Kuanzia 2023, unaweza kuona ujumbe wa kuonesha kosa wakati unapojaribu kuweka nafasi ya ibada kwa ajili ya mtu fulani ambaye ana “Tatizo kuhusu Lugha ya Jina" kwenye taarifa kwenye ukurasa binafsi wa mti wa familia.
Unaweza kuona kosa linalofanana na hilo wakati unapochapisha kadi kwa ajili ya uwekaji nafasi wa sasa au unapojiandaa kupeleka jina hekaluni kama ukurasa wa mtu huyo una tatizo hilo. Katika hali hizi zote mbili, tatizo la "Lugha ya Jina" ni rahisi kurekebishika. Hapa ni namna ya kurekebisha:
- Kama bado hauko kwenye ukurasa wa mhusika kwenye Mti wa Familia, bonyeza kwenye jina ili kuufikia. Kisha nenda kwenye kibao cha maelezo, na kisha bonyeza alama ya penseli iliyo baada ya jina.
- Wakati ukirekebisha jina, angalia ni muswada upi umetumika, na hakikisha mpangilio wa kiolezo cha lugha unaendana na muswada. Kwa mfano, kama umeweka herufi za Kichina kwa ajili ya jina kwenye Mti wa Familia lakini mpangilio wa lugha umewekwa kwa Kingereza au lugha nyingine, utahitajika kubadili kiolezo cha lugha ili kuondoa kutofanana.
Zingatia: Wakati kiolezo cha lugha kinapobadilishwa, unaweza kuhitajika kusogeza jina kwenye sehemu sahihi ya muswada wake. Baadhi ya violezo vya lugha vina miswada tofautitofauti ya uandishi ya kuchagua. - Kama tatizo bado linaendelea, FamilySearch yaweza kuwa pia inagundua kwamba kuna mifumo mbalimbali inayotumika kwenye kuandika kwenye sehemu moja ya jina. Angalia kila sehemu ya kujaza kuona kama kila herufi kwenye sehemu hizo inaendana na mfumo husika wa uandishi, na rekebisha herufi kadiri inavyohitajika. Wakati mpangilio sahihi wa lugha unapochaguliwa, unaweza kuona chaguzi za kuongeza jina lililochapishwa kama utapenda.
Kurekebisha tatizo hili kunasaidia kadi za ibada ambazo zimechapishwa kuonesha jina la mtu kwa usahihi. Pia inaweza kuruhusu mfumo kuonesha utamkwaji wa jina katika lugha zingine. Tazama picha ya skrini hapa chini kama mfano.
Kwa taarifa zaidi kuhusu "Tatizo la Lugha ya Jina" , Soma makala hii.
Katika FamilySearch tunajali kuhusu kukuunganisha na familia yako, na tunatoa uzoefu wa ugunduzi wa kufurahisha na huduma za historia ya familia bila malipo. Kwa nini? Kwa sababu tunathamini familia na kuamini kuwa kuunganisha vizazi kunaweza kuboresha maisha yetu, sasa na milele. Sisi ni shirika lisilo la faida linalofadhiliwa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Ili kujifunza zaidi kuhusu yale tunayoyaamini, bofya hapa.