Je, ni kwa jinsi gani ninafungua mti wa kundi la familia kwenye kundi la familia lililopo tayari?

Share
Turn on a Family Group Tree in an existing family group
0:00 / 0:00
videoCompanion

Kama wewe ni msimamizi wa kundi la familia, unaweza kufungua mti wa kundi la familia kwenye kundi lililopo tayari. Mti wa kundi la familia huruhusu washiriki wa kundi kujenga na kutazama mti ule ule wa wanafamilia walio hai na pia kuona jinsi wanavyounganika na wahenga wao waliofariki katika mti wa umma.

Kipengele hiki bado hakipatikani katika app iOS ya simu ya mkononi.

Hatua (tovuti)

  1. Kwenye FamilySearch.org Bofya Mti wa Familia.
  2. Chagua Makundi ya Familia.
  3. Bofya kundi la familia.
  4. Bofya Hariri Kundi.
  5. Bofya Ruhusu kundi hili kufanya kazi pamoja katika Mti wa Kundi la Familia.
  6. Soma taarifa za makubaliano, na kisha bofya 2 visanduku vya kuweka tiki.
  7. Bofya Hifadhi.
  8. Bofya Chagua Watu.
  9. Bofya kisanduku cha kuweka tiki katika kibao cha kila mtu ambaye unataka kumjumuisha katika mti wa kundi la familia. Tumia vibonye vya mishale ili kuonyesha ndugu, binamu, mashangazi, na wajomba kwenye chati.
  10. Bofya Nakili kwenye Kundi.
  11. Bofya Endelea hadi kwenye Ukoo.

Washiriki wote wa kundi la familia watatumiwa ujumbe kwamba mti mpya wa kundi la familia unapatikana. Wote wataweza kuona na kuhariri taarifa kuhusu watu walio hai katika mti huu.

Hatua (app ya simu ya mkononi)

Fahamu: Hali unaweza kutengeneza makundi ya familia katika toleo la Android la app ya Mti wa Familia ya simu ya mkononi, hauwezi kushiriki miti ya kundi la familia. Mpaka kipengele hiki kitakapoongezwa kwenye app ya Android ya simu ya mkononi, tunapendeleza kutumia Mti wa Familia kwenye kivinajri cha tovuti badala yake.

  1. Katika toleo la iOS la app ya simu ya mkono ya Mti wa Familia, fungua kipengele cha makundi ya familia.
    • iOS ya Apple: Bofya Zaidi.
    • Android: Katika sehemu ya juu kushoto mwa skrini, gusa laini 3.p
  2. Gusa Makundi ya Familia.
  3. Gusa kundi ambalo unataka.
  4. Gusa ... .
  5. Gusa Hariri Maelezo ya Kundi.
  6. Gusa Ruhusu kundi hili kufanya kazi pamoja katika Mti wa Kundi la Familia.
    • Chaguo hili kwa sasa linapatikana katika toleo la iOS ya app ya Mti wa Familia katika simu ya mkononi.
    • Kama hauoni chaguo hili, unaweza kuhitaji kusasisha app hiyo.
  7. Gusa visanduku vya kuweka tiki kwa ajili ya maafikiano.
  8. Bofya Hifadhi.
  9. Kama kundi litakuwa na mti wa kundi la familia, chagua watu wa kuongeza kwenye mti.

    1. Ili tu kujiongeza wewe mwenyewe kwenye mti wa kundi la familia, gusaNakili Mimi Mwenyewe Tu. Ili kunakili watu kutoka kwenye orodha yako ya faragha, gusa majina, na uguse Nakili Iliyochaguliwa.
    2. Gusa Endelea hadi kwenye Mti.
    3. Gusa Badili.

Makala zinazohusiana

Je, ni kwa jinsi gani nitatengeneza kundi la familia au mti wa kundi la familia?

moduleTitle