inapatikana, unaweza kubofya Rejesha ili kurejea kwenye taarifa ya awali.
Hatua (Family Tree Lite)
Family Tree Lite kwa sasa haitoi chaguo la kutazama mabadiliko.
Makala zinazohusiana
Je, ninawezaje kurejesha uhusiano uliofutwa katika Mti wa Familia?
Ni kwa jinsi gani ninarejesha kumbukumbu iliyofutwa kwa ajili ya mtu katika Mti wa Familia?
Je, nitatenguaje uunganishaji katika Mti wa Familia?
Ni kwa jinsi gani ninarejesha vyanzo ambavyo viliondolewa kutoka kwenye Mti wa Familia?