Ninaripoti vipi matumizi mabaya, barua taka, barua za ulaghai, kumbukumbu zisizofaa, na maudhui mengine?

Share

Jinsi ya kutoa taarifa ya matumizi mabaya au maudhui yasiyofaa ambayo unakumbana nayo kwenye FamilySearch na kipengele cha Ripoti ya Matumizi Mabaya.

Ikiwa mtu atakutumia ujumbe usiohitajika, unaweza kumnyamazisha mtu huyo. Baada ya hapo, jumbe zao kwako hazionekani tena. Angalia taarifa katika makala Zinazohusiana kwa maelezo.

Ni nini kinachochukuliwa kuwa matumizi mabaya?

Matumizi mabaya, katika hali hii, inafafanuliwa kama nyenzo yoyote inayohifadhiwa kwenye FamilySearch ambayo inachukuliwa kuwa ya kukera au isiyofaa, kama ifuatayo: 

  • Lugha ya kukera au maudhui
  • Taarifa ambazo zinaweza kuwadhuru au kuwaaibisha ndugu walio hai.
  • Viungo kwenda kurasa za nje ya tovuti zilizo na maudhui yasiyofaa
  • Utafutaji wa biashara au huduma za utafiti
  • Bughudha
  • Kauli ya kisiasa
  • Ukiukwaji wa haki miliki

Matumizi mabaya ya FamilySearch pia unahusisha kuweka baraka za patriaki au kumbukumbu rasmi za hekalu katika sehemu yoyote ya hizi:

  • Mijadala
  • Muhtasari
  • Kumbukumbu
  • Historia Fupi ya Maisha

Je, nini hakichukuliwi kuwa matumizi mabaya?

Makosa au mabadiliko katika kumbukumbu hayafikiriwi kuwa matumizi mabaya. Ikiwa una maswali kuhusu makosa yasiyo ya kukusudia au yawezekana kuwa mabaya katika kumbukumbu ambazo huwezi kutatua, tafadhali wasiliana na Msaada wa FamilySearch.

Sera yetu imefafanuliwa katika Taarifa ya Haki na Matumizi ya FamilySearch Rights, inayopatikana chini ya kurasa nyingi kwenye FamilySearch.

Hatua (tovuti)

  1. Nenda mahali kwenye FamilySearch ambapo unaweza kutoa taarifa ya matumizi mabaya:
    1. Zana: Kwenye ukurasa wa Mtu, angalia chini ya Zana kwa ajili ya kiunganishi cha Ripoti Matumizi Mabaya.
      1. - Kwenye ukurasa wa Mtu, chagua kichupo cha Maelezo .
      2. - Katika safu ya kulia, bingirisha chini kwenye sehemu ya Zana.
      3. Katika sehemu ya Zana, bofya Ripoti Matumizi Mabaya.
    2. Kitazamaji cha kumbukumbu: Katika kitazamaji cha kipengee cha kumbukumbu, kwenye kona ya juu kulia, bofya nukta 3 na kisha bofya Ripoti Matumizi Mabaya.
    3. Soga: Bofya jina la mtu karibu na soga, na bofya Ripoti ya Matumizi Mabaya.
  2. Jaza taarifa zinazohitajika, na bofya Wasilisha. Taarifa zote zibaki faragha.

Hatua (app ya simu ya mkononi)

Unaweza kuripoti ujumbe wa kukera ambao unapokea katika Soga ya FamilySearch.

  1. Fungua app ya Mti wa Familia kwenye simu yako.
  2. Gusa ikoni ya menyu.
    • Kwenye kifaa cha iOS cha Apple, gusa mistari 3 sambamba kwenye kona ya chini kulia.
    • Kwenye kifaa cha Android, gusa mistari 3 sambamba kwenye kona ya juu kushoto.
  3. Gusa Soga.
  4. Gusa soga ambayo unataka kuitolea taarifa.
  5. Katika kona ya juu kulia ya dirisha la kidukizo la soga, gusa nukta wima 3, na kisha gusa Ripoti Matumizi Mabaya.
  6. Chagua aina ya matumizi mabaya.
  7. Katika sehemu ya "Ripoti", tafadhali elezea wasiwasi wako.
  8. Ingiza barua pepe yako au namba ya simu. Moja ya chaguzi hizi mbili lazima zijazwe ili kuwasilisha ripoti.
  9. Gusa Wasilisha.

Hatua (Mti wa Familia)

Family Tree Lite inakosa vitufe vya Ripoti Matumizi Mabaya. Hata hivyo, unaweza kubiringisha hadi chini ya ukurasa wowote na kubofya Maoni na Msaada, kisha utume ujumbe kuhusu matumizi mabaya.

Makala zinazohusiana

Ni kwa jinsi gani ninanyamazisha, kuficha au kumzuia mtu kuzungumza nami?
Sheria za mijadala na soga ni zipi?

moduleTitle