Unaweza kuwapata watu waliofariki katika Mti wa Familia. Unaweza kutafuta kwa jina, jinsia, ukoo, wanafamilia au taarifa za tukio. Unaweza pia kutafuta kwa Utambulisho.
Unaweza kupata watu walio hai katika Mti wa Familia ikiwa tu uliwaweka kwenye Mti na kuwatafuta kwa kutumia Utambulisho.
Kipengele cha Hivi Karibuni kinapatikana baada ya kuingia. Tumia hivi karibuni kufikia kwa haraka maelezo mafupi ya Mti wa Familia uliyoyatazama hivi karibuni.
Hatua (tovuti)
- Ingia katika FamlySearch.org, na fanya moja ya yafuatayo:
- Bofya Mti wa Familia, na kisha bofya Tafuta.
- Bofya Tafuta, na kisha bofya Mti wa Familia.
- Bofya kichupo kwa aina ya utafutaji ambao unataka kuutumia:
- Tafuta kwa Jina. Ingiza jina na taarifa nyingine.
- Unaweza kutumia kadi katika majina ya watu na sehemu. Ingiza* kubadilisha sifuri au herufi zaidi. Ingiza? kubadilisha herufi moja.
- Ili kuona sehemu za ziada za utafutaji, bofya Chaguzi Zaidi:
- Onyesha machaguzi ya utafutaji halisi.
- Ongeza sehemu za ziada kwa ajili ya majina ya ndoa, majina mengine mbadala, jinsia na rangi.
- Ongeza sehemu kwa ajili ya matukio maalumu, kama vile kuzaliwa, ndoa, makazi au kifo. Utafutaji wa tukio la kuzaliwa hupata habari zote za kuzaliwa na za ukristo. Utafutaji wa tukio la kifo hupata vyote taarifa za kifo na mazishi.
- Tafuta Mtu kwa Utambulisho Ingiza Utambulisho wa Mti wa Familia.
- Tafuta kwa Jina. Ingiza jina na taarifa nyingine.
- Bofya Tafuta
- Pitia tena matokeo.
- Kama humpati mtu unayemtaka, badilisha kigezo chako cha utafutaji:
- Katika sehemu ya taarifa upande wa kulia, fanya mabadiliko yako.
- Bofya Tafuta
- Pitia tena matokeo.
- Katika matokeo ya utafutaji, bofya jina la mtu ili kutazama kadi ya mtu.
- Ili kuona wasifu kamili, kwenye kadi ya mtu, bofya jina.
Unaweza pia kutumia kipengele cha Hivi Karibuni kutafuta kwa Jina au Tafuta kwa Utambulisho.
- Bofya Hivi Karibuni.
- Ingiza taarifa katika kisanduku cha Ingiza Jina au Utambulisho.
- Unapoingiza jina, mfumo unatafuta tu majina katika orodha yako ya Hivi karibuni, ikitoa matokeo yasiyozidi 50.
- Unapoingiza Utambulisho na kubofya Nenda, mfumo unatafuta hifadhidata yote ya FamilySearch.
Hatua (app ya simu ya mkononi)
- Kwenye app ya Family Tree ya simu ya mkononi, nenda kwenye mwonekano wa ukoo.
- Gusa ikoni ya Kukuzia.
- Gusa aina ya utafutaji ambao unataka kuutumia:
- Tafuta kwa Jina Ingiza jina. Kama unajua jinsia, gusa aidha Mwanamume au Mwanamke. Kama unataka kuongeza taarifa za kuzaliwa, kifo, au ndoa, gusa katika sehemu sahihi, na ingiza taarifa.
- Tafuta Mtu kwa Utambulisho Ingiza Utambulisho wa Mti wa Familia wa mtu binafsi.
- Gusa Tafuta. Unaona Watu wanaopatikana kwenye Mti wa Familia shirikishi (matokeo yasiyozidi 24).
- Rejelea matokeo ya upekuzi na uguse jina la mtu.
- Kama humpati mtu unayemtaka, gusa kwenye mshale unaoelekeza nyuma mara mbili na rekebisha maneno yako ya utafutaji.
Hatua (Family Tree Lite)
- Ingia kwenye Family Tree Lite (lite.fs.org), na gusa Tafuta.
- Gusa aina ya utafutaji ambao unataka kuutumia:
- Jina Ingiza jina, jinsia, na taarifa zingine.
- UTAMBULISHO Ingiza Utambulisho wa Mti wa Familia wa mtu binafsi.
- Historia Ona watu 50 wa hivi karibuni ambao uliwatazama. Ili kuona mmoja, gusa jina.
- Gusa Tafuta.
- Pitia tena matokeo.
- Kama humpati mtu unayemtaka, bofya Rekebisha Utafutaji ili kurekebisha vigezo vyako vya utafutaji.
- Katika matokeo ya utafutaji, gusa jina la mtu.
Makala zinazohusiana
Ninanakili vipi kiurahisi namba ya utambulisho wa mtu katika Mti wa Familia?
Wapi ninaweza kupata msaada wa nasaba yangu?