Agosti 2024
Miti ya kundi la familia
Miti ya kundi la familia sasa inapatikana kwa watumiaji wote wa Mti wa Familia. Huhitaji tena kwenda kwenye Maabara ya FamilySearch ili kushiriki mti na wanafamilia wako walio hai.
Uboreshaji wa usimamizi wa kikundi
Kutengeneza, kusimamia, na kushirikiana ndani ya makundi ya familia kumeboreshwa na kutanuliwa. Vikundi sasa vinaweza kushiriki mti, kuchagua mti unaopendelewa, na kubaki na taarifa kupitia kifaa cha kutoa nyenzo cha familia.
null
Julai 2024
Chati mpya ya umbo duara
Tumesasisha chati ya umbo duara wakati tukibakiza vipengele vyote unavyopenda kwa sasa. Mwonekano umesafishwa kidogo.
- Rangi. Rangi zimepunguzwa ung'aavu kidogo. Maandishi sasa ni meusi, ambapo huboresha mwonekanao na usomaji
- Menyu ya hiari. Menyu ya Chaguo hubakiza vipengee sawa, lakini mwonekano wake umesasishwa.
- Mwonekano wa rangi nyeusi. Chaguo la Geuza Rangi limebadilishwa kuwa mwonekano wa rangi nyeusi (Bofya kubadili.) Wakati mwonekano wa rangi nyeusi unapowekwa, chati ya duara pia huwa na mwonekano sawa na huo. Hapo awali, iliwezekana kwenye eneo la nyuma pekee
null
Juni 2024
Mwonekano mpya wa wima
Mwonekano mpya wa wima unaboreshwa katika Mti wa Familia ili kufanya iwe rahisi kwako kuona na kupitia familia nzima na vizazi vingine vya familia kwa mara moja.
null
Machi 2023
Mwonekano wa Rangi Angavu
Katika Mipangilio Yangu ya Mwonekano, Chaguo jipya la mwonekano wa rangi angavu hufanya ukurasa wa mtu kuwa rahisi kusomeka.
null
Januari 2023
- Karatasi ya pembeni ya kuonyesha vyanzo. Sasa unaweza kuona vyanzo vya mtu kutoka kwenye kioneshi cha Maelezo. Katika sehemu ya Zana, bofya Sources. Vyanzo vinaonekana katika orodha kando ya upande wa kulia wa skrini.
- Utafutaji wa vyanzo ulioboreshwa. Sasa unaweza kutagi vyanzo kwa kila aina ya habari katika sehemu za Muhimu na Habari Zingine.
- Mipangilio Yangu ya Mwonekano. Sasa unaweza kupanga upya kioneshi cha Maelezo:
- Unaweza kuchagua kama utaonyesha taarifa katika sehemu za Muhimu na Taarifa Zingine katika safu ya 1 au ya 2.
- Badili mpangilio wa sehemu.
- Vidokezo vya Taarifa. Kila mtu katika Mti wa Familia sasa ana vidokezo vya taarifa ambavyo huwajulisha watumiaji wengine kuhusu uwepo wa maelezo ya utafiti au maonyo ambayo wanapaswa kuyasoma kabla ya kuhariri.
- Mahusiano mengine. Sasa unaweza kurekodi mahusiano kati ya watu ambao hawana mahusiano ya moja kwa moja ya mzazi-mtoto au mwenza
- Uboreshaji wa uchujaji na mpangilio wa kioneshi cha kumbukumbu.
- Kuhusu Kioneshi. Ukurasa mpya wa mtu una kioneshi cha "Kuhusu" ambacho kinatoa njia inayohusisha kujifunza kuhusu mtu katika Mti wa Familia.
Na zaidi! Ona kipi kingine ni kipya.