Katika Mti wa Familia, kipengele cha rudufu yamkini yawezekana kisiorodheshe kumbukumbu rudufu zote za mtu. Ikiwa unajua namba ya utambulisho ya rudufu ambayo haijaorodheshwa, unaweza kuitumia kuunganisha kumbukumbu.
Kabla haujaanza
Pata namba ya Utambulisho ya kumbukumbu zitakazounganishwa. Kumbukumbu zote mbili lazima ziwe katika mti ule ule ikiwa utazihamisha, kwa mfano, zote mbili katika mti wa umma, zote mbili katika mti wako wa faragha, au zote mbili katika mti ule ule wa kundi la familia.
Hatua (tovuti)
- Kwenye menyu ya juu, bofya Mti wa Familia, na kisha bofya Mti.
- Ikiwa inahitajika, badili hadi mti ambao rudufu ziko.
- Tafuta mtu ambaye unataka kumuunganisha.
- Bofya jina la mtu huyo. Katika maelezo ambayo yanajitokeza, bofya jina la mtu huyo tena. Utaongozwa hadi kwenye ukurasa wa mtu huyo.
- Bofya kichupo cha Maelezo ya kina .
- Bofya Unganisha kwa Utambulisho. Inapatikana sehemu ya Vifaa, kando ya upande wa kulia wa ukurasa.
- Ingiza namba ya Utambulisho kwa herufi kubwa na kistariungio.
- Bofya Endelea. Skrini ya kuunganisha inafunguka katika kichupo cha kivinjari kipya.
- Upande wa kushoto: Hii ni rudufu yamkini. Inafutwa ikiwa utaunganisha kumbukumbu.
- Upande wa kulia: Hii ni kumbukumbu uliyoanza nayo. Inahifadhiwa ikiwa utangaunganisha kumbukumbu.
- Amua kama kumbukumbu ni za mtu yule yule.
- Linganisha upande wa kushoto na upande wa kulia kwa ajili ya majina yanayooana, tarehe, mahali, na wanafamilia.
- Soma ujumbe wowote wa onyo kwenye skrini.
- Kama kumbukumbu upande wa kushoto ndizo sahihi zaidi, anzisha tena mchakato wa kuunganisha kutoka kwa ukurasa wa yule mtu mwingine ili kumbukumbu zake zihifadhiwe.
- Kama kumbukumbu si za kuhusu mtu yule yule, bofya Hazifanani. Kama kumbukumbu ni za kuhusu mtu yule yule, bofya Ndio Endelea. Ikiwa hauna hakika, bofya Batilisha.
- Kwenye kumbukumbu inayobaki, pitia tena taarifa zote ambazo zina usuli wa rangi kijani. Taarifa zilizoangaziwa zitanakiliwa kwenye kumbukumbu iliyobaki wakati utakapokamilisha kuunganisha. Ikiwa taarifa hii haitahifadhiwa kwenye kumbukumbu iliyobaki, bofya Tengua.
- Bofya Endelea.
- Malizia kuunganisha:
- Pitia tena kumbukumbu iliyobaki.
- Ikiwa kila kitu kinaonekana kinavyopaswa, bofya Malizia Kuunganisha.
- Ili kuelezea kwa nini kumbukumbu hizi zimeunganishwa, aidha chagua maelezo ya sababu iliyopendekezwa, au ingiza moja ya kwako mwenyewe.
- Bofya Hifadhi.
Mara moja baada ya kuunganisha na kwa muda mfupi, chaguo la “tengua” litapatikana. Inakuwezesha kwa urahisi kuondoa kuunganishwa kwa kumbukumbu 2.
Hatua (Simu ya Mkononi)
- Katika app ya simu ya mkono ya Mti wa Familia, onyesha ukurasa wa mtu wa mojawapo wa kumbukumbu rudufu.
- Kama inahitajika, badili hadi mti ambao rudufu ziko.
- Gusa nukta tatu kwenye sehemu ya juu, pembeni kulia.
- Gusa Rudufu Yamkini.
- Gusa Unganisha kwa Utambulisho.
- Ingiza namba ya Utambulisho kwa herufi kubwa na kistariungio, na uguse Nenda
- Gusa Pitia Tena Kuunganisha
- Soma onyo, na uguse Endelea Kuunganisha. Ukurasa wa kuunganisha unatokea.
- Upande wa kushoto: Hii ni rudufu yamkini. Inafutwa ikiwa utaunganisha kumbukumbu.
- Upande wa kulia: Hii ni kumbukumbu uliyoanza nayo. Inahifadhiwa kama utaunganisha kumbukumbu.
- Amua ikiwa kumbukumbu ni za mtu yule yule.
- Linganisha upande wa kushoto na upande wa kulia kwa ajili ya majina yanayooana, tarehe, mahali, na wanafamilia.
- Ikiwa kumbukumbu upande wa kushoto ndizo sahihi zaidi, bofyaBadili ili kuzitunza badala yake.
- Amua ikiwa utatunza taarifa zo zote kutoka kwa mtu huyu anayefutwa.
- Ili kuhamisha taarifa kutoka kushoto kwenda kulia, bofya Badilisha.
- Ili kuongeza taarifa kutoka kushoto kwenda kulia, bofya Ongeza.
- Kidokezo: Kama kumbukumbu upande wa kushoto zina wazazi rudufu, wenza, au watoto, waongeze kwenye kumbukumbu inayobaki. Unaweza kuunganisha hizi rudufu baadaye.
- Unapomaliza, biringishaa chini upande wa chini wa ukurasa, na uguse Endelea Kuunganisha.
- Ingiza sababu ya kuelezea kwa nini umeunganisha kumbukumbu hizi.
- Gusa Unganisha.
Fahamu: Toleo la iOS la app lina chaguo la Kubadilisha taarifa tu badala ya Kubadili au Kuongeza
Hatua (Mti wa Familia)
Kwa sasa, Family Tree Lite hairuhusu kuunganisha. Ingia kwenye tovuti ya FamilySearch au app ya Mti wa Familia ya simu ya mkononi ili kuendelea na mchakato wa kuunganisha.
Hatua pendekezwa zifuatazo
- Ondoa vyanzo visivyo sahihi au kumbukumbu kutoka kwenye kumbukumbu inayobaki.
- Pitia tena wanafamilia wa mtu huyo ili kuona kama pia wanazo rudufu yamkini.
Makala zinazohusiana
Je, ninaunganishaje kumbukumbu rudufu kwenye Mti wa Familia?
Je, ninawezaje kumpata mtu aliyefariki katika Mti wa Familia?
Je, ninaamuaje kama kumbukumbu 2 katika Mti wa Familia ni za kuhusu mtu yule yule?
Je, nitatenguaje uunganishaji katika Mti wa Familia?