Ni kwa jinsi gani ninaongeza namba yangu ya kumbukumbu ya Kanisa kwenye akaunti yangu?

Share

Waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaweza kuongeza namba yao ya kumbukumbu ya Kanisa kwenye akaunti yao ya FamilySearch. Akaunti zilizounganishwa kwenye namba ya kumbukumbu ya Kanisa zina vipengele kwa ajili ya waumini wa Kanisa. Kama hukuongeza namba yako wakati ulipotengeneza akaunti yako, unaweza kuiongeza baadaye. Karani wako wa kata au tawi anaweza kukupatia namba. Namba pia inapatikana katika appya Member Tools.

Hatua (tovuti FamilySearch.org)

  1. Ingia kwenye https://familysearch.org/
  2. Katika sehemu ya juu ya kulia ya skrini, bofya jina lako.
  3. Bofya Mipangilio
  4. Bofya kichupo cha Akaunti.
  5. Ongeza namba yako ya kumbukumbu ya Kanisa kwenye akaunti yako:
    1. Karibu na chini ya skrini, bofya Ongeza Namba ya Kumbukumbu ya Kanisa. Tazama: Kama huoni kipengele hiki, inamaanisha namba yako ya kumbukumbu ya Kanisa tayari imeunganishwa kwenye akaunti yako ya FamilySearch.
    2. Ingiza taarifa:
      1. Jina la kwanza na la mwisho
      2. Tarehe ya kuzaliwa
      3. Sifuri zozote zinazotangulia kama sehemu ya namba ya kumbukumbu ya Kanisa ya tarakimu 11. Alama za deshi hazihitajiki.
  6. Bofya Hifadhi.
  7. Ondoka, na ingia tena. 

Kama utapokea ujumbe wa hitilafu unaoonyesha namba au tarehe yako ya kuzaliwa si sahihi, kuna uwezekano kwamba uliingiza aidha kimoja au vyote visivyo sahihi. Tafadhali:

  • Jaribu kuingiza tena tarehe yako ya kuzaliwa na namba ya kumbukumbu ya Kanisa. Kuwa mwangalifu kuingiza tarakimu sahihi.
  • Hakiki na karani wa kitengo chako ili kuthibitisha kwamba tarehe yako ya kuzaliwa ni sahihi katika kumbukumbu yako ya Kanisa.
  • Hakiki na karani wa kitengo chako ili kuthibitisha kwamba namba yako ya kumbukumbu ya Kanisa ni sahihi.

Hatua (tovuti ChurchofJesusChrist.org website)

  1. Ingia kwenye https://ChurchofJesusChrist.org.
  2. Kwenye sehemu ya juu kulia ya skrini, bofya picha au ikoni yako.
  3. Bofya Mipangilio ya Akaunti.
  4. Upande wa kulia, bofya Uumini.
  5. Ingiza herufi zote 13 za namba yako, ikijumuisha alama za deshi.
  6. Chini ya ukurasa, bofya Hifadhi Mabadiliko.

Baada ya kuongeza namba yako ya kumbukumbu, ingia kwenye tovuti ya FamilySearch.org kwa kwenda kwenye tovuti, bofya Ingia upande wa juu kulia, kisha tumia uchaguzi wa Endelea na Akaunti ya Kanisa.

Hatua (Simu ya mkononi)

Hakuna chaguo katika app za simu ya mkononi la kuongeza namba yako ya kumbukumbu ya Kanisa kwenye akaunti yako. Lazima utoke kwenye app na utumie kivinjari kwenye kifaa chako, na kisha ufuate hatua hapo juu kwa tovuti ya FamilySearch.org au tovuti ya ChurchofJesusChrist.org.

Ujumbe wa “Mtumiaji tayari yupo”

Ujumbe “Unaonekana kama tayari una akaunti ya uumini” humaanisha kwamba namba yako ya kumbukumbu ya Kanisa imeongezwa kwenye akaunti iliyopo. Pengine ulitengeneza akaunti ili itumie bidhaa zingine za kompyuta za Kanisa. Unaweza tu kuongeza namba yako ya kumbukumbu ya Kanisa kwenye akaunti moja. Ona makala inayohusiana hapa chini kwa msaada wa ziada ikiwa namba yako ya kumbukumbu ya Kanisa tayari inatumika.

Makala zinazohusiana

Wapi ninaweza kupata namba yangu ya kumbukumbu ya Kanisa?
Nimesahau nywila yangu ya FamilySearch au jina la mtumiaji
Ninapojaribu kuongeza namba yangu ya kumbukumbu ya Kanisa kwenye akaunti yangu, ninapata ujumbe kwamba namba yangu ya kumbukumbu ya Kanisa tayari inatumika

moduleTitle