Menyu ya msaada ya FamilySearch inafanya iwe rahisi kupata msaada unaohitaji unapokuwa unafanya kazi kwenye historia ya familia yako. Jifunze jinsi unavyoweza kutumia menyu kupita vizuizi na kufanikiwa malengo yako.
Msaada Binafsi na Mada Zilizopendekezwa
Menyu ya msaada inapatikana kutoka ukurasa wa tovuti yoyote ya FamilySearch. Ona kwenye kona ya kulia mwa skrini, na bofyamduara mdogo wenye alama ya kuuliza ndani yake. Kijisanduku kidogo cha menyu kitafunguka popote pale ulipo kwenye FamilySearch.org, ambayo inamaanisha kwamba unaweza kutumia sehemu ya msaada bila kuwa na haja ya kufunga ukurasa unaoufanyia kazi.


Juu ya menyu, utaona kijisanduku cha upekuzi. Ingiza maneno muhimu ya mada au changamoto ambayo unataka msaada juu yake, na matokeo ya upekuzi wako yatatokea ndani ya kisanduku cha menyu cha msaada. Tafuta msaada unaouhitaji, na uutumie kwenye kazi iliyopo—bila usumbufu wa kuhama hama skrini.
Chini ya kijisanduku cha upekuzi ni sehemu yenye jina “Suggested Topics.” Viungo unavyoviona pale vyote vimetengenezwa kulingana na mwonekano wa ukurasa wako wa sasa. Tuseme, kwa mfano, kwamba upo kwenye ukurasa mkuu wa FamilySearch.org lakini hujaingia kwenye akaunti yako. Mada zilizopendekezwa zitafokasi kwenye kuliweka upya neno la siri au kupata tena jina la mtumiaji na na mada zinginezo zihusianazo na.
Kisha tena, huenda unafanya kazi katika Mti wa Familia. Katika hali kama hiyo, mada zilizopendekezwa zitakuwa zimelengwa kwenye shughuli au kazi ambazo unaweza kuzifanya kwenye ukurasa ule—kuongeza taarifa kuhusu mwanafamilia, kwa mfano, au kubadili mwonekano au taswira ya chati ya ukoo wako.
Unapofungua menyu ya msaada, tunapendekeza kwamba usiache kuangalia kwenye mada zilizopendekezwa kwanza. Watu mara nyingi wana maswali yanayofanana, na makala ambazo huonekana huwa zimeandaliwa zikiwa na maswali hayo akilini.
Uchaguzi wa Misaada Mingi ya Kuchagua
Wakati mwingine unapokuwa na swali, unataka tu kuzungumza na mtu fulani. Wakati mwingine, sio tu majibu rahisi ambayo unayatafuta bali maelezo au mada ya utafiti kwenye mada ambayo inakupendeza. Katika hali kama hizo, menyu ya msaada inaweza kukuongoza kwenye mwelekeo sahihi.
Muda huu utahitaji kuangalia chini ya mada zilizopendekezwa mpaka chini sana ya kijisanduku cha menyu ya msaada. Pale unaona vitu kadha vya kuchagua. Kila kimoja kinakupeleka kwenye aina tofauti ya msaada. Tumia kile unachokihitaji.

Fikiri juu ya kituo cha msaada kama maktaba ya mtandaoni ya nyenzo za msaada za FamilySearch. Kama mada zilizopendekezwa hazikuwa na kile ulichokuwa unakitafuta na swali la upekuzi wako likakosa kitu, pekua kwenye kituo cha msaada. Taarifa imegawanyika katika aina—Mti wa familia, kumbukumbu na faharasa, kutaja vichache tu. Unaweza kuchagua mada na kuanza kuvinjari yaliyomo. Kutoka kituo cha msaada, unaweza pia kuingia kwenye kituo chetu cha kujifunzia, ambacho kinakupa wewe kozi za bure zilizounganishwa kwenye kompyuta kuu kwenye mada mbalimbali za historia ya familia.
Nyingi za nyenzo zilizopo kwenye kituo cha msaada zilikuwa hapo awali katika lugha ya Kiingereza. Kama ulikuwa unaangalia FamilySearch.org katika lugha tofauti na kiingereza na mada fulani bado haijatafsiriwa, unaweza kuona toleo la Kiingereza badala yake. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Tunakuhakikishia kwamba tunafanya kazi kwa bidii kutafsiri na kupanua maktaba yetu ya nyenzo saidizi kwenye lugha nyingi kadiri iwezekanavyo.

Chaguo la The Community ni kifaa kwa ajili ya kujumuika na wengine ambao wana vitu vinavyoelekeana na wako tayari kushiriki utaalamu wao.
Chaguo la Contacts Us hukupeleka kwenye ukurasa na taarifa kwa ajili ya kuwasiliana na FamilySearch au kutambua moja ya vituo vyetu vingi vya historia ya familia ulimwenguni kote. Waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wataona taarifa ya mawasiliano kwa ajili ya washauri wa hekalu wa kata yao na wa historia ya familia. Katika sehemu hii, pia utapata orodha ya mazungumzo yako ya sasa na ya zamani uliyoyafanya na kitengo cha msaada wa FamilySearch.
Chaguo la The Helper Resources hukupeleka kwenye ukurasa wa FamilySearch ambao ni maalumu kwa wale wanaowasaidia kwenye historia ya familia zao na malengo. Kuchagua chaguo hili hukupa taarifa muhimu kuhusu masasisho kwenye tovuti na nyenzo za FamilySearch unavyoweza kutumia kumsaidia mtu mwingine. Waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho watapata taarifa kuhusu majukumu yao ya kanisa na wanaweza kutumia kitabu cha mipango.
Msaada Upo Njiani
Asante kwa kutenga muda mchache ili kujifunza zaidi kuhusu menyu ya msaada. katika FamillySearch, tunaelewa kwamba ipo siku, kila mwanahistoria wa familia—anayeanza au mtaalamu—anahitaji msaada kidogo. Wakati mwingine ukigonga kizuizi katika historia ya familia yako, usikatishwe tamaa—na kwa uhakika usikate tamaa!
Nenda tu kwenye menyu ya msaada. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba ina kile unachokitafuta. Mwisho kabisa, itakuunganisha wewe na wanaojitolea, huduma kwa mteja, na wasaidizi wengine, wote ambao wanataka kuona unafanikiwa.