Ni nani anaweza kuona na kuhariri watu katika mti wa kundi la familia?

Share

Washiriki wote katika kikundi cha familia wanaweza yote kuona na kuhariri taarifa zote katika mti wa kundi la familia. Hii inawaruhusu wanafamilia wengine, kwa mfano kushiriki picha na kumbukumbu kuhusu kila mtu.

Washiriki wa kundi pia wanaweza kuchagua mtu wao wa kuanzia kwa ajili ya matumizi wakati wanapoonyesha mti wa kundi la familia.

Washiriki wote wa kundi wanapaswa kujua na kufuata miongozo ya faragha, Masharti ya matumizi ya FamilySearch, na kanuni za mwendendo za kundi.

Wachangiaji wanalo jukumu la kuhakikisha kwamba wanayo haki na ruhusa za kushiriki taarifa ndani ya kundi, ikijumuisha taarifa za kibinafsi za watu wengine walio hai.

Watu walio hai

Washiriki wote katika kunsi la familia wanaweza yote kuona na kuhariri taarifa zote katika mti wa kundi la familia.

Hakuna njia yoyote kwa mtumiaji kufungia kumbukumbu zao katika mti wa kundi la familia ili kuwazuia washiriki wengine wa kundi kuzibadilisha.

Mababu walio fariki

Washiriki wote wa kundi wanaweza kuona na kuhariri taarifa za mababu waliofariki ambao wameunganika na watu walio hai katika mti wa kundi la familia.

Tofauti kuu kati ya watu walio hai na watu waliofariki katika mti wa kundi la familia ni kwamba mababu waliofariki wako katika mti wa umma, pale watumiaji wote wa FamilySearch wanaweza kuona na kuhariri taarifa.

Hakuna njia ya kumhamisha mhenga kutoka kwenye mti wa umma ili kwamba kundi la familia pekee ndio waweze kuona na kuhariri.

Watu wa siri

Ikiwa una watu wa faragha katika orodha yako ya faragha, unaweza kuwanakili kwenye mti wa kundi la familia na kushiriki kufikiwa kwa taarifa hiyo na washiriki wa kundi. Hii ndiyo hali ya pekee ambapo mababu waliofariki wanaonekana tu na washiriki wa kundi.

Makala zinazohusiana

Je, ni kwa jinsi gani Mti wa Familia unalinda faragha ya watu walio hai?
Nani anaweza kuona taarifa kuhusu watu walio hai katika Mti wa Familia?
Nani anaweza kuona wasifu wa watu wa faragha katika Mti wa Familia?

moduleTitle