Je, ni kwa jinsi gani ninajiunga na kundi la familia?

Share

Kila mtumiaji wa FamilySearch anaweza kujiunga na hadi makundi ya familia 10. Ili kujiunga na kundi la familia, wewe lazima upokee mwaliko kutoka kwa msimamizi wa kundi.

Mwaliko huu ungeweza kuja katika njia nyingi tofauti, kama vile barua pepe. Ungeweza pia kupokea mwaliko kupitia ujumbe wa maandishi, au mfumo mwingine wa kutuma ujumbe ambao nyote wawili na msimamizi wa kikundi mnautumia.

Hatua (tovuti)

  1. Pata na fungua mwaliko. Kama ulitumwa kwa baruapepe, hakikisha unaangalia folda lako la taka.
  2. Bofya kiungo katika mwaliko.
  3. Ingia kwenye FamilySearch
  4. Ili kukubaliana na masharti, bofya kisanduku cha kuweka tiki.
  5. Bofya Ndiyo, Jiunge. Mwaliko wako wa kujiunga uko kwenye hali ya kusubiria. Msimamizi wa kundi anahitaji kumalizia kwa kuidhinisha ombi lako.
  6. Wakati idhini inapotolewa, mfumo utajaribu kuoanaisha wasifu wako wa mtumiaji na mtu katika mti wa kundi la familia.
    • Kama utapata wasifu, unaweza kuonyesha kama ni wewe.
    • Kama hautapata wasifu, wewe utapatiwa nafasi ya kuwasiliana na msimamizi kwa ajili ya msaada. Wakati msimamizi anaposema kwamba uko katika mti, bofya Kuanzisha Mtu, na kisha kujichagua mwenyewe kutoka kwenye orodha.

Hatua (app ya simu ya mkononi)

  1. Gusa kiungo cha mwaliko.
  2. Ingia kwenye app ya Mti wa Familia ya simu ya mkononi.
  3. Ili kukubalina na maudhui ya mawasilisho na maafikiano mengine, gusa kisanduku cha kuweka tiki.
  4. Gusa Ndiyo, Jiunge. Mwaliko wako wa kujiunga unasubiria. Msimamizi wa kundi anahitaji kumalizia kwa kuidhinisha ombi lako.
  5. Wakati idhini inapotolewa, mfumo utajaribu kuoanaisha wasifu wako wa mtumiaji na mtu katika mti wa kundi la familia.

    • Ikiwa utapata wasifu, unaweza kuonyesha kama ni wewe.
    • Ikiwa hautapata wasifu, utapatiwa nafasi ya kuwasiliana na msimamizi kwa ajili ya msaada. Wakati msimamizi anaposema kwamba uko ndani ya mti, bofya Kuanzisha Mtu, na kisha jichague mwenyewe kutoka kwenye orodha.

Makala zinazohusiana

Makundi ya familia ni nini?
Je, ni kwa jinsi gani ninatuma ujumbe kwa washiriki wa kundi la familia?
Je, ni kwa jinsi gani ninaondoka kutoka kwenye kundi la familia?

moduleTitle