Je, ni kwa jnsi gani ninaongeza au kubadilisha taarifa za ndoa katika Mti wa Familia?

Share

Katika Mti wa Familia, mahusiano ya wanandoa huunganisha watu waliooana, ambao waliishi pamoja, ambao pamoja walikuwa na watoto, au ambao vinginevyo walijifikiria wao wenyewe kama wenza.

Matukio ya ndoa yanaonesha pamoja na uhusiano wa wanandoa. Matukio kwa undani huelezea kuanzishwa au kumalizika kwa uhusiano. Unaweza kuongeza, kuhariri na kufuta aina 5 za matukio ya ndoa katika Mti wa Familia:

  • Ndoa
  • Talaka
  • Kubatilisha
  • Sheria ya kawaida
  • Waliishi pamoja

Wanandoa wanaweza kuwa na zaidi ya tukio moja la ndoa. Unaweza kufuta rudufu za tukio.
Matukio ya ndoa huathiri jinsi taarifa katika Mti wa Familia inavyoonesha. 

  • Wakati mtu anapokuwa na zaidi ya mwenza mmoja, wenzi huonyeshwa kwa utaratibu wa muda tukio la ndoa lilitokea.
  • Tarehe ya mwanzo inaonyeshwa katika kisanduku cha wanandoa kwenye ukurasa wa Mtu.

Kiasi cha taarifa za ndoa kinachoonekana kwenye Mti wa Familia kinatofautiana kulingana na mwonekano wa mti.

Hatua (tovuti)

  1. Ingia kwenye FamilySearch na bofya Mti wa Familia. Kisha bofya Mti.
  2. Mtafute mtu aliye kwenye mti.
  3. Bofya jina la mtu. Katika maelezo ambayo yanadukiza, bofya jina la mtu tena.
  4. Bofya Maelezo ya kina kichupo.
  5. Biringiza kwenye sehemu ya Wanafamilia.
  6. Bofya ikoni ya penseli karibu na tukio la ndoa kwa wanandoa.
  7. Ongeza tukio la ndoa:
    1. Bofya Ongeza Tukio.
    2. Bofya mshale wa chini, na bofya aina ya tukio.
    3. Ingiza tarehe na mahali.
    4. Elezea jinsi unavyojua kwamba taarifa ya tukio ni sahihi.
    5. Bofya Hifadhi.
  8. Badilisha tukio lililopo la ndoa:
    1. Bofya ikoni ya penseli kwa wanandoa.
    2. Tafuta tukio lililopo, na bofya ikoni ya penseli.
    3. Fanya mabadiliko.
    4. Elezea jinsi unavyojua mabadiliko uliyoyafanya ni sahihi.
    5. Bofya Hifadhi.
  9. Futa tukio la ndoa:
    1. Bofya ikoni ya penseli kwa wanandoa.
    2. Tafuta tukio lililopo, na bofya ikoni ya penseli.
    3. Upande wa chini kushoto wa skrini ya hariri, bofya Futa Tukio.
    4. Ingiza sababu ya kufuta tukio.
    5. Bofya Futa.

Hatua (app ya Simu ya Mkononi)

  1. Katika app ya simu ya Mti wa Familia, nenda kwenye ukurasa wa Mtu wa mtu binafsi au mwenza.
  2. Gusa Wanandoa.
  3. Gusa ikoni ya penseli karibu na ingizo la Ndoa.
  4. Ongeza tukio la ndoa:
    1. Gusa Ongeza Tukio.
    2. Gusa mshale wa chini, na gusa aina ya tukio.
    3. Ingiza tarehe na mahali.
    4. Gusa Endelea.
    5. Elezea jinsi unavyojua kwamba taarifa ya tukio ni sahihi.
    6. Gusa Hifadhi.
  5. Hariri tukio la ndoa lililopo:
    1. Bonyeza ikoni ya penseli kwa ajili ya tukio la ndoa ambalo unataka kulibadilisha.
    2. Gusa Hariri.
    3. Unaweza kuhariri aina ya tukio, tarehe, na mahali.
    4. Elezea kwa nini taarifa ni sahihi.
    5. Bofya Hifadhi.
  6. Futa tukio la ndoa:
    1. Gusa ikoni ya penseli kwa ajili ya tukio la ndoa ambalo unataka kufuta.
    2. Gusa Futa Tukio la Ndoa
    3. Eleza kwa nini unafuta tukio.
    4. Gusa Futa.

Hatua (Mti wa Familia)

Katika Family Tree Lite, unaweza kuongeza aina 4 za matukio ya ndoa: Ndoa, Talaka, Sheria ya Kawaida, na Kubatilishwa. Tukio la Waliishi Pamoja halipatikani katika Mti wa Familia. Ili kuongeza tukio la Waliishi Pamoja, tumia toleo la wavuti la Mti wa Familia au aplikesheni ya Mti wa Familia.
 

  1. Ingia kwenye Family Tree Lite.
  2. Ongoza kwenye ukurasa wa Mtu wa mtu binafsi au mwenza.
  3. Gusa ikoni ya penseli kwa ajili ya taarifa ya ndoa ya wanandoa.
  4. Ongeza tukio la ndoa:
    1. Katika sehemu ya Matukio ya Ndoa, gusa Ongeza Tukio.
    2. Gusa mshale wa chini, na gusa aina ya tukio la wanandoa.
    3. Ingiza tarehe na mahali.
    4. Elezea jinsi unavyojua kwamba taarifa ya tukio ni sahihi.
    5. Gusa Hifadhi.
  5. Hariri tukio la ndoa lililopo:
    1. Gusa tukio hilo.
    2. Gusa Hariri
    3. Unaweza kuhariri aina ya tukio, tarehe, na mahali.
    4. Elezea jinsi unavyojua kwamba taarifa ya tukio ni sahihi.
    5. Gusa Hifadhi.
  6. Futa tukio la ndoa:
    1. Gusa tukio la ndoa ambalo unataka kufuta.
    2. Gusa Futa.
    3. Eleza kwa nini unafuta tukio.
    4. Gusa Futa.

Masuala ya kiufundi

  • Kama huwezi kuingiza tarehe ya ndoa, inaweza kuwa ni kwa sababu mmoja wa wanandoa hayupo kwenye Mti wa Familia. Wanandoa wote lazima waonyeshwe kwenye Mti wa Familia kabla ya kuweza kuingiza taarifa kuhusu ndoa. Unaweza kumpata na kumwambatisha mwenza au kutengeneza kumbukumbu.
  • Unaona hitilafu: "Hifadhi imeshindikana. Data hizi tayari zipo. Mti wa Familia unakuwezesha kuhusisha tukio moja na tarehe na kuweka muunganiko. Kama toleo moja lipo, huwezi kuongeza lingine ili kulioanisha. Badala yake, futa tukio lisilo sahihi.

Makala zinazohusiana

Ni kwa jinsi gani ninawaweka wenza katika utaratibu wa tarehe ya ndoa katika Mti wa Familia?
Mtu katika Mti wa Familia ana mwenza asiye sahihi
Je, nitarudishaje mahuhusiano katika Mti wa Familia?
Ni kwa jinsi gani ninaonyesha kwamba mtu katika Mti wa Familia hakuwa na watoto au hakuwahi kamwe kuwa katika uhusiano?
Ni kwa jinsi gani ninaonyesha kwamba wenzi katika Mti wa Familia kamwe hawakuwa na watoto?

moduleTitle