Baadhi ya vipande bora mno vya historia ya familia yetu huja kwenye umbo la picha. Kuwa na uwezo wa kupiga na kutunza picha za wanafamilia, zamani na sasa, imekuwa sehemu muhimu ya kurekodi hadithi ya familia yetu. Kuna nyenzo nyingi na programu leo ambazo zinafanya iwe rahisi kufanya hivi. Nyenzo mojawapo ya msingi ni Google Photos app. Unaweza kuwa unashangaa, Google Photos ni nini hasa na ni vitu gani vinavyovutia unavyoweza kuvifanya kwa aplikesheni hii?
Google Photos ni programu ya picha ya bure ambayo inafanya kutunza, kusimamia na kushiriki picha zako kuwe rahisi. Moja ya sehemu muhimu ya kuvutia sana ni teknolojia ya utambuzi wa sura ambayo inakuruhusu kutengeneza na kushiriki albamu, kolagi, video hadithi na mengi zaidi. Inatoa hifadhi isiyo na kikomo na ni tofauti na aplikesheni nyingine ya picha.
Mpangilio

Kushiriki kumbukumbu za zmani na wanafamilia inapaswa kuwa thawabu na sio ya kuvunja moyo. Kwa teknolojia iliyopo siku hizi, imefanya iwe rahisi kupiga, kuhariri na kutunza picha kidijitali. Lakini bado watu wanapoteza picha, au wanahangaika kuzipanga. Kujifunza jinsi ya kutumia Google Photos kutakusaidia kufuatilia picha zako zote na kuzipanga, kuhariri na kuzishiriki kwa urahisi.
Kupatikana Kirahisi
Kuna njia mbili rahisi za kupata Google Photos. Kama una simu au tableti, nenda kwenye app store na pakua Google Photos app. Kama una simu ya Android ambayo ni toleo la karibuni, teknolojia hii inaweza kuwa tayari imewekwa ndani ya simu.
Unaweza pia kupata aplikesheni ya picha mtandaoni. Nenda kwenye photos.google.com, na ingia. Kumbuka kwamba baadhi ya utendaji kazi maalumu unaouona kwenye Google Photos ya vifaa vya kiganjani bado haupatikani katika kompyuta.
Chelezo
Sababu nyingine Google Photos ni aplikesheni bora ya picha ni hutoa uhifadhi wa tahadhari (chelezo) wa picha wa haraka, rahisi, na usio na kikomo (mara unapochagua chaguo hili). Kuwa na hifadhi ya tahadhari ya kidijitali wa picha hulinda kumbukumbu hizo zote zenye thamani kubwa mno ulizokusanya kutokana na madhara, kama vile unapofuta faili kwa bahati mbaya au kompyuta yako inapokoma kufanya kazi. Piga picha na kamera ya simu yako, na kisha, unapopata sehemu ambapo WiFi inapatikama, unganisha tu, na fungua programu kwenye simu yako. Kwa ajili ya picha mpaka kwenye 16MP na video mpaka kwenye 1080HD, programu itahifadhi picha zako na video bure kwa ajili ya tahadhari. Unaweza kuzipata kupitia simu yoyote, kishikwambi, au kompyuta, na kuziondoa kutoka kwenye simu yako kama utapenda.

Kumbuka, nguvu ya Google Photos ziko kwenye vipengele vyake.
- Assistant. Kipengele hiki hutengeneza kolagi, uhuishaji, na sinema kwa kutumia picha zako. Kama unazipenda, zitunze tu.
- Photos. Kipengele hiki kimsingi ni cha kusambaza picha zako. Picha zako zote zinatunzwa hapa, zikipangwa kwa mwaka.
- Albams. Unaweza kiurahisi kutengeneza albamu kufuatilia picha ulizopakia. Kipengele hiki pia hufanya picha ziwe rahisi kushiriki na wengine kwa kuwatumia kiungo au kwa kuwaalika kuchangia picha zao wenyewe.

Edit
Google Photos pia ina vifaa vya nguvu vya kuhariri. Mchakato wa kuhariri ni mzuri zaidi, na unaweza kirahisi kutunza mabadiliko yako. Unaweza kuwa umetumia programu ya Picasa hapo zamani, na sasa utendaji kazi wa programu hiyo uko kwenye Google Photos. Aplikesheni hii ni kama kifaa mbadala cha Google.
Search

Teknolojia ile ile ambayo Google inatumia kwa ajili ya upekuzi wake sasa inaweza kutumika kwenye kuchuja picha zako! Kwa utambuzi wa sifa ya uso, Google Photos inaweza kuunda albamu kwa ajili yako. Kirahisi bofya kwenye sehemu ya kupekua, na waunganishe watu au sehemu, na aplikesheni itapanga picha kwa ajili yako. Ni mtunzaji mkubwa wa muda unapokuwa unatafuta picha ya kitu fulani maalumu. Unaweza pia kupekua kwa ajili ya vitu katika picha na kwa ajili ya jumbe katika picha.
Aina bora mno ya kamera ni ile katika mfuko wako! Kwa hiyo ipakuwe, fungua programu na uone maajabu yakitokea. Kwa taarifa zaidi juu ya Google Photos, sikiliza hii mafunzo haya yasiyo na malipo kwenye Legacy FamilyTree Webinar.