Mti wa bure wa mtandaoni ulio mkubwa kuliko yote
FamilySearch inakusaidia kuunganisha wakati uliopita, uliopo na ujao. Tengeneza akaunti ili kujenga mti wa familia, tafuta kumbukumbu za nasaba na hifadhi historia ya familia yako milele bila malipo.

Tracing Your Chinese Roots
Explore the guide
Guangdong Village Finder
Start searching1:59
Endeleza Urithi wa Familia Yako kwa Kutunza Kumbukumbu
FamilySearch ni Nini?
FamilySearch ni shirika lisilo la faida linalotoa huduma za bure kwa kila mtu. Nyenzo zetu tele za historia ya familia zinawasaidia mamilioni ya watu kote ulimwenguni kugundua urithi wa familia zao na kuunganika na wanafamilia.
Timu ya [FamilySearch] ilifanya karakana kupitia Zoom kwa ajili ya Jumuiya ya Vizazi huko Singapore mwaka uliopita, wakitambulisha programu ya FamilySearch na databezi yake pana. Ushiriki wao hai katika kundi la soga huunga mkono washiriki wengi wa GSS katika kutafiri vyanzo vya mababu zao. Ilionesha dhahiri tamanio na utaalamu wa timu kubwa.Lee Khong KeeMkurugenzi wa Maendeleo ya Programu, Jumuiya ya Nasaba Singapore
Ushiriki wa Family Search katika kuweka eneo kwa ajili ya Mwaka Mpya wa Kichina 2022 pamoja na Kituo cha Utamaduni wa Kichina huko Singapore ilishukuriwa sana.
Maktaba ya Shanghai na FamilySearch kwanza walianza kufanya kazi pamoja mwishoni mwa karne ya mwisho na ushirikiano wetu rasmi wa kukusanya, kupangilia, kutafiti na kutoa huduma zinazohusiana na nasaba za ukoo wa Kichina (jiapu) umedumu kwa zaidi ya miaka 20. Nasaba za ukoo huweka nyaraka za ukoo, watu binafsi na matendo ya familia zikishiriki ukoo uleule wa mababu. Ni sehemu muhimu ya urithi wa utamaduni wa mwanadamu na ni vifaa muhimu kwa ajili ya nasaba, utafiti wa kielimu na kujenga utulivu katika jamii. Hii ni sawia na kuelewa nasaba ya FamilySearch.Zhou DemingNaibu Mkurugenzi Aliyepita, Maktaba ya Shanghai
Mti wangu wa familia ulirudi nyuma vizazi vinne pekee, lakini nilijua kwamba baadhi ya ndugu kutoka kwenye ukoo unaofanana huko China ya bara walikuwa na kitabu kikubwa cha nasaba (jiapu). Baba yangu alikuwa amefariki na pia sikumjua ndugu yeyote upande wa bara na sikuwa na njia ya kuwasiliana nao. Mnamo katikati ya Oktoba 2020, niliona kwamba FamilySearch ilikuwa na kipengele kipya cha utafutaji kwa kutumia sifa za kizazi cha mababu zangu na kisha nilifuata ukoo ili kupata majina ya baba yangu, babu yangu na babu yangu mkuu. Nilihisi kama vile nilikuwa kwenye utafutaji wa hazina. Sikuwa nimetambua jinsi gani ukoo wangu ulikuwa mkubwa—watu wenye sifa zinazofanana za kizazi walijaza juzuu nyingi—na ilinibidi nitafute kwa subira ukurasa baada ya ukurasa. Baada ya siku mbili za kutafuta, hatimaye niliipata. Shangwe moyoni mwangu ilikuwa isiyoelezeka. Hakika hii ni hazina kuu.Chang Pei-peiMtumiaji wa FamilySearch, Taiwan




